Naona Mboso anaichukua nafasi ya Aslay....

Chinga One

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
11,469
Reaction score
12,391
Kwa wafuatiliaji wa muziki mtakubaliana na mimi,naona spidi ya Mboso inazidi kushika kasi huku akipenya kila engo ya bongo,hii inamfanya akubalike vizuri sana na kuchukua nafasi ya Aslay ambaye alipata kutamba kwa vibao vyake kadhaa mwaka wa jana na mwanzoni mwa mwaka huu kwa mgongo wa mawingu kwa kupewa promo zilizoshiba lakini ndo hivyo tena lakuvunda.....

Kwa sasa mboso anakimbiza na ngoma yake ya Nipepee noma sana....dogo anajua sana sema kuna mambo madogo madogo anahitaji abadilike asije akazoeleka mapema na kuwafanya mashabikiwakakinai muziki wake kama walivyomkinai Aslay na staili yake ile ile ya kuimba kama anaongea....
 
Bado hajamfikia aslay, ila aslay naona anapotea kidogo kidogo sijajua tatizo ni management yake mpya au anafanya nyimbo zinazofanana kuanzia ujumbe, melody hata sometimes biti watu wamechoka. Ila nae alikosea kutoa nyimbo mfululizo, kama angetoa at least nyimbo nne kwa mwaka naona mpaka sasa angekuwa anatamba.
 
Akiichukuwa nafasi we utafaidika nini
 
hahaaa " wewe jamaa bhana hii mada umeileta" kiushabiki mnooo" by the way mboso wakawaida mnooo" ..katika nyimbo zake zote" kali ni ile Nadekezwa tu pekee"" Kama hiyo ni Pepeee ni ya kawaida mnoo"" ..mboso anasauti nzuri" but anaupungufu" wa utunzi mzuri na Melody " Mkitaka atoboe mwambieni" Harmonies awe anamtungia nyimbo
 
Tuwe objective kidogo, kwenye muziki huwa halibaki ombwe au wengine wanasema pengo, mmoja akipoa mwingine anaibuka na kuitumia hiyo nafasi. Kupoa kwa Aslay ni faida kwa Mbosso! Japo Mbosso sio mkali ila ndio hivyo kakuta nafasi acha aitumie... Aslay ni kama vile ubunifu umefika ukomo, hawezi kubadirika badirika na kiukweli game la bongo usipokuwa na ladha tofauti tofauti, utachokwa tu! Mbosso hawezi kufika mbali kwa kuwa nae somo la kubadirika amefeli.

Kwenye hiyo list yupo pia muimba kaswida almaarufu kwa jina la Lavalava.. WCB wanaoibeba ni Mondi, Harmonize na Rayvanny, hawa wengine wanabebwa na wataendelea kubebwa saaaaana
 
Yan hiyo nipepee tu ndio imekuchanganya hivi mpk umfananishe Aslay na Mboso mbona ni km mbingu na ardhi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…