Napaswa kurudisha Passport kwa kuwa nimeshindwa kusafiri?

Patriot3

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2022
Posts
336
Reaction score
553
Kuna wakati nilipata nafasi ya masomo nje. Nikatafuta passport. Mwishowe nikashindwa kwenda masomoni kwa sababu Fulani.

Kama utaratibu kuwa na sababu ya kusafiri ndo upewe, hainibidi kuwarudishia? Maana sikusafiri. Just thinking loudly.
 
Hapana. Hupaswi kurudisha passport kwani passport ni hati yako ya kusafiria, hata kama husafiri unaweza kuiweka hadi siku utakaopata safari. Passport ni kwaajili ya kwenda popote pale. Inakutambulisha tu wewe ni nani na raia wa nchi gani. Ni tofauti na visa ambayo inakupa uhalali wa kuingia katika nchi fulani kwa kusudi fulani kama vile kutalii, kusoma, biashara, n.k. Visa inabandikwa kwenye passport. Unaweza kuwa na passport usiwe na visa, ila huwezi kuwa na visa bila passport.
 
Daah nimecheka sana sasa msomi tena huoni kuwa ni haki yako kuwa na Passport kwa hiyo ukichukua Leseni usipoendesha gari kwa muda fulani unatakiwa uwarudishie leseni yao ukitaka kuendesha gari ukaombe tena hapo kazi ipo aisee...CAG lete report tena Watanzania na wabunge wao washangilie...
 
Ile ya kusema kuwa lazima uwe na safari ndio uombe passport ni kuthibiti uwingi wa waombaji. Kila mtu anatakiwa kuwa nayo kwa safari ya dharura. Mfano umeumwa ghafla na unatakiwa kwenda matibabu nje ya nchi. So pasi ya kusafiria ni haki ya kila raia, awe na safari kwa Sasa au asiwe nayo
 
Hapana. Hupaswi kurudisha passport kwani passport ni hati yako ya kusafiria, hata kama husafiri unaweza kuiweka hadi siku utakaopata safari. Passport ni kwaajili ya kwenda popote pale. Inakutambulisha tu wewe ni nani na raia wa nchi gani. Ni tofauti na visa ambayo inakupa uhalali wa kuingia katika nchi fulani kwa kusudi fulani kama vile kutalii, kusoma, biashara, n.k. Visa inabandikwa kwenye passport. Unaweza kuwa na passport usiwe na visa, ila huwezi kuwa na visa bila passport.
Ahsantee kwa Somo.
 
Kuna wakati nilipata nafasi ya masomo nje. Nikatafuta passport. Mwishowe nikashindwa kwenda masomoni kwa sababu Fulani.

Kama utaratibu kuwa na sababu ya kusafiri ndo upewe, hainibidi kuwarudishia? Maana sikusafiri. Just thinking loudly.

Kwamba unaitaka 150k yako sio?
 
Ile ya kusema kuwa lazima uwe na safari ndio uombe passport ni kuthibiti uwingi wa waombaji. Kila mtu anatakiwa kuwa nayo kwa safari ya dharura. Mfano umeumwa ghafla na unatakiwa kwenda matibabu nje ya nchi. So pasi ya kusafiria ni haki ya kila raia, awe na safari kwa Sasa au asiwe nayo
Passport sio kitambulisho cha taifa ile ni kitambulisho cha kimataifa na kukipata ni lazima uwe na sababu ya kuvuka mpaka wa nchi kwenda nje, kuna watu hawana mpango wa kusafiri nje sasa unampa kitambulisho sasa hivi cha nini, siku atakayopata sababu ya kusafiri basi ataomba na atapata hata iwe dharura passport kwa hali ya dharura kama matibabu zinatolewa haraka sana ndani ya saa 24 tu. Katika hili nawaunga mkono uhamiaji wasitoe passport bila sababu ya safari.
 
Saa 24 kwenye ugonjwa ni nyingi sana. Kila MTU ana haki ya kuwa nayo. Dunia ni kijiji siku hizi
 
Hata hiyo rufaa ya hospitali mpaka kukamilika na kupewa documents ni masaa mengi tu wala usiweke kichaka cha muda hapo.

Kila mtu ana haki ya kuwa na passport muda wowote autakao ila ni lazima uwe na sababu ya safari. Hata kama dunia ni kijiji lakini wapo watanzania wasiokuwa na uhitaji wa safari muda huu sasa unawapa passport ya kazi gani.
 
Kuna wakati nilipata nafasi ya masomo nje. Nikatafuta passport. Mwishowe nikashindwa kwenda masomoni kwa sababu Fulani.

Kama utaratibu kuwa na sababu ya kusafiri ndo upewe, hainibidi kuwarudishia? Maana sikusafiri. Just thinking loudly.

Ili serikali wa ifanyie nn
 
Hivi mtoa mada unafahamu kazi ya passport lakini?
 
Back
Top Bottom