Naona si uungwana kusimamisha Ligi Kuu ili kupisha mechi za kirafiki dhidi ya Mamelodi Sundown.

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Nionavyo tu!

Kusimamisha Ligi( Kusimamisha baadhi ya michezo ya LigiKuu) hasa ya Simba SC na Yanga Sc ili kupisha ombi la Klabu ya Afrika Kusini (Ambao ni Mabingwa wa Afrika) si uungwana kabisa..

Inaonyesha ni jinsi gani tunashindwa kuthamini vya kwetu humu ndani!. Yaani tunashindwa kuwa wazalendo wa vyakwetu kwa malengo ya kuendekeza Jambo ambalo kimsingi halina tija wala umuhimu wowote!

Kuna tetesi kuwa eti wanakuja kwa ajili ya Kampeni ya kupinga Mauaji ya Tembo. (Hiki ni kisingizio cha kipuuzi mno). Kwani sisi tunashindwa nini kutumia hiyo Kampeni kwenye mechi za ligi ?

Nawaza: eti sikumoja itatokea Bingwa wowote yule wa LigiKuu aende Afrika kusini na kusimamisha Ligi ili bingwa huyo wa Bongo aweze kucheza mechi na Kaizer Chiefs na Orlando Pirate.(kwa kisingizio cha Kupiga vita suala fulani).

Nawaasa viongozi wa hivi vilabu kutupilia mbali hili Ombi: Hakuna sababu ya kutengua mlolongo waratiba ili kupisha sulala lisilo la msingi.

Nawaomba pia viongozi wangu wa Vinara wa LigiKuu Bara, Mabingwa watetezi, Mabingwa wa kihistoria wa Tanzania, Dar es salaam Young Afrika Sports Club wazingatie ratiba muhimu iliyo mbele yamashindano na kupuuza kufuata matakwa yasiyo ya Msingi kwa Klabu yetu pendwa.

Mamelodi Sundowns to face Yanga and Simba in friendlies

nawasilisha!
 
Huyu Jamal Malinzi ni jipu sana hapo TFF...

Huyu bora akawe mwenyekiti wa chama cha mpira wa Miguu cha wilaya ya Bukoba.
 
Kama ni Mamelodi ni Vema tu hata Ligi yote ikisimamishwa, kuliko kusimama kwa ajili
ya KOMBE LA MAPINDUZI
 
TFF kwa sasa wanasubiri gate collections.
 
Huyu Jamal Malinzi ni jipu sana hapo TFF...

Huyu bora akawe mwenyekiti wa chama cha mpira wa Miguu cha wilaya ya Bukoba.


ni kweli mkuu!

ila sehemu kubwa ya Maamuzi ya kushiriki kwenye mechi hizo za kirafiki ipo kwa vilabu! Ni vyema vilabu vikazingatia na kuvipa kipaumbele ratiba yake ya msingi.
 
Hapa ndio utaona kama ligi yetu ni armature ama professional. Je, Mamelody walipaswa kufuata kalenda yetu au sisi tufuate kalenda yao?
 
TFF kwa sasa wanasubiri gate collections.


nadhani pengine hii ndio sababu kuu!

Huenda pesa ndio ikawa mshawasho mkuu kwa kukubari kutengua ratiba za ligi ili kupisha Mechi ambazo kwa akili ya kawaida hazina msingi kwa wakati huu!
 
KAMA VIPI HAO MAMELODI WACHEZE NA TIMU ZOOOOTE ZA LIGI! WHY KUSIMAMISHA LIGI KWAAJILI YA SIMBA NA YANGA TU?? HUU NI UDHALILISHAJI WA LIGI YETU
 

nadhani pengine hii ndio sababu kuu!

Huenda pesa ndio ikawa mshawasho mkuu kwa kukubari kutengua ratiba za ligi ili kupisha Mechi ambazo kwa akili ya kawaida hazina msingi kwa wakati hu!

Kuhusu ratiba ya mzunguko wa pili, Manara alisema kama haitabadilishwa ndani ya mwezi mmoja toka ianze atatembea uchi kutoka ofisi za EFM mpaka wapi sikumbuki vizuri.
 
Kama ni Mamelodi ni Vema tu hata Ligi yote ikisimamishwa, kuliko kusimama kwa ajili
ya KOMBE LA MAPINDUZI

mkuu! ni vyema ukatafakari kwa jicho la ziada!

Hii inaonyesha desparation ya kutaka kuonekana kuwa ''umecheza na fulani''...hata pasipo kuwa na sababu ya msingi.

Hivi vilabu (simba na yanga) vinapaswa vikajikita zaidi kwenye Michezo yao ya Ligi kwa kuwa wote wana nafasi ya kutwaa Ubingwa. Hivyo kupoteza muelekea wa ratiba kunaonyesha ni jinsi gani hatuthamini vya kwetu......na kuzingatia cha mwingine...

Umeona wapi kuna mechi ya kirafiki inayotokea na Ligi nzima inasimamishwa kupisha timu moja inayotoka nje kuja kukamilisha ratiba yake ya mechi za kirafiki?
 
Kuhusu ratiba ya mzunguko wa pili, Manara alisema kama haitabadilishwa ndani ya mwezi mmoja toka ianze atatembea uchi kutoka ofisi za EFM mpaka wapi sikumbuki vizuri.



ni kweli hata mimi namuunga mkono katika hiko kiapo chake!

ila itakuwa ''Unafiki Mkubwa'' kama Klabu yake itaridhia kuvurugwa kwa ratiba ili kupisha Mechi ya kirafiki ambayo haina faida yeyote kwa kilabu.
 
Jamani waacheni tu maana mwaka wa 5 sasa mechi za kimataifa wanazisikia kwa majirani zao Yanga na Azam
 
Hapa ndio utaona kama ligi yetu ni armature ama professional. Je, Mamelody walipaswa kufuata kalenda yetu au sisi tufuate kalenda yao?

mkuu!

hapo ndio nimechanganyikiwaa kabisa!

Yaani makaburu wanakuja na ratiba yao hapa, wanaikabidhi kwa viongozi wa vilabu vyetu ili waifuate ratiba hiyo yao na kuachana na ratiba kuu ya Ligi....

nimeshangaa sana aisee!
 
Jamani waacheni tu maana mwaka wa 5 sasa mechi za kimataifa wanazisikia kwa majirani zao Yanga na Azam
Hili si la Uyanga na Usimba!

linahusu vilabu vyote ....simba ....yanga....na azam.
 
Hakuna tatizo, kucheza na bingwa wa vilabu barani, ni fursa


Inaaminika kila ''FURSA'' inawakati wake...

Je hata kama ukiwa na Jambo muhimu la kufanya ni vyema ulitelekezena kufuata fursa.?

Ina maana ''Fursa'' ya Kucheza na Mamelodi Sundown ni kubwa kuliko ''LigiKuu Tanzania Bara.''?
 
Mkuu umeielewa comment yangu?
Ebu irudie tena kuisoma alafu angalia ulichocomment
nimekuelewa sana ulichokiandika..

hapa hatuzungumzii mechi za kimataifa za Yanga na Azam ambazo wamekuwa wakishiriki....
unazungumzia kuvurungwa kwa ratiba ya ligikuu ili kupisha ratiba ya klabu ya Mamelodi sundown ifanyiwe kazi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…