Nape aongoza mazishi ya Sharomillionea

Nape aongoza mazishi ya Sharomillionea

ujue nilikuwa sijakuelewa mwanzo!nilipokuelewa nimecheka sana!lol
af muda si mrefu mkasi utafanana nae!

oooh snowhite usipime mtu wangu,,yule jamaa anajiskia burudani sana kukata kata tepe mbali mbali

eti watu wanasema kwamba hua anatembea na mkasi mfukoni,,yan hua anajiandaa kabisa,,ikitokea uzinduzi tuh faster anaingia mfukoni ana chanja kama kawa,,af jinsi anavojiskia burudani,,hua anakata huku akitoa sura ya bashasha kabisa,,lol

mr mikasi noma sana
 
Hawa watu wakiwa hai,chama cha mapinduzi wanalala usingizi wa pono bungeni na kuwaacha wasanii wakiibiwa kazi zao,pamoja na mazingira magumu ya kuendeleza sanaa.Kwenye misiba basi Mkuu wa wilaya (ccm) na Nape (ccm) wapo mstari wa mbele kutukumbusha tuenzi mema ya marehemu.Ni lini wasanii watajivunia matunda ya uwepo wa serikali ya ccm,kabla ya kuona tu ukijani msibani? Anyway R.I.P Sharo Millionea!
 
Yan sisi em inashangaza sana,,kila mahala,kila siku mzuka wa chadema umekua unawaandama sana,,hapo wameona may be wasipoKua wao kimbele mbele basi cdm wangewahi na kwenda kuzika huku wakikosoa ubovu wa bara bara za ccm ndzo zinakua vyanzo vya ajali wangekosa pa kutokea ndio maana wakaamua kukimbilia speed 360,,kufa kupo pale pale ccm
 
Wasanii wa Bongo bana!!!!!!!!!! Pozi msibani ya nini?Jitu linakaa miguu juu kwenye kiti na mengine Mikufu mikubwaa!!!!!! Ivi amuwezi kua simple angalau kwa masaa machache tu? Na ndo mana umaarufu wenu unaishia Bongo tu.

CCM nao ndo hata kusoma alama nyakati shida, utaendaje msibani na mavazi ya chama?? Au ilikua two in one nini-msiba na kampeni?

Yote kwa yote Mama Sharo pole sana jamani.Mungu akupe uvumilivu katika kipindi kigumu ulichokua nacho.
 
Ifike mahali ipigwe marufuku kuvaa nguo za chama cha siasa kwenye misiba.
 
Tulitoka mavumbini na mavumbini tutarudi
Nimejikuta nadodosha machozi kwa uchungu!
RIP Sharobaro tulikupenda sana lakini mwenyezi mungu kakupenda zaidi
Jina lake libarikiwe
 
Cdm sijawaona Nape kaongoza mazishi na eneo zima limepambwa kwa rangi za kijani...kulikoni?

Wenye sare za CCM wazomewa

Katika msiba huo watu waliokuwa wamevalia sare za CCM walijikuta katika wakati mgumu baada ya kuzomewa na waombolezaji ambao walisema hakukuwa na haja ya kujitambulisha kiitikadi katika msiba huo.

Kundi la vijana waliokuwa kando ya barabara ielekeayo kitongoji cha Jibandeni, nyumbani kwa mama mzazi wa marehemu, waliwazomea watu hao huku wakisema kuwa huo haukuwa msiba wa CCM bali ni wa wasanii wa filamu.

Vijana hao walieleza kushangazwa kwao na kitendo cha makada hao kuvaa sare katika msiba huo wakati kiongozi wao ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aliwasili msibani hapo akiwa amevaa nguo za kawaida.

Source: gazeti la Mwananchi
 
Maskini CCM,Hakika hali imekuwa mbaya sana kwa ccm katika ustawi wake na imeanza kubuni mbinu chafu za kuombea vifo vya watu maarufu kujitangaza kuwa kipo na kinnawajali.Wachambuzi wa masuala ya siasa na mahusiano wanabanisha kuwa mbinu hii ni mbaya kwa umma na wananchi ambayo hakika wanaona ni vema ccm kingebuni mbinu ya kuzuia vifo ili kipate wananchama padala ya kuibukia kwenye misiba na kutoa ngojera.Kwa misiba ya wasanii maarufu hivi karibuni Katibu mwenezi makao makuu ya ccm ndg Nepi ameonekana akitoa ngojera na pia hapo jana alisafri kutoka DAR hadi Muheza zaidi ya kilometa 200 kutoka DAR na ccm kuteka protocol yote ya mazishi.
Kama ccm ingekuwa inapenda kushiriki mambo ya kijamii siyo tatizo kama NEPI angetoa maagizo kwa viongozi wa ccm wilaya,kijiji ulipo msiba na Kata husika kushiriki na siyo kukurupuka kutoka makao makuu na timu ya ccm hadi Muheza na kuagiza harakati za ccm zitawale msiba wa Sharomilionea kuvika kitambaa cha rangi ya kijani.Kama hali itakuwa sia ajabu ccm akatamani hata akina mzee Majuto,Jay day nao watangulie mbele za haki ili kupata sehemu za kuanzisha harakati za kisiasa.
CCM imekwisha kufa ni wajibu wa viongozi kuandaa mikakati endelevu na siyo kutafuta umarufu katika misiba ili kuokoa chama chenu.
ALUTA CONTNIUA, ALUTA CATABUU
 
Niliona hiyo, lakini si unajua wasanii wengi maararufu huwa wanajipendekeza CCM acha iwazike kwa mbwembwe tu! Afterall wana mahusiano mazuri saaaana!
 
Cdm sijawaona Nape kaongoza mazishi na eneo zima limepambwa kwa rangi za kijani...kulikoni?

Tulikuwepo mazishi siyo sehemu ya kufanya siasa, wapo wananchi wengi wanaokufa kila siku mbona hatuioni CCM na Nape wakija kuzika? This is just cheap politics..
 
ccm imesha kufa kama kama sharo alivyo kufa sasa mfu kumzika mfu mwenzake kuna tatizo gani si anaandaa wanachama huko ahela ambako ndiyo makazi rasmi ya ccm kuanzia mwaka 2015
 
Kaongozaje?
Yeye alkuwa kama nani baba mdogo/shemeji/mjomba wa marehemu au shekhe kama sio ustaadhi aliesoma kitabu....

Kama hakuwa na title za hapo sielewi aliongozaje na badala yake atakuwa ameshiriki kama yeye binafsi au mwakilishi wa ccm.

My take:
waandishi wetu wamekuwa watumwa wa wanasiasa na ccm kwa ujumla wake, yani kwenye msiba akiwepo mtu wa serikali au ccm lazima waripoti kuwa ndie alieongoza mazishi hayo.
 
Kuna picha nimeona jeneza lililobeba mwili wa marehemu limefunikwa kwa bendera ya CCM.

Ni ndugu waliomba iwe hivo au kijana alikuwa na uongozi CCM au ndo kutafuta political popularity kwenye mazishi,unaweza kufuata hiyo link kwa picha.
http://4.bp.blogspot.com/-_Oox3SjoH6A/ULbtJQhs4dI/AAAAAAACROw/gVOq-KDXYmg/s1600/sharo.jpg
 
Akili za Nape anatumia misiba na kila nafasi itakayojitokeza mbele yake.
 
Kuna picha nimeona jeneza lililobeba mwili wa marehemu limefunikwa kwa bendera ya CCM.

Ni ndugu waliomba iwe hivo au kijana alikuwa na uongozi CCM au ndo kutafuta political popularity kwenye mazishi,unaweza kufuata hiyo link kwa picha.
http://4.bp.blogspot.com/-_Oox3SjoH6A/ULbtJQhs4dI/AAAAAAACROw/gVOq-KDXYmg/s1600/sharo.jpg

Usilete mambo yasiyokuwa na msingi, Jeneza halikuwa na viashiria vyovyote vya CCM hivyo vitambaa vilivyokuwa vimefunikwa ni vitambaa tu ambavyo vina rangi ya kijani lakini havina maana na CCM
 
Back
Top Bottom