Wakuu, mimi nadhani tufike mahali tutafute njia bora ya kuwa na Vyama vya Siasa HAI na BORA katika Taifa letu. Kuwepo na Kanuni, 1. "kwamba Chama cha Siasa ili kiendelea kuwa Chama hai ni budi kiwe na Kiongozi/Viongozi wa kuchaguliwa na Wananchi katika UCHAGUZI MKUU, ndani ya Mihimili yetu (Serikali, Bunge na Mhakama). 2. "Chama cha Siasa ambacho hakikutimiza takwa hilo hapo juu ndani ya miaka kumi (Chaguzi Kuu 2) basi Msajili wa Vyama akiondoe kuwa Chama cha Siasa".
Utaratibu huu utaondoa ile dhana ya kuona Vyama vikubwa vinaunda vyama vyao vidogovidogo (vyama "B", "C".... ), ambavyo kazi yao kuu ni ya-kidalali. Kanuni hii itaokoa fedha nyingi ambayo itatumika kibajeti kwa manufaa ya Nchi.