Nikiangalia jinsi mjadala unavyoendelea juu DP word kuwekeza bandari ya Dar es salaam, nathubutu kusema kweli ubaguzi unaendelea kuwepo Africa, na ndio kizuizi kikubwa Cha maendeleo ya nchi, hivi unathubutu vipi kusema hatutaki DP world kisa ni waarabu na wataleta udini bandarini!
Kwa nilivyoona Mimi kwa namna mtu mwingine anavyochangia mjadala juu anaona Bora ya wangebaki TICTS kwakuwa walilinda kazi zao kama watu wa Imani fulani tofauti na waarabu. Utamshawishi vipi Alie upande wa dini nyingine kuunga mkono hoja Yako? Chama X, kosa Hili munaruhusu sana kulirudia mara kwa mara, mulifanya hivyo uchaguzi wa 2015, na mulifeli, mtu anajiuliza kwa ubaguzi huu, vipi tukiwapa mamlaka kamili?
Kwangu ni Bora CCM ibaki milele ila umoja na utulivu uwepo kuliko Hawa wahubiri mgawanyiko. Ndio maana China ya Mao ilikataa dini, Ndio maana waingereza wakaanzisha Anglicana, ndio maana katika harakati za maendeleo baadhi ya maeneo ya dunia viongozi wa dini waliuwawa. Dini huwa inaleta mgawanyiko baina ya watu na palipo mgawanyiko hakuna maendeleo.
Au ndio tuseme hii kampeni ni ya TICTS ili kufanikisha mpango wao haramu wa kuendelea kutuhujumu? Tuikatae DP World kwa hoja zilizoshiba na sio chuki za kiimani. Sio sawa na hazileti umoja wa kitaifa.