Napataje malighafi ya mchikichi, nataka kuanza kukamua Mafuta

Napataje malighafi ya mchikichi, nataka kuanza kukamua Mafuta

Habarini Guys.

Nimepata idea ya Kukamua Mafuta ya Mawese au ya Mchikichi ila sasa maligafi ya uhakika na bei rafiki ndio najaribu kuwaza.. inapatikan wapi kwa wingi??

Kama una uzoefu wa Ukamuaji wa Mawese na Mchikichi naomba unisaidie kujua yafuatayo:

1. Mkoa wenye uhakika wa Mchikichi na Mawese!
2.Gharama za mashine ya Kukamulia yakuanzia siyo zile kubwa sana
3. Changamoto za kuyafanyia refine na hatuazake..

Asanteni


Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Mkuu umewaza idea bora sana hadi sasa.. Mimi nafanya hiyo kazi kwa muda mrefu sasa. Lakini pia nasaidia baadhi ya watu wanaopenda kuweza kuanzisha..

Kama unapenda na upo. Serious wasiliana nami na ikiwezekana kuonana notakupa muongozo uliokamilika sana.

Tumia mawasiliano haya kuweza kunipata: 0682836463 sinaga choyo na fursa.

Lakini pia ingia Instagram tafuta account inaitwa @efox_industries utapata msaada pia. ( Login • Instagram ).

Ila usisahau kunipogia mkuu.
 
Boss naomba kuwasiliana na wewe.. Namba zangu hizi hapa: haya WhatsApp pia mkuu: 0682836463
Sorry nimeshindwa Ku quote.Bei za machine za kisasa sijui kwakweli labda SIDO wanaweza kuwa na details zaidi.Huku niliko ni kijijini na hakuna mwenye hiyo mashine ya kisasa hivyo ni fursa nyingine hiyo kwani watu watakuwa wanakuja kukamua kwako na kukupa pesa au mawese. pia kama utakuwa na mtaji na soko lako zuri la mawese watakuwa wanakuuzia hapohapo baada ya kukamua kwani wengi hawasafirishi bali kuna wanunuzi wanapita kila asubuhi kwenye eneo ambapo processing inafanyika kwa ajili ya kutoa order ya kukusanya product. Pia wanakuuzia mise ambayo utaimenya(machine zipo au utanunua yako) then utapeleka SIDO kusaga,utapata mafuta ambayo wanatengeneza sabuni pia na mashudu ambavyo utauza kwa pesa nzuri tu hapo hapo SIDO. Pia itakuwea rahisi kupata connection zaid juu ya upatikanaji wa hizo raw materials na Wateja zaidi kwani watakuwa wanakufuata popote ulipo wakihitaji either kukamua,kuuza au kununua ngazi,mise au mawese.

Ngazi (amagazi kwa kiha)
Ni Yale matunda ambayo yakiiva yanakuwa na rangi ya njano au nyekundu.Haya yakikamuliwa hutoa mafuta ya mawese ambayo ni mazuri na Matamu sana kwa kula

Mise
Ni lile ganda linalobaki baada ya lile ganda la ngazi kukamuliwa. Hili linakuwa kama mfano wa Nazi tofauti ni size tu kwani mise ni midogo kwa size.Hii pia humenywa kwa mashine ambayo hutumia muda mfupi zaidi na kwa debe moja bei yake ni tshs 300/ au kwa kutumia mawe locally na hutumia muda mwingi sana ambapo baada ya kumenya kwa ndani kunakuwa na mse kama Nazi vile ila ni kadogo kwa size .Baada ya kukusanya kiasi cha kutosha cha mise utachagua either uuze mise au upeleke SIDO kusaga na kupata mafuta ambayo ndiyo hayo wanatengeneza sabuni maarufu kama sabuni za Kigoma (gwanji) ambayo ina povu nyingi sana na hutakatisha nguo vizuri sana but si nzuri kwa kuogea japo watu wanatumia. Pia baada ya kukamua tunapata Mashudu ambayo ni chakula kizuri sana cha mifugo kama kuku na nguruwe.
Kwa kifupi hii ni bonge moja la fursa kama utaamua kuifanya seriously na ukiwa na capital nzuri kwani soko lake ni zaidi ya uhakika.
Asante na kila la kheri kama utaamua kuwekeza mwenye eneo hili.
 
Back
Top Bottom