GE2025 Nape aonya vijana kuhusu ushabiki wa uchaguzi, kuna maisha baada ya uchaguzi

GE2025 Nape aonya vijana kuhusu ushabiki wa uchaguzi, kuna maisha baada ya uchaguzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye, amewataka vijana nchini kutanguliza hekima na kujitambua wakati wa uchaguzi, akisisitiza kuwa kuna maisha marefu baada ya kura kupigwa. Amesema si sahihi mtu kujitumbukiza kwenye vurugu au migogoro ya kisiasa kwa sababu ya siku moja ya uchaguzi na kuathiri mustakabali wake.

Ameeleza kuwa mara nyingi vijana ndiyo hulengwa na baadhi ya watu wanaotafuta kuwashawishi kuandamana au kufanya fujo, bila kuzingatia madhara ya vitendo hivyo. Nape amesisitiza kuwa ni rahisi kushawishiwa kwa maneno makali na kauli za jazba, lakini matokeo yake yanaweza kuwa mabaya na ya muda mrefu kwa mhusika binafsi.

Nape ametahadharisha kuwa siku ya kupiga kura, wapo watakaokwenda vituoni kutekeleza haki yao ya kikatiba kwa amani, huku wengine wakiambiwa wabaki mitaani kuandamana au kufanya fujo. Ameonya kuwa pindi mambo yanapoharibika, hasara na adhabu huangukia moja kwa moja kwa kijana aliyejihusisha na machafuko, siyo kwa wale waliomshawishi.

Amesisitiza kuwa ushabiki wa kisiasa si sababu ya kuhatarisha maisha, uhuru au mustakabali wa kijana. Amehimiza vijana kuweka ushabiki pembeni na kufikiri kuhusu elimu yao, familia zao na nafasi yao katika jamii baada ya uchaguzi, akisisitiza kuwa amani na busara ndiyo ngao bora katika kipindi hiki cha mabadiliko ya kisiasa.

Zaidi: Nape: Waliosusa wameamua kukiua chama chao wenyewe
 
Hakuna kijana mwenye Balls za kutoka na kuandamana Oktoba 29 wanajifurahisha tuu
 
Wanacho waza baada ya uchaguzi ndinga mpyaaaa inapaki nje inamsubiri na bank zero zinaongezeka tu kwa nn asiwashauri mkae kimya wale kimya kimya ... Acha kinuke kwanza tuheshimiane
 
Mtoeni Lissu gerezani tungelee hio nusu mkate.
 
Sasa kama haya mambo ni immaterial kwanini Kodi zetu zinatumika kwenye hizi Hekaya ?

 
Back
Top Bottom