dr alikuambia sababu ya hayo majimaji ya ukeni kupungua? maybe unahitaji kumuona tena,ungerudi kwake.
kunaweza kuwepo sababu kadhaa za hali hii
1 aina ya chupi unazovaa. zinapaswa kuwa za cotton ili upate hewa ya kutosha.ni ngumu kiasi kupata pure cotton ila huna jinsi
2 hakikisha unaanika chupi zako kwenye jua. mambo ya kuanika chini ya godoro ama bafuni,kunakua na unyevu unaosababisha kuzaliana kwa bacteria. walau mara moja kwa wiki unaweza kuloweka chupi zako kwenye maji ya uvuguvugu yenye jik (1:20 v/v)
3 hygiene issues: nawa mikono kabla na baada ya kujisaidia (kuna hand sanitizer siku hizi,zinauzwa kwenye kichupa kidogo kwenye phamacy). baada ya haja kubwa tumia toilet paper kabla ya maji. jifute kuanzia mbele kuelekea nyuma. kila wakati unapotumia choo jifute ukeni kuanzia mbele kuelekea nyuma, then jifute nyuma kwa style hiyo hiyo ya kuanzia mbele kuelekea nyuma. sikushauri sana kutumia maji unless unakua na kitambaa cha kujifuta kila mara unapomaliza haja (usirudie kitambaa!!!). oriflame wana wet tissue zinaitwa femme,unaweza kuzitumia baada ya kutumia toilet papes.
4 epuka kutumia antibiotic ama madawa makali,huchangia kuua wadudu rafiki wa ukeni. usitumie pia sabuni zenye harufu kali. kuna sabuni maalum ambayo ni soap free ya kunawia ukeni, mary rose wanayo kama upo dsm.
5 usifanye douching (kujiswafi uke kwa kuingiza kidole). google uone jinsi ambavyo unajihatarisha kwa kuingiza uchafu na kusababisha vidonda. uke una mechanism yake ya kujiswafi wenyewe. na kama una hiyo obssession kuna kifaa maalum cha kufanyia douching
wakati unajaribu kuzingatia haya kwa ajili ya kubadili life style, inabidi uende hospitali,onana na daktari wa wanawake ikibidi.utapata ushauri wa kutibu na kuepuka maambukizi mapya.