Napata ndoto za kutisha baada ya kwenda kwa mganga wa kienyeji

Napata ndoto za kutisha baada ya kwenda kwa mganga wa kienyeji

Nilijenga msingi mzuri wa imani yangu kwa Mungu, kuwa ndio anayeweza kunitoa kwenye hili dimbwi la kukosa kipato licha ya kugraduate since 2014 hizi digrii yeboyebo. Japokuwa Mungu alinisaidia kupata kazi za mikataba ya muda mfupi lakini mishahara ni ile ikizidi sana ni laki nne, sehemu nyingi niliambulia laki mbili, mpk laki moja kwa mwezi.
Kutokana na majukumu ya kusomesha mtoto na mama yake, kwangu inakuwa ni ngumu kusogea kimaisha. Hivyo muda mwingi ninakuwa kwenye stress ya kipato kidogo na madeni mengi.

Nilijitahidi kuwa muaminifu kwenye fungu la kumi na sadaka, maombi na kujitoa kwa kiwango kizuri kumtumikia Mungu. Nilitegemea nikifanya hayo angalau nut zitaanza kulegea kwenye uchumi, lakini ndio mambo yakazidi kuwa magumu sana. Madeni yakaongezeka kwa sababu natakiwa nilipe ada ya mtoto na mama yake(nilimpa mimba dent kuepuka mvua 30 ikabidi nibebe jukumu la kusomesha private school. kwa sasa anamalizia six on May)

Mapema February kuna jamaa akanishauri anipeleke mahali nikaangalie kwa nini nakula msoto hivi licha ya bidii ninayowekeza kutafuta noti. Bibi wa kupiga bao akaniambia shida yangu ni ishu za mila za kwetu na NYOTA yangu imechezewa. Hivyo, nikamilishe mambo ya mila then nitafute fundi wa kusafisha nyota.

Nikapata ushuhuda mahali kuwa kuna fundi mzuri wa hayo mambo, kwa buku mbili tu ana darubini za kuona rohoni mwako. Siku ya kwanza nikaenda nikakuta nyomi, nikafanikiwa kumuona nkaeleza shida akaniambia nina nyota ya kutoa tu, ila ya kupokea, kutunza na nyingine nmesahau zimefungwa. Nikapewa dawa ya kuogea baada ya kurudi nyumbani

Usiku wa siku nliyotoka kwake, nikaota kuna mtu ananifukuza na ananitupia mishale mingi. Nilipambana kuikwepa kwa nguvu zangu ikashindikana lakini nikakumbuka kukemea kwa jina la Yesu mrusha mishale akapote.
Nikarudi kwa doctor siku ya pili kwenda kufanyiwa huduma kuu yenyewe ya kusafishwa nyota. usiku wake tena baada ya kutoka huko nikaota tena kuna nyoka black ananishambulia kwa kunirushia mate ya sumu, nilipambana kwa nguvu zangu lkn alitaka kunizidi nguvu, nkakumbuka kukemea kwa damu ya Yesu ndio akapotea. Nilimpigia kalmanzila kumueleza kuhusu hizo ndoto, akaniambia nirudi akanipe kinga...mpaka muda sijarudi tena huko

Matokeo baada ya huduma yake, ni kuwa nimepata kazi japo ni ya muda mfupi lakini ina maslahi mazuri na kuna HR wa shirika moja zuri aminiahidi soon kuna neema inatoka kwenye shirika lao nitakuwa front line kwa sababu ni qualifications zote na experience wanayoihitaji. Naweza kusema angalau naona mabadiliko kwenye suala la kibali tofauti na mwanzoni

Sasa wanajamvii nauliza, nirudi kwa kalmanzila nikamalizie dozi au nikatubu nimrudie Mungu.
Biblia inasema, "KUFANIKIWA KWA MPUMBAVU KUTAMUANGAMIZA"

kamwe usikubali Kumsujudia shetani ili upate mali....

Shetani alimuonyesha Yesu milki yote ya Dunia na fahari yake kisha akamuambia "Ukiinama kunisujudia nitakupa"

......itakufaidi nini ukipata utajiri na mali zote za dunia ukamkose Mungu?

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
aliponipa dawa aliniambia nisikutane kimwili na mwanamke, ila hakuniambia nisisali. Nikajiuliza, mtu akienda hospitali anaumwa maleria katibiwa akapona obvious atamshukuru Mungu na siyo doctor aliyetibu akapona
Aiseeee
Usikutane na mwanamke kwa mda gani?

Je hata mkeo usikutane nae?
 
Biblia inasema, "KUFANIKIWA KWA MPUMBAVU KUTAMUANGAMIZA"

kamwe usikubali Kumsujudia shetani ili upate mali....

Shetani alimuonyesha Yesu milki yote ya Dunia na fahari yake kisha akamuambia "Ukiinama kunisujudia nitakupa"

......itakufaidi nini ukipata utajiri na mali zote za dunia ukamkose Mungu?

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile
unaamini kuwa kila mtu ana kibali/luteka/nyota inayomuwezesha kufanikiwa katika kufanya kile alichoumbiwa hapa duniani. km mama jusi walivyoona nyota ya Yesu alipozaliwa na kugundua ni mfalme amezaliwa kupitia unajimu wao. Kibali cha mtu kinaweza kuchafuliwa na ikafanya maisha ya mtu huyo kuwa magumu
 
Mwisho wake hauwagi powa mkulu katubu tu kabla hujala mahatua mengi zaid unatafuta hela kwaajili ya familia mwisho wa siku waweza kujikuta unaiuza familia kwa hizo miamala za kijadi
najua, najitoa sadaka for sake ya family
 
Kuota unakimbizwa ni ishara ya kufukuzwa kwenye mafanikio yako halisi na kupewa feki ambayo ndo unayaona sasa.

Lakini pia kuota nyoka anakutemea sumu ni ishara nyingine kwamba umeingia kwenye milki ya shetani (nyoka) na tayari amekupa sumu ambayo baada ya muda ndo itaanza kuonyesha makali yake.

Ulivyokuwa ukiomba na kukemea kwenye ndoto ni Mungu anasema na wewe kuwa bado mlango wa neema ya Kristu kupitia damu yake haujafungwa na anatamani uwe na nguvu za kiroho halisi kupitia Neno lake badala ya kutembea katika mafanikio hafifu na ya muda ya giza.

Jitafakari before ts too late. Umefanya jambo ambalo Mungu alitaka kuwaangamiza wana wa Israeli wote at once pale walipochanganya miungu (walitengeneza ndama) wakaiabudu.

Mungu akurehemu sana rafiki yangu. Moyoni wangu umepata huzuni kusoma andiko hili kama ni la kweli.

Be Blessed.
 
nifanyeje kiongozi, hawa watu waliweza kuona nyota yangu haijakaa sawa. Kwenye bible kuna vifungu na muongozo mzuri wa kusafisha kibali changu ili mambo yaniendee vizuri. kama ulishawahi pitia maisha ya kukaa mwezi bila kuingiza hata mia utaelewa. efforts zangu haziniletei matunda
 
Therapy ya mganga ambaye ni kiumbe cha Mungu, inasema ana mkono wa kutoa. Hii ina maana anatoa kuliko anavyopata. Je, kuna ukweli kweye hili. Siku hizi kuna hata mapasta na maaskofu wanaohubiri injili ya utajirisho, ambayo kwangu naona ni utapeli tu. Kama hao wahubiri wanaamini kwenye hiyo injili ya utajirisho kwa nini wawakamue waumini? Kwa nini wao wasijazwe mapesa na Mungu kama wanavyowaaminisha maskini kuwa waendelee kumuomba Mungu atawajaza utajiri. Hiyo injili ni ya uongo ikielekezwa ama kwa wajinga au watu waliokwisha tekwa kiakili na sasa ni mazuzu au mazezeta.
 
unaamini kuwa kila mtu ana kibali/luteka/nyota inayomuwezesha kufanikiwa katika kufanya kile alichoumbiwa hapa duniani. km mama jusi walivyoona nyota ya Yesu alipozaliwa na kugundua ni mfalme amezaliwa kupitia unajimu wao. Kibali cha mtu kinaweza kuchafuliwa na ikafanya maisha ya mtu huyo kuwa magumu
Ni kweli lakini siyo sahihi kumuangukia Shetani ili asafishe nyota yako kwa maana hata shetani Mwenyewe Biblia inamuita Nyota

Ukisoma Isaya 14:12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!

shetani ni nyota lakini kazi yake ni kuwaangusha mataifa

Kwa hyo mtafute Yesu atakusafisha na Utafanikiwa...

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
nifanyeje kiongozi, hawa watu waliweza kuona nyota yangu haijakaa sawa. Kwenye bible kuna vifungu na muongozo mzuri wa kusafisha kibali changu ili mambo yaniendee vizuri. kama ulishawahi pitia maisha ya kukaa mwezi bila kuingiza hata mia utaelewa. efforts zangu haziniletei matunda
Wewe siyo wa kwanza kupitia Economic crisis Mkuu..

Tatizo hukupata ushauri sahihi matokeo yake ukashauriwa kuziendea njia za giza..
(kumsujudia Shetani)

Itakufaidi nini ukipata milki zote za Dunia halafu ukamkosa Mungu?

Kwa maana Shetani anao uwezo wa kukupa mali...lakini Mwisho wake ni Kifo tena cha Ghafla ili usipate Muda wa kutubu....

Na hiyo Dhambi utaona ni ndogo lakini...itakuandama wewe na uzao wako wote na ni machungu yasiyo na mfano...

Wewe unajiangalia binafsi yako lakini shetani analenga madhara yatakayokuandama vizazi vyako vyote...

Unajisikiaje unaendesha gari, una nyumba, na mali nyingi halafu moyoni mwako unajua wazi Mdhamini wako ni Shetani?

Hili jambo linaumiza nafsi za wengi wanaopata mali kwa njia za uganga na uchawi sema hawasemi...

SHETANI AKIKUKOPESHA UTALIPA, HATA KAMA UTACHELEWA KUDAIWA.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
nifanyeje kiongozi, hawa watu waliweza kuona nyota yangu haijakaa sawa. Kwenye bible kuna vifungu na muongozo mzuri wa kusafisha kibali changu ili mambo yaniendee vizuri. kama ulishawahi pitia maisha ya kukaa mwezi bila kuingiza hata mia utaelewa. efforts zangu haziniletei matunda
Suala la waganga na wachawi kuona nyota yako na kukuambia mambo ya sirini wala siyo shida kwa maana hata Biblia inatuambia kwamba waganga na wachawi wanao huo uwezo....sema lengo lao ni Kuipoteza nafsi yako kabisa...

Ukisoma biblia katika Kumbukumbu la Torati 13:1-3

Biblia inasema :-

1.Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu,

2.ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo;

3.wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
unajichanganya mwenyewe kaka.
kwani mganga amekukataza kukemea kwa jina la Yesu?
katika vita yoyote unapaswa kupigana kwa njia yoyote ili mradi uwe salama.
(ulikuwa ktk vita ya kiroho)
rudi kamalizie chanjo ya uviko19, pia mshukuru MUNGU kwa kukupa maarifa ya kusolve tatizo lako.

Hos 4:6​

Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.

Maathayo 7...

21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
 
unaamini kuwa kila mtu ana kibali/luteka/nyota inayomuwezesha kufanikiwa katika kufanya kile alichoumbiwa hapa duniani. km mama jusi walivyoona nyota ya Yesu alipozaliwa na kugundua ni mfalme amezaliwa kupitia unajimu wao. Kibali cha mtu kinaweza kuchafuliwa na ikafanya maisha ya mtu huyo kuwa magumu
Umenukuu maandiko visivyo....

Mamajusi hawakuwa wanajimu...wala Biblia haijasema hvyo

Utambuzi wa kuitambua ile nyota walipewa na Mungu ili wasipotee njia na kufika eneo alikozaliwa Yesu...
Kwa ufupi ni kwamba ile nyota ilikuwa inawaongoza njia kufika alipo Mtoto Yesu....

Na ndyo maana baada ya kufika Ile nyota ilipotea.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: _ly
Back
Top Bottom