Napata ndoto za kutisha baada ya kwenda kwa mganga wa kienyeji

Napata ndoto za kutisha baada ya kwenda kwa mganga wa kienyeji

emmarki

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,001
Reaction score
1,430
Nilijenga msingi mzuri wa imani yangu kwa Mungu, kuwa ndio anayeweza kunitoa kwenye hili dimbwi la kukosa kipato licha ya kugraduate since 2014 hizi digrii yeboyebo. Japokuwa Mungu alinisaidia kupata kazi za mikataba ya muda mfupi lakini mishahara ni ile ikizidi sana ni laki nne, sehemu nyingi niliambulia laki mbili, mpk laki moja kwa mwezi.

Kutokana na majukumu ya kusomesha mtoto na mama yake, kwangu inakuwa ni ngumu kusogea kimaisha. Hivyo muda mwingi ninakuwa kwenye stress ya kipato kidogo na madeni mengi.

Nilijitahidi kuwa muaminifu kwenye fungu la kumi na sadaka, maombi na kujitoa kwa kiwango kizuri kumtumikia Mungu. Nilitegemea nikifanya hayo angalau nut zitaanza kulegea kwenye uchumi, lakini ndio mambo yakazidi kuwa magumu sana.

Madeni yakaongezeka kwa sababu natakiwa nilipe ada ya mtoto na mama yake(nilimpa mimba dent kuepuka mvua 30 ikabidi nibebe jukumu la kusomesha private school. kwa sasa anamalizia six on May)

Mapema February kuna jamaa akanishauri anipeleke mahali nikaangalie kwa nini nakula msoto hivi licha ya bidii ninayowekeza kutafuta noti. Bibi wa kupiga bao akaniambia shida yangu ni ishu za mila za kwetu na NYOTA yangu imechezewa. Hivyo, nikamilishe mambo ya mila then nitafute fundi wa kusafisha nyota.

Nikapata ushuhuda mahali kuwa kuna fundi mzuri wa hayo mambo, kwa buku mbili tu ana darubini za kuona rohoni mwako. Siku ya kwanza nikaenda nikakuta nyomi, nikafanikiwa kumuona nkaeleza shida akaniambia nina nyota ya kutoa tu, ila ya kupokea, kutunza na nyingine nmesahau zimefungwa. Nikapewa dawa ya kuogea baada ya kurudi nyumbani

Usiku wa siku nliyotoka kwake, nikaota kuna mtu ananifukuza na ananitupia mishale mingi. Nilipambana kuikwepa kwa nguvu zangu ikashindikana lakini nikakumbuka kukemea kwa jina la Yesu mrusha mishale akapotea.

Nikarudi kwa doctor siku ya pili kwenda kufanyiwa huduma kuu yenyewe ya kusafishwa nyota. usiku wake tena baada ya kutoka huko nikaota tena kuna nyoka black ananishambulia kwa kunirushia mate ya sumu, nilipambana kwa nguvu zangu lkn alitaka kunizidi nguvu, nkakumbuka kukemea kwa damu ya Yesu ndio akapotea.

Nilimpigia kalmanzila kumueleza kuhusu hizo ndoto, akaniambia nirudi akanipe kinga...mpaka muda sijarudi tena huko

Matokeo baada ya huduma yake, ni kuwa nimepata kazi japo ni ya muda mfupi lakini ina maslahi mazuri na kuna HR wa shirika moja zuri aminiahidi soon kuna neema inatoka kwenye shirika lao nitakuwa front line kwa sababu ni qualifications zote na experience wanayoihitaji.

Naweza kusema angalau naona mabadiliko kwenye suala la kibali tofauti na mwanzoni

Sasa wanajamvii nauliza, nirudi kwa kalmanzila nikamalizie dozi au nikatubu nimrudie Mungu.
 
unajichanganya mwenyewe kaka.
kwani mganga amekukataza kukemea kwa jina la Yesu?
katika vita yoyote unapaswa kupigana kwa njia yoyote ili mradi uwe salama.
(ulikuwa ktk vita ya kiroho)
rudi kamalizie chanjo ya uviko19, pia mshukuru MUNGU kwa kukupa maarifa ya kusolve tatizo lako.

Hos 4:6​

Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.
 
Mbna Kali hi
Duh Kaz umepat na ndotA majoka meuz Bado unaota mban hatri hii
Angalia usije kuwa kichaaaa
 
aliponipa dawa aliniambia nisikutane kimwili na mwanamke, ila hakuniambia nisisali. Nikajiuliza, mtu akienda hospitali anaumwa maleria katibiwa akapona obvious atamshukuru Mungu na siyo doctor aliyetibu akapona
 
Mbna Kali hi
Duh Kaz umepat na ndotA majoka meuz Bado unaota mban hatri hii
Angalia usije kuwa kichaaaa
ndoto hizo ni siku ile nilipoenda tu kwake,, kwa sasa hivi hazipo tena hizo ndoto
 
Ingekua poa sana Kama huu ushauri mnaompa ingekua unatolewa na watu wanaoishi maisha matakatifu

Mtoa mada Yesu kristo alionya kuhusu maisha ya uvuguvugu
Kama umeamua kuwa wabaridi kuwa baridi kweli kweli
Na Kama umeamua kuwa wamoto kuwa moto kweli kweli
maisha yananiforce mkuu, jaribu langu kubwa ndio liko hapa. nikipambana kuvuka naishia njiani.
 
Nilijenga msingi mzuri wa imani yangu kwa Mungu, kuwa ndio anayeweza kunitoa kwenye hili dimbwi la kukosa kipato licha ya kugraduate since 2014 hizi digrii yeboyebo. Japokuwa Mungu alinisaidia kupata kazi za mikataba ya muda mfupi lakini mishahara ni ile ikizidi sana ni laki nne, sehemu nyingi niliambulia laki mbili, mpk laki moja kwa mwezi.
Kutokana na majukumu ya kusomesha mtoto na mama yake, kwangu inakuwa ni ngumu kusogea kimaisha. Hivyo muda mwingi ninakuwa kwenye stress ya kipato kidogo na madeni mengi.

Nilijitahidi kuwa muaminifu kwenye fungu la kumi na sadaka, maombi na kujitoa kwa kiwango kizuri kumtumikia Mungu. Nilitegemea nikifanya hayo angalau nut zitaanza kulegea kwenye uchumi, lakini ndio mambo yakazidi kuwa magumu sana. Madeni yakaongezeka kwa sababu natakiwa nilipe ada ya mtoto na mama yake(nilimpa mimba dent kuepuka mvua 30 ikabidi nibebe jukumu la kusomesha private school. kwa sasa anamalizia six on May)

Mapema February kuna jamaa akanishauri anipeleke mahali nikaangalie kwa nini nakula msoto hivi licha ya bidii ninayowekeza kutafuta noti. Bibi wa kupiga bao akaniambia shida yangu ni ishu za mila za kwetu na NYOTA yangu imechezewa. Hivyo, nikamilishe mambo ya mila then nitafute fundi wa kusafisha nyota.

Nikapata ushuhuda mahali kuwa kuna fundi mzuri wa hayo mambo, kwa buku mbili tu ana darubini za kuona rohoni mwako. Siku ya kwanza nikaenda nikakuta nyomi, nikafanikiwa kumuona nkaeleza shida akaniambia nina nyota ya kutoa tu, ila ya kupokea, kutunza na nyingine nmesahau zimefungwa. Nikapewa dawa ya kuogea baada ya kurudi nyumbani

Usiku wa siku nliyotoka kwake, nikaota kuna mtu ananifukuza na ananitupia mishale mingi. Nilipambana kuikwepa kwa nguvu zangu ikashindikana lakini nikakumbuka kukemea kwa jina la Yesu mrusha mishale akapote.
Nikarudi kwa doctor siku ya pili kwenda kufanyiwa huduma kuu yenyewe ya kusafishwa nyota. usiku wake tena baada ya kutoka huko nikaota tena kuna nyoka black ananishambulia kwa kunirushia mate ya sumu, nilipambana kwa nguvu zangu lkn alitaka kunizidi nguvu, nkakumbuka kukemea kwa damu ya Yesu ndio akapotea. Nilimpigia kalmanzila kumueleza kuhusu hizo ndoto, akaniambia nirudi akanipe kinga...mpaka muda sijarudi tena huko

Matokeo baada ya huduma yake, ni kuwa nimepata kazi japo ni ya muda mfupi lakini ina maslahi mazuri na kuna HR wa shirika moja zuri aminiahidi soon kuna neema inatoka kwenye shirika lao nitakuwa front line kwa sababu ni qualifications zote na experience wanayoihitaji. Naweza kusema angalau naona mabadiliko kwenye suala la kibali tofauti na mwanzoni

Sasa wanajamvii nauliza, nirudi kwa kalmanzila nikamalizie dozi au nikatubu nimrudie Mungu.
rudi umalizie therapy
 
Ingekua poa sana Kama huu ushauri mnaompa ingekua unatolewa na watu wanaoishi maisha matakatifu

Mtoa mada Yesu kristo alionya kuhusu maisha ya uvuguvugu
Kama umeamua kuwa wabaridi kuwa baridi kweli kweli
Na Kama umeamua kuwa wamoto kuwa moto kweli kweli
Mwisho wake hauwagi powa mkulu katubu tu kabla hujala mahatua mengi zaid unatafuta hela kwaajili ya familia mwisho wa siku waweza kujikuta unaiuza familia kwa hizo miamala za kijadi
 
Dunia kuna nguvu mbili ya Nuru na ya giza mwanadamu kapewa UHURU wa kuchagua. Kama unaona Mungu Yehova atakusaidia mtumikie kama unaona mungu baal atakusaidia mtumikie epuka kuwa vuguvugu.
Ndoto za kuumwa na nyoka, kufukuzwa, kutupiwa mishale. Ni vita vya kiroho ulivyopigana navyo
 
Back
Top Bottom