Naona Kula Mgahawani ni nafuu kuliko kupika kwa mtu mmoja

Nilivyokuwa bachelor nilikuwa napika mboga kwa staili hii, maharage nusu na nyama nanunua nusu navichemsha hadi viive then naviweka kwenye friji halaf nakuwa naiunga nikiitaji kula, kuku nanunua mzima nampika mchemsho yaani viazi, ndizi,karoti,hoho,kitunguu nachanganyia pamoja naweka kwenye friji in case kama

Siku nimechoka sana napasha kidogo then nakula,hii shughuli nilikuwa naifanya weekend kuandaa ili kuepuka kupoteza muda Sikh za kaz kwa kuwa nakuwa na uchov sana.nikiamua kubadili mboga zaid nanunua samaki waliokwisha kaangwa, chakula n ugali na wali tu
 
Upo kama mimi mkuu
 
Sasa hivi mgahawani msosi wa 2000 unawekewa nyama(tufinyango) moja then msosi wenyewe unachotwa kwenye kibakuli...ila amini ukipika mwenyewe huu mchele nusu unaweza kula kutwa nzima na ukapata wa kuamshia nao kama breakfast.

Nyama ukinunua robo unakula na kuridhika.

Hivyo viungo vya buku huwezi kuvipikia vyote kwa siku moja ,so siku ya pili unapunguza gharama za matumizi.

Ukipika mwenyewe unakula chakula kizuri chenye ladha nzuri sio hao mama ntilie wanaopika michuzi ya masalo
 
Ishu kubwa kwa sisi wanaume inakuja ktk suala la kuosha vyombo mara baada ya kupika. Hapo kunakuwa na kipengele kizito.

Kwenye mapishi wanaume ni wapishi wazuri sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…