Napambana na uraibu wa kutamani wanawake

Napambana na uraibu wa kutamani wanawake

Mungu akusaidie, jitahid uwe muwazi Kwa Mungu Kwa kuomba pia, utavuka,

Sababu tabia kabla haijatoka nje kuonekana, inaanza ndani( mbegu)
Wahi mapema kabla haijaota, ife hiyo mbegu ndani omba toba, na ombea malango yako ya ufahamu.

Hakuna awezaye
 
Moja ya kitu kinachonisumbua ni kuwa mimi ni mraibu wa wanawake.

Ni kitu nilicho dhani nimesha kishinda, ila baada ya kupata vijisenti juzi kati nimejikuta automatically hii hali inanijia hasa kwa hatari mbaya sana...

Napenda sana wanawake, nikiona mwanamke mrembo, mwenye uzuri wa umbo mpaka sura, nachanganyikiwa kabisa. Ndo maana Mungu hataki niwe maarufu mapema, huenda ningelitumia umaarufu huo kama yule jamaa aliye trend sijui nchi gani ile.

Imagine leo kuna jirani kahamia nilipopanga Kaja na mchumba wake, aisee sijui nini hiki nimetoka leo nje nakutana nayo imejifunga kanga. Sijui ni nini nikajikuta nimeifikia tu na kuanza kuipigisha stori kama sio mke wa mtu..

So nipende kumshukuru Mungu kwa kuliweka swala hili katika awareness yangu. Ndugu zanguni ndo maana makosa kupiga hatua, kukaa Natamani wanawake bila aibu kabisa. Hili ni pepo nalikemea katika jina la yesu.

Sasa namowmba Mungu anisaidie nisiwe mtu wa kutamani, ngono na wanawake hasa wenye waume zao. Kwa kweli ukitaka kujua udhaifu wako pata pesa. Yaani deep subconscious pattern inarudi kwa nguvu mpaka najiuliza huku ni kurogwa ama?

Hata kinacho tokea nchini unashangaa mtu yuko madarakani despite uchafu unao tokea nje! Sio kwamba haoni bali ile nguvu ya pesa inakufanya kuwa beast.

Enyi ndugu zangu msisite kuniweka katika maombi niachane na hii dhambi mbaya ilioambatabishwa katika amri kumi za Mungu.

Niwatakie weekend njema na Mungu awabariki. 🙏
Umerushiwa roho ya uzinzi ili iharibu sifa yako. Kupo kupenda wanawake kawaida kunako sababishwa na tamaa zako mwenyewe lakini kupo kupenda wanawake hovyohovyo kunako sababishwa na roho ya uzinzi. Mwombe Mungu aliye ziumba Mbingu na Nchi katika jina la Yesu atakusaidia kuondoa roho ya uzinzi utakua sawa.
 
Back
Top Bottom