Uchaguzi 2020 Naona wote wanapiga tu chenga, watuambie sisi vijana tunapataje ajira au tunajiajirije

Uchaguzi 2020 Naona wote wanapiga tu chenga, watuambie sisi vijana tunapataje ajira au tunajiajirije

yuda75

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2020
Posts
520
Reaction score
1,385
Naona wote wanapiga tu chenga watuambie sisi vijana tunapataje ajira au tunajiajirije wakati mikopo kwa ujasiriamali kupata vigezo ni vingi pia riba kubwa

Watuambie wananchi wa kipato cha chini wanaishije, watuambie kuhusu afya na mazingira rafiki ya kibiashara yako wapi.

Si kutupa shuhuda za kupigwa risasi au shuhuda za kuongeza ndege na kuzunguka na wasanii, tumechoka shuhuda za maneno mengi wenye vyeo washibe maskini walie.

We are tired
 
Umenena vyema kila mmoja ameangalia katika angle yake! Magufuli anaamini katika kutengellneza njia ili kila mwenye juhudi ajipatie Riziki. Hili limefanyika katika kuboresha miundombinu, kuwaruhusu wakulima kupanga bei za mazao yao, Watumishi wa umma kula jasho lao, uboreshaji wa huduma za afya ili wakapige kazi.

Tundu Lissu; anatusimlia jinsi alivyojenga urafiki na malaika wa kifo, anatuahidi kulipa malimbikizi ya mishahara pamoja na Kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma, wakati huo huo anapinga ukusanyaji wa kodi na kutaka kuipunguza, anaponda vyanzo vya mapato anazungumzia matumizi...

MWAROBAINI WA AJIRA KWA VIJANA KUAJIRIWA AU KUJIAJIRI NI

Kuufumua mfumo wa elimu ya nadharia na kujikita kwenye mfumo wa elimu wa vitendo.

Ikiwa ni pamoja na kuanzisha somo la ufundi kwa shule za msingi kuanzia darasa la sita hadi kidato Cha nne.

Kuzigeuza ofisi za kata badala ya kuandika barua za dhamana, ushahidi nk. Ziwe ni centre kwa ajili ya kumobilize vijana katika kuanzisha na kushiriki kwenye shughuli za maendeleo.
 
naona wote wanapiga tu chenga watuambie sisi vijana tunapataje ajira au tunajiajirije
wakati mikopo kwa ujasiriamali kupata vigezo ni vingi pia riba kubwa

watuambie wananchi wa kipato cha chini wanaishije
watuambie kusu afya na mazingira rafiki ya kibiashara yako wapi

si kutupa shuhuda za kupigwa risasi
au shuhuda za kuongeza ndege na kuzunguka na wasani
tumechoka shuhuda za maneno mengi wenye vyeo washibe maskini walie

we are tired
Nikuambie tu Hakuna kipindi nchi hii kumekua na ajira nyingi kama awamu hii

Tanzania nzima kwa sasa Hakuna wilaya isio na mradi mkubwa wa serikali iwe ni wa barabara, madaraja makubwa, reli, umeme vijijini, miradi mikubwa ya maji, ujenzi wa bandari, ujenzi wa vivuko na meli, ujenzi wa miradi ya kufua umeme, ujenzi wa majengo makubwa ya serikali/binafsi na viwanda vipya vingi

Hizi sector zimetoa ajira kubwa sana nchini na kiwango cha chini kabisa unskilled labor kwenye hii miradi niliotaja analipwa 400k kwa mwezi.
 
Nikuambie tu Hakuna kipindi nchi hii kumekua na ajira nyingi kama awamu hii

Tanzania nzima kwa sasa Hakuna wilaya isio na mradi mkubwa wa serikali iwe ni wa barabara, madaraja makubwa, reli, umeme vijijini, miradi mikubwa ya maji, ujenzi wa bandari, ujenzi wa vivuko na meli, ujenzi wa majengo makubwa ya serikali/binafsi na viwanda vipya vingi

Hizi sector zimetoa ajira kubwa sana nchini na kiwango cha chini kabisa unskilled labor kwenye hii miradi niliotaja analipwa 400k kwa mwezi.
hawo ni vibarua na sio ajira za kudumuuu mkuu tofautisha panga na kisu
 
hawo ni vibarua na sio ajira za kudumuuu mkuu tofautisha panga na kisu
Ndio lakini katika hii miradi mingi ni ya kuanzia miaka mi3 kuendelea, bado ni mda mrefu kufikia malengo yako hasa ukizingatia serikali kwenye hii miradi inasimamia sana maslahi ya watanzania, kwa hiyo miaka mitatu kuendelea hata ukija kupokea mafao yako NSSF bado haitakua sawa na bure

Kuna wafanyakazi nawajua walikua ni unskilled labor kwenye hii miradi niliotaja, pamoja na huo mshahara wa 400k kwa kiwango cha chini kwa mwezi, wamepokea mafao yao baadhi, wengi walikuwa na million 5 just for 3 years, hiyo pesa ni nyingi kwa mwenye akili ya maisha.
 
Nenda wilayani kwenu kapambane mkuu....kuna mikopo inatoka ya vijana bila riba.

Hata huko wilayani hiyo mikopo haitoshi ni kupambana kuupata. Ajira ni tatizo la Dunia sio Chadema wala CUF wanaoweza kulitatua...labda kulipunguza tu.

Usikae hapo na kulia lia ukitegemea kuna meanasiasa atakuja na ajira za wahitimu wote. Wenyewe wanapambania familia zao kwanza.

Acha lawama tafuta namna ya kujikwamua. Ukishapata pakujishikiza ndiyo uwaze kuanza kupiga kelele.
 
Back
Top Bottom