Napata choo lakini hakitoki

kingkongtz

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2019
Posts
1,058
Reaction score
3,613
habarini ndugu zangu

sina tatzo la bawasiri wala sina tatzo la kukosa choo ,ni hali imenitokea hivi karibuni

ipo hivi

nilisafiri kwenda burundi siku 3 kabla ya Christmas.
Ni mara yangu ya kwanza kwenda huko,chakula cha kule kiufupi kilinishinda ikawa ni mwendo wa nyamachoma tu na biscuits,hata kunywa maji ilikuw nadra sbb tulipokuw ilikuw porini sana.

sasa toka Christmas hadi leo nmerud Tanzania sijajisaidia yapata siku 4

haja huwa naisikia ila nikienda uani nikichuchumaa wakat nasukuma nasikia kama jiwe na maumivu makali sana,

msaada jamani kwa wenye uzoefu
 
Nenda duka la dawa lolote, nunua laxatives, e.g Castor oil, unywe, utatoa uchafu wote ila ukae na msuli masaa kama 6 hv, alafu uje ushukuru JF.
Nakazia. Kuna dawa nyingi tu zinauzwa pharmacy na tena hazihitaji cheti cha dr. Unakunywa kilingana na unavyotaka kuharisha au kupata choo. Ukitaka kupata choo kilaini unakunywa kidogo, na ukitaka kuharisha sana unakunywa nyingi. Kuna hii: Polyethylene glycol-electrolyte solution. Dukani zinauzwa zikiwa na branda name tofauti tofauti, lakini ukimwambia muuzaji unataka hii atajua. Ni ya unga na unaweka kwenye maji halafu unakunywa.
 
Ishawahi nitokea nlipoenda pima hospital nikaambiwa nina dalili za vidonda vya tumbo nkapewa dawa za kutumia mwez mzima....nikawa fresh
 
boss hapo kwenye kukaa na msuli masaa 6 unaweza nifafanulia
Utakuwa unaharisha mara kwa mara, tupa suruali au bukta mbali kaa karibu na choo, huelewi msuli… wale mafuska wanajua msuli kwa mwanaume ni urahisi wa kutoa tu na kumpandia mwanamke, ila msuli wako ni kwa ajili ya kuharisha, weka suruali na bukta mbali
 


Over the Counter wanaziita..!! Good..!!
 
boss hapo kwenye kukaa na msuli masaa 6 unaweza nifafanulia
Unakuwa unaharisha sana. Ila kuna hiyo niliyoelekeza post iliyopita i.e. Polyethylene glycol-electrolyte solution. Ni nzuri sana na kama ukiipata tumia hiyo. Siyo lazima uharishe kwani inategemea umekunywa kiasi gani. Inakuwa kwenye paketi.
 
Chakula kaka.

Ulikuwa unakunywa maji machache na chakula chenyewe ni aina ya vyakula vikavu ambavyo vilihitaji maji kwa wingi kufanya mmeng'enyo.

Watu wengi wanaolalamika constipation hulalamika ni kwa sababu ya vyakula wanavyokula.
 
Nunua Ukwaju Kilogram 1
Chemsha Chuja Vema Acha Upoe Halafu Kunywa Nusu Litre
Kaa Muda Wa Saa 1 Jirani Na Maliwato Vaa Msuli




Baadaye Lete Mrejesho Hapa
 
nalifanyia kaz kiongoz
 
punguza uvivu wa kunywa maji na matunda
 
ndugu zangu nawashukuru sana maoni yenu yamesaidia ,nlienda duka la dawa nikapewa vidonge vidogo vidogo kama 6 nikaambiwa nimeze vyote,baada ya muda kdogo mzgo umeshuka wote

najiskia huru sasa nipo nakunywa maji mengi
 
ndugu zangu nawashukuru sana maoni yenu yamesaidia ,nlienda duka la dawa nikapewa vidonge vidogo vidogo kama 6 nikaambiwa nimeze vyote,baada ya muda kdogo mzgo umeshuka wote

najiskia huru sasa nipo nakunywa maji mengi
Hahah haukuumia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…