Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,916
- 43,505
Sasa mbona mtoa mada anaongelea habari ya "Tozo"!! Au ameamua tu kupotosha kwa makusudi?
Maana kama ni ishu ya tozo, hii ni sheria iliyo pitishwa na bunge. Ila kuhusu vifurushi, hili ni suala lililo ndani ya mamlaka ya Waziri mwenye dhamana, TCRA, na makampuni ya simu!
Kuwekwa kwa tozo na kupandishwa kwa kodi ndio sababu ya kupanda kwa gharama za huduma hili jambo mbona dogo sana kulielewa? Kabla ya Nape aliyekuwepo alijaribu lakini jiulize alikwamia wapi? Ukitaka waongeze Mbs punguza tozo na kodi kwenye huduma basi na wao wataongeza Mbs kinyume na hapo hakuna atakaye kubali kupata hasara