Naona nimpe sunspension kama ya mwezi hivi

Naona nimpe sunspension kama ya mwezi hivi

We jamaa acha upuuzi wa kuja kijiliza hapa. Possibly hizi story zako ni chai tu.
Kwani huyo mwanamke umezaliwa naye, nyie wanaume wa Dar es salaam wapumbuvu sana.
Kumradhi ashakum si matusi
 
mi hata nisingekuja kufungua uzi tayari angekuwa keshapata tiba yake!. maisha sio lele mama kuna muda mtu lazima ujibane tu!.
hakuna tajiri ambae alianza kutafuta mwenyewe na akawa hana nidhamu ya pesa,pesa inahitaji nidhamu kubwa mno na shughuli huwa hainzii kwenye kuitunza tu,ukishaitunza kuna kitu kinaitwa kuizalisha hichi bila maarifa pesa inateketea kama unavyoteketeza kipande cha gogo kwa moto wa kiberiti!..

ndio maana watu walipigania utajiri wao ukiuteketeza lazima nao wakuteketeze!!.
pesa ni jasho,uvumilivu, nidhamu na akili vikikosa hivyo sahau kitu kinaitwa utajiri hata upewe billions utaiteketeza kama bata mrafi anaekula mayai yake mwenyewe!.
 
Endelea kumuendekeza.

Ishi kwa kujiangalia wewe na siyo yeye.

Wewe ukiwa sawa inatosha. Kama anataka hiyo ya 60 mwambie aongeze 10 itimie na kama hana asikusumbue kichwa.

Mwanamke siyo ndugu yako na usilete mazoea kabisa na mwanamke.

Mpe utaratibu wako kama hawezi aondoke akaishi maisha anayoyataka kwa hela zake.

Acha kujitesa kisa mwanamke.
 
We jamaa acha upuuzi wa kuja kijiliza hapa. Possibly hizi story zako ni chai tu.
Kwani huyo mwanamke umezaliwa naye, nyie wanaume wa Dar es salaam wapumbuvu sana.
Kumradhi ashakum si matusi
Wala sio chai tangu mwaka juzi anateswa na demu
 
Kama haelekei kila unalomwelekeza mwache aende huenda kidogo akajifunza uhalisia wa Life akiwa mbali na wewe,
Hawa viumbe sometime wanahitaji uoneshe ubabe kinyume na hapo shekhe wangu wanakuzeesha
 
Wakuu, poleni kwa kuwasumbua sana. Ni vile naipenda familia yangu na pia naipambania sana licha ya mwenzi wangu kutokuwa na shukrani.

Huenda yote haya yanatokana na kuzoeana sana ndani ya nyumba, yaani ile hali ambapo ugomvi huanza, halafu anajua kuwa hata nikinuna, mwisho wake huwa ni mwepesi tu. Kwa hiyo, anajua siwezi kufanya chochote.

Iko hivi wakuu, hapa tulipopanga tunaishi kwenye vyumba ambavyo ni vya shilingi 50,000 na 60,000. Sasa, mwenye nyumba hupokea kodi za mwaka mzima, hana habari ya miezi sita, miezi mitatu, au miezi sita—ni mwaka mzima.

Sasa kwa mimi, kazi yangu ya boda ni ngumu sana kupata hiyo hela kwa muda mfupi. Hunichukua mpaka miezi miwili kuikamilisha. Ni mpambano wa kuvuja jasho haswa, asubuhi hadi kulala saa sita usiku, na hivyo ninamshukuru Mungu sifanyi marejesho sehemu yoyote, ni ya kwangu. Wakati huohuo, mimi napambana na nimefanikiwa kupata kodi ya miezi kumi nikamkabidhi mwenye nyumba na kumsihi anivumilie japo wiki mbili nimalizie laki moja ili iwe laki sita kusudi niwe nimelipia mwaka mzima.

Kumbe huku mwenzangu hakitaki chumba cha shilingi 50,000, yeye anataka cha 60,000.

Ilitokea mvutano kwelikweli, mpaka baadhi ya huduma zilikuwa zimesitishwa. Mwanamke kavimbisha sura, amenuna hadi hivi navyoandika hapa, eti kisa sijalipia chumba cha shilingi 60,000.

Mimi nimejaribu kukaa naye chini kumueleza kuwa mbona kabla sijafukuzwa mishe kule kwa mchina kila kitu kilienda sawa? Iweje hii ndio iwe sababu ya kugombana humu ndani? Hiki chumba kina shida gani, kwani?

Okay basi, kama unaona ni shida na hukipendi chumba, jaza hela yako. Yaani, atoe 120,000, mimi nimalizie ile laki moja niliyoahidi kwa mwenye nyumba. Kama ni rahisi hivyo.

Kuna siku jirani, mama mmoja kamfumbia eti anaosha vyombo vya plastiki tu. Yaani, alivoniambia, hadi nikacheka tu. Nikampa hela akanunue vya udongo. Maisha ya kuigana iguana, ili mradi tutumie hela ovyo, tukose hata akiba.

Nimemueleza kuwa hakuna kitu kizuri kama kuishi kwako sababu una uhuru—unajua upike nini, ule nini. Hii ni tofauti kabisa na ukiwa kwa mama yako; uhuru huna. Ila kama anahisi hapamfai kwangu, mimi ninamrejesha kwao ili nifanye mambo yangu. Nataka nifocus kwenye kazi, ninunue hata kiwanja.
Vijana "wakataa ndoa" wakiona hii tumekwisha
 
Back
Top Bottom