Zamani za kale mtu anakuomba kazi unampatia na anafanya vizuri sana.
Sasa hivi mtu ni lazima ajulikane na aletwe na mtu anayejulikana na mwenye kuthaminika na mwajiri mwenyewe.
Mtu anakuja kwa unyenyekevu kuomba kazi hasa kazi za Taasisi Binafsi, kumbe huyo mtu ni Jambazi au Gaidi, au Mwizi au Mchawi.
Matokeo yake atampa hasara kubwa mwenye Taasisi au Kampuni husika.
Pata fani yako kuwa mwaminifu katika kazi yako, watu watakuona na kukuunganishia kazi hata kama hujaitafuta.
Mala nyingi bosi akinunua Maroli mapya huwa ananiagiza
"Lete Mtembezaji Sasa"
Akimaanisha Dereva Mwaminifu na Mahiri.