Napata wasiwasi wabunge wa CHADEMA wanataka kuwafanya nini! Serikali, Bunge wote wanaacha kujadili bajeti wanawajadili

Napata wasiwasi wabunge wa CHADEMA wanataka kuwafanya nini! Serikali, Bunge wote wanaacha kujadili bajeti wanawajadili

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,896
Kuna anayefikiri kama mimi?

1. Walipoondoka bungeni spika alifurahi na kusema hata wasipokuwepo ccm wanatosha kupitisha mambo yao na cdm hawana madhara yoyote na hawajavunja sheria wala kanuni yoyote.

2. Akaja Rais Magufuli akaonyesha kuumia sana kwa wao kuondoka akatoa amri wasilipwe posho. Yaani muhimili unaingiliwa na muhimili mwingine.

3. Akaja Waziri wa Sheria na Katiba na wabunge wote wa CCM hawasimami bila kuwataja CHADEMA.

4. Akaja Makonda na mikwara mbuzi.

5. Leo kaja spika na kauli nyingine lengo kutaka wawaone sehemu.

Hivi wanalengo jema na wabunge hawa au kuna kitu kinatengenezwa?
 
hivi bado kuna wabunge cdm au ni udikteta wa DJ!! Wenye akili wameshashutuka! wamebaki vifuu tu huko
 
Saccos imeshafutika tayari kama wabunge zaidi ya 10 hawakubaliani na jinsi saccos inavyoendeshwa na Mbowe Mugabe sasa unafikiri kuna saccos hapo?
 
Kweli leo supika kawa mbogo, wakati alidai hata wangejiuzulu wote ubunge haoni shida na hawajavunja kanuni yoyote.

Leo anawataka kurejea bungeni haraka na wawe wamepima corona, na warudishe posho.
Na akamaliza kwa kusema, "yajayo kwa hili kundi la wabunge wa CDM yanafurahisha".
Akashangiliwa sana wa wagonga meza.
Mmhh! Nahisi harufu ya panya aliyeoza!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Saccos imeshafutika tayari kama wabunge zaidi ya 10 hawakubaliani na jinsi saccos inavyoendeshwa na Mbowe Mugabe sasa unafikiri kuna saccos hapo?
Lakini mbona kutwa hamlali bila ya kuwataja wao.
Wakiwa bungeni mnawafanyia kila hila mbaya leo wametoka mmeacjiwa pekeyenu bado hamjiamini.

Mbona mnakuwa kama wanawake malaya.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni kutaka kujua tu. Mfano Mhe. Mbunge akiamua kutohudhuria Bungeni kwa hiari yake. Je kuna sheria ya Bunge inayomlazimisha kuhudhuria kikao cha bunge?.
 
Wasiende bungeni. Wanataka kuwauwa. Roho ya mtu mbaya hujidhihirisha kwa kinywa chake.

Chadema msiende Wala msiingie watawafanya kitu kibaya. Haiwezekani wakasirike kiasi hiki.

CCM ni genge baya sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi naona kama Chadema wanapewa promo ya bure tena isiyostahili kabisa.

Sasa imekuwa ni kawaida kila mbunge anayesimama kuchangia bajeti kabla hata ya kumshukuru Mungu kwa uzima anaanza kuitaja Chadema.
Hata kiti cha Spika kabla ya kuahirisha bunge lazima kiitaje Chadema.

Kinachonishangaza ni ukweli kuwa karibia nusu ya wabunge wa Chadema wanahudhuria vikao vya bunge na wanachangia sasa hii nongwa inatoka wapi?

Mwishowe watu wataziamini habari za historia ya " unga unga" kutaka kujirudia.

Mungu awabariki nyote.

Maendeleo hayana vyama!
 
Unadhani kusemwa semwa Kwa sifa za kijinga ndio ushujaa?

Toka Utumwani wewe, Tumia akiri yako ukomboke!!
 
Back
Top Bottom