Uchaguzi 2020 Naongea na vijana wenzangu

ELIZAYO LAMU

Member
Joined
May 5, 2020
Posts
11
Reaction score
24
Niliandika makala hii 2017 mnasemaje kuelekea uchaguzi 2020

POLENI SANA VIJANA, MNAKUWA MAJESHI YA MINYUKANO YA KISIASA MWISHO INAKUWA AIBU KWENU.

Poleni sana vijana wa ACT - WAZALENDO mliomtukana matusi yote Mh Mbowe kisa mapenzi makubwa mliyonayo kwa Mh Zitto pengine hamkujua wanasiasa hupatana wakati wowote kwa maslahi yao wakitumia mwamvuli wa utaifa .Poleni sana vijana wa ACT WAZALENDO pengine hamkutambua vita ya ZZK ilikuwa dhidi ya uboss wa chama kuliko demokrasia ndani ya chama.

Poleni sana vijana wa CDM mliomtukana sana Mh ZZK kumfurahisha Mh Mbowe pengine hamkujua usaliti, umamluki na kutumika kwa ZZK kuivuruga CDM ni mpishano wa maslahi kati ya mabaunsa wawili ZZK Vs Mbowe ninyi mkaingia kichwa kichwa , poleni sana vijana wenzangu.

Poleni sana vijana wa CHADEMA mliomtukana mzee LOWASSA matusi ya aina yote kuwafurahisha viongozi wenu wa chama pengine hamkujua kwenye siasa zetu hakuna msafi wala mchafu mbele ya maslahi, poleni sana vijana wenzangu sasa msafisheni mpendwa wenu ili kudumisha furaha ya viongozi wenu

Poleni sana vijana wa NCCR-MAGEUZI , CUF na CHADEMA mlionyukana kwa hoja, matusi, ngumi na kejeli kila kundi likijinasibu kuwa chama cha upinzani imara vingine ni matawi ya CCM, poleni sana hamkujua viongozi wetu hubadilika kama kinyonga, sasa pendaneni na kuungana mkono kwa amri ya viongozi wenu maana siyo ruhusa kuuliza maumivu na mateso mliyopata enzi za minyukano yenu

Poleni sana vijana wa ACT WAZALENDO hasa kigoma mliofanya dhambi ya kumtibulia ubunge Mh David Kafulila kisa amejiunga na watu wasiopendwa na kipenzi chenu ZZK , mlimshambulia sana kijana wa watu eti kajiunga na Mbowe mbaya , mlitengeneza T-shirt za michambo, mlimzomea kwenye kampeni hamkutambua ipo siku ZZK nae atakaa meza moja na Mbowe. Poleni sana vijana kwa kutenda dhambi ya uonevu bila kujua ugomvi wa wanasiasa hukoma kwenye maslahi yao natambua mnajiona wenye dhambi usoni mwa Kafulila

Poleni sana vijana wa CUF mnaopigana na kunyukana vikali kisa prof Lipumba na Maalim Seif nawaonea huruma maana siku ya kupatana kwao itakuwa rahisi kuliko mnavyodhani ninyi majeshi yao , mtaambiwa wekeni silaha chini mkiwa na nguvu na ari kubwa ya kupambana na prof Lipumba msaliti wala hamtaamini maneno matamu ya JJ MTATIRO dhidi ya prof Lipumba hakika mtashikwa na butwaa. Poleni sana vijana endeleeni kuwadharilisha viongozi wa CUF wenye ugomvi wao wakipatana mtaomba radhi

Poleni sana vijana wa upinzani mlioungana na viongozi wenu kumtukana matusi yote Mh JK KIKWETE pengine hamkujua hakuna kiongozi mzuri usoni mwa wapinzani wa Tanzania, poleni sana vijana nina hakika mioyo yenu inawasuta kwa kuingia kwenye vita ya kumshambulia kiongozi pasipo kujua ni suala la msimu tu sasa unganeni na viongozi wenu kumlilia na kumkumbuka kwa wema wake .

Poleni sana vijana wa CCM mliomtukana sana Dkt Emanuel Nchimbi matusi yote mpaka kufanya press conference kumchafua , poleni sana vijana pengine hamkujua siasa ni kuchagua na kuchagua siyo dhambi huenda mlidhani kuonesha mapenzi yake kwa mgombea ampendae ni kosa sasa mnamtazama kwa jicho la aibu poleni sana vijana wenzangu.

Poleni sana vijana wa vyama vyote mnaorushiana maneno kisa Mh Nape na Mh Paul Makonda pengine hamjui kwenye kazi kuna kupishana mitazamo, nawaonea huruma sana hamjui wao ni marafiki tena wote ni watoto wa baba mmoja na wanafanya kazi chini ya boss mmoja. Poleni sana vijana endeleeni kutafunana ipo siku mtaona aibu kuwatazama kwa maneno yenu mnayotamka.

Poleni sana vijana CCM mnaoshambulia wabunge wa CCM eti ni wasaliti kwenye vita dhidi ya dawa za kulevya pengine hamjui wabunge wanatimiza wajibu wao kikatiba , ipo siku mtajidharau na kujiona wakosaji poleni sana vijana endeleeni na kejeli kwa wabunge wa CCM ipo siku mtawazama kwa aibu.

Poleni sana vijana kwa ujumla, nawapa pole nyingi sana ninyi ni majeshi ya wanasiasa vigogo mnakuwa vinara wa kushambulia wakati mwingine hata hamjui kiini cha minyukano ya vigogo, mnapigana kwa moyo wote, mnawakejeli mahasimu wenu mpaka mnaacha utu wenu mwisho wanasiasa wanapatana kwa muda wao pasipo hata kufikria matokeo ya vita mliyopigana kwa niaba yao.

Binafsi nawapa pole wala siwezi kusema mnatumika kisiasa hapana ni mapenzi yenu yanawaponza, mna mapenzi ya kweli kwa viongozi wenu ndiyo maana mnapata tabu kufanya maamuzi sahihi kujiepusha na minyukano isiyo wahusu.

LAMU ELIZAYO PASCAL KILIMBA
lamuelizayo@gmail.com
+255766033331
 
What is your point now?? MTU akikosea watu wasitoe madukuduku yao? Unataka vijana wawe dormant kwenye mambo yahusuyo mstakabali wa siasa za taifa lao??
Tofautisha kuingilia mahusiano binafsi ya kimapenzi na kuingilia mitizamo ihusuyo maisha ya kilasiku na hoja za kimaendeleo katika siasa,uchumi ama jamii.
Erevuka kidogo mtoto taifa lenye vijana lonyalonya na walozubaa unavyotaka/ulivyo ni taifa mfu. Kwani hupendi watu wapatanage? Pole yanini unapomchana mjinga? Hapa nakuchana upunguze uzembe kwahivyo ukibadilika Mimi napewa pole au hongera?!?
Bora uufiche huu ujinga wako, hili ni jukwaa la fikra kubwa alafu unajianika majina na namba kwamba unapoint unaeza tumiwa salio na MTU ama??
 
Maneno meeeeeeeeeengi.....,
1. Kavae barakoa
2. Kanawe mikono
3. Una hela wewe? Nyuzi zenye tag ya uchaguzi 2020 hatusomi Kama hujaweka namba yako ya simu, na Kama huja print t dhirt, kanga na vitenge
 
Niliandika makala hii 2017 mnasemaje kuelekea uchaguzi 2020

POLENI SANA VIJANA, MNAKUWA MAJESHI YA MINYUKANO YA KISIASA MWISHO INAKUWA AIBU KWENU.
Binafsi nawapa pole wala siwezi kusema mnatumika kisiasa hapana ni mapenzi yenu yanawaponza, mna mapenzi ya kweli kwa viongozi wenu ndiyo maana mnapata tabu kufanya maamuzi sahihi kujiepusha na minyukano isiyo wahusu.

LAMU ELIZAYO PASCAL KILIMBA
lamuelizayo@gmail.com
+255766033331
Mkuu Mwanangu Elizayo, asante kwa mada hii fikirishi.
P
 
[emoji124][emoji124][emoji124]

Sent using [emoji106]
 
LOooh, hawa ndio vijana!
Nimechoka kwenye mstari wa tano.

Itapendeza sana kama vijana uliolenga wakusome watapata muda wa kusoma hadi huko mwisho.

Nikuulize swali: hivi kule CCM hakuna vijana; au sikufikia sehemu uliyowaandika wa huko?

Na akina..., nani yule jJulia, au sijui nani, naibu waziri wa matunguri, sijui Shonza, huko kwenye makundi yako umemweka kundi gani; kwa maana naye alikuwa kati ya hao unaowaandika hapa, akina Mwa(nani sijui?) wako wapi?

Nilitaka kukupa ushauri...; nasita kufanya hivyo kwa sasa.

Potelea mbali, ngoja nitoe huu wa laini laini.

Usiandike kumchosha unayetaka asome ulichoandika.
 
Sifanya ubaguzi wa chama nimesema wote unaweza kupitia uone
 
What is your point now?? MTU akikosea watu wasitoe madukuduku yao? Unataka vijana wawe dormant kwenye mambo yahusuyo mstakabali wa siasa za taifa lao??
Tofautisha kuingilia mahusiano binafsi ya kimapenzi na kuingilia mitizamo ihusuyo maisha ya kilasiku na hoja za kimaendeleo katika siasa,uchumi ama jamii.
Erevuka kidogo mtoto taifa lenye vijana lonyalonya na walozubaa unavyotaka/ulivyo ni taifa mfu. Kwani hupendi watu wapatanage? Pole yanini unapomchana mjinga? Hapa nakuchana upunguze uzembe kwahivyo ukibadilika Mimi napewa pole au hongera?!?
Bora uufiche huu ujinga wako, hili ni jukwaa la fikra kubwa alafu unajianika majina na namba kwamba unapoint unaeza tumiwa salio na MTU ama??
Nadhani hujaelewa vema
 
Niliandika makala hii 2017 mnasemaje kuelekea uchaguzi 2020

POLENI SANA VIJANA, MNAKUWA MAJESHI YA MINYUKANO YA KISIASA MWISHO INAKUWA AIBU KWENU.

Poleni sana vijana wa ACT - WAZALENDO mliomtukana matusi yote Mh Mbowe kisa mapenzi makubwa mliyonayo kwa Mh Zitto pengine hamkujua wanasiasa hupatana wakati wowote kwa maslahi yao wakitumia mwamvuli wa utaifa .Poleni sana vijana wa ACT WAZALENDO pengine hamkutambua vita ya ZZK ilikuwa dhidi ya uboss wa chama kuliko demokrasia ndani ya chama.

Poleni sana vijana wa CDM mliomtukana sana Mh ZZK kumfurahisha Mh Mbowe pengine hamkujua usaliti, umamluki na kutumika kwa ZZK kuivuruga CDM ni mpishano wa maslahi kati ya mabaunsa wawili ZZK Vs Mbowe ninyi mkaingia kichwa kichwa , poleni sana vijana wenzangu.

Poleni sana vijana wa CHADEMA mliomtukana mzee LOWASSA matusi ya aina yote kuwafurahisha viongozi wenu wa chama pengine hamkujua kwenye siasa zetu hakuna msafi wala mchafu mbele ya maslahi, poleni sana vijana wenzangu sasa msafisheni mpendwa wenu ili kudumisha furaha ya viongozi wenu

Poleni sana vijana wa NCCR-MAGEUZI , CUF na CHADEMA mlionyukana kwa hoja, matusi, ngumi na kejeli kila kundi likijinasibu kuwa chama cha upinzani imara vingine ni matawi ya CCM, poleni sana hamkujua viongozi wetu hubadilika kama kinyonga, sasa pendaneni na kuungana mkono kwa amri ya viongozi wenu maana siyo ruhusa kuuliza maumivu na mateso mliyopata enzi za minyukano yenu

Poleni sana vijana wa ACT WAZALENDO hasa kigoma mliofanya dhambi ya kumtibulia ubunge Mh David Kafulila kisa amejiunga na watu wasiopendwa na kipenzi chenu ZZK , mlimshambulia sana kijana wa watu eti kajiunga na Mbowe mbaya , mlitengeneza T-shirt za michambo, mlimzomea kwenye kampeni hamkutambua ipo siku ZZK nae atakaa meza moja na Mbowe. Poleni sana vijana kwa kutenda dhambi ya uonevu bila kujua ugomvi wa wanasiasa hukoma kwenye maslahi yao natambua mnajiona wenye dhambi usoni mwa Kafulila

Poleni sana vijana wa CUF mnaopigana na kunyukana vikali kisa prof Lipumba na Maalim Seif nawaonea huruma maana siku ya kupatana kwao itakuwa rahisi kuliko mnavyodhani ninyi majeshi yao , mtaambiwa wekeni silaha chini mkiwa na nguvu na ari kubwa ya kupambana na prof Lipumba msaliti wala hamtaamini maneno matamu ya JJ MTATIRO dhidi ya prof Lipumba hakika mtashikwa na butwaa. Poleni sana vijana endeleeni kuwadharilisha viongozi wa CUF wenye ugomvi wao wakipatana mtaomba radhi

Poleni sana vijana wa upinzani mlioungana na viongozi wenu kumtukana matusi yote Mh JK KIKWETE pengine hamkujua hakuna kiongozi mzuri usoni mwa wapinzani wa Tanzania, poleni sana vijana nina hakika mioyo yenu inawasuta kwa kuingia kwenye vita ya kumshambulia kiongozi pasipo kujua ni suala la msimu tu sasa unganeni na viongozi wenu kumlilia na kumkumbuka kwa wema wake .

Poleni sana vijana wa CCM mliomtukana sana Dkt Emanuel Nchimbi matusi yote mpaka kufanya press conference kumchafua , poleni sana vijana pengine hamkujua siasa ni kuchagua na kuchagua siyo dhambi huenda mlidhani kuonesha mapenzi yake kwa mgombea ampendae ni kosa sasa mnamtazama kwa jicho la aibu poleni sana vijana wenzangu.

Poleni sana vijana wa vyama vyote mnaorushiana maneno kisa Mh Nape na Mh Paul Makonda pengine hamjui kwenye kazi kuna kupishana mitazamo, nawaonea huruma sana hamjui wao ni marafiki tena wote ni watoto wa baba mmoja na wanafanya kazi chini ya boss mmoja. Poleni sana vijana endeleeni kutafunana ipo siku mtaona aibu kuwatazama kwa maneno yenu mnayotamka.

Poleni sana vijana CCM mnaoshambulia wabunge wa CCM eti ni wasaliti kwenye vita dhidi ya dawa za kulevya pengine hamjui wabunge wanatimiza wajibu wao kikatiba , ipo siku mtajidharau na kujiona wakosaji poleni sana vijana endeleeni na kejeli kwa wabunge wa CCM ipo siku mtawazama kwa aibu.

Poleni sana vijana kwa ujumla, nawapa pole nyingi sana ninyi ni majeshi ya wanasiasa vigogo mnakuwa vinara wa kushambulia wakati mwingine hata hamjui kiini cha minyukano ya vigogo, mnapigana kwa moyo wote, mnawakejeli mahasimu wenu mpaka mnaacha utu wenu mwisho wanasiasa wanapatana kwa muda wao pasipo hata kufikria matokeo ya vita mliyopigana kwa niaba yao.

Binafsi nawapa pole wala siwezi kusema mnatumika kisiasa hapana ni mapenzi yenu yanawaponza, mna mapenzi ya kweli kwa viongozi wenu ndiyo maana mnapata tabu kufanya maamuzi sahihi kujiepusha na minyukano isiyo wahusu.

LAMU ELIZAYO PASCAL KILIMBA
lamuelizayo@gmail.com
+255766033331
Mkuu,
Sijui ni mimi tu naona pole zimekuwa nyingi sana kwa vijana... lakini sijaona 'conclusion' ya huu uzi. Kwa hio ulitaka kusema nini baada ya kuwa pole?
 
Dah....wanasiasa wote ni ndugu....wanapigania maslahi ya matumbo yao....waswahili wanasema....ndugu wakigombana shika jembe ukalime [emoji41]

Sent using Beretta ARX160
 
Poleni sana vijana mnaodhani Mh. Membe anaweza kuwa mpinzani.
Pole nyingi umezitoa kwa vijana wa upinzani na ndio lilikuwa lengo lako, huko kwingine umetoa pole kinafiki. Matumbo yanaponza vichwa. Hivi sisi Watanzania nani katuroga??????????
 
Upuuzi mwingine huu.

Back
Top Bottom