Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
CCM, kiuhalisia, kamwe haiwezi kuheshimu demokrasia wala haki za wananchi kuwachagua watu wanaotaka wawaongoze.
CCM inaamini katika kupora kura au kupora maamuzi ya wananchi. Inaamini zaidi katika wizi kwenye kila jambo.
Mwizi huwa hachagui cha kuiba. Ndiyo maana wakishaiba kura, au wakaamua kuiba maamuzi ya wananchi kwa kujitangaza ni washindi, wakishaunda Serikali wanaendelea kuiba kodi za wananchi kila mwaka (reports za CAG) zinathibitisha hilo. Wanaendelea kupora mpaka rasilimali za nchi (IGA kwenye bandari, mikataba ya kupora mbuga za wanyama na hifadhi za misitu, viwanja vya ndege na mradi wa mabasi ya mwendokasi; vyote vinathibitisha hilo).
Nape, aliyoyasema siyo kwa bahati mbaya. Anajua jinsi ambavyo wamekuwa wakifanya wakati wote kwenye uchaguzi. Anajua kuwa CCM haitegemei kura za wananchi. Kuondoka kwake CCM lazima iwe ni kwa nguvu, na siyo sanduku la kura. Awali Nape aliwahi kusema kuwa CCM ni lazima ishinde, isipopata kura za wananchi, inaenda na bao la mkono, yaani kupora ushindi wa vyama vingine kwa njia chafu. Rais Samia naye aliwahi kutamka kuwa wananchi hata wakivipigia kura vyama vya upinzani, lakini kura hizo walizowapa wapinzani zitahesabika CCM.
Bashiru naye aliwahi kusema kuwa CCM itashinda kwa kutumia dola.
Safari hii Nape amefafanua ni namna gani CCM huwa inafanya kwenye bao la mkono, na ni kwa namna gani zile kura za wapinzani huwa zinahesabiwa CCM, kama alivyowahi kutamka Rais Samia. Nape alichokisema ni kuwa wanaitumia Tume ya Uchaguzi kupitia wasimamizi wa uchaguzi. Na hiyo ndiyo sababu kuu ambayo Rais Samia amekataa kabisa kuifanya Tume ya Uchaguzi kuwa Huru, katika ile maana halisi ya kuwa huru.
Tumshukuru sana Nape kwa kukiri bila woga kuwa CCM huwa wanapora maamuzi ya wananchi, jambo ambalo kila.mtu alikuwa anajua. Hapa mchawi ameingiwa na utashi angalao wa kuunena uchawi wake na jinsi ambavyo amekuwa akiwaua wanadamu wenzake.
Wananchi tutambue kuwa chini ya CCM, kamwe wizi, ufisadi na kila uchafu, haviwezi kwisha. Aliyeingia kwa uchafu, uchafu unakuwa ndiyo dini yake, hawezi kuja kuusaliti uchafu ambao ndio ulimpa madaraka ambayo daima anayataka.
PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Nape Nnauye: Kauli ya "Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza" ilikuwa ni ya utani
- Uchaguzi 2020 - Samia Suluhu: Hata mkipigia kura kule kwingine CCM ndio inaenda kuunda Serikali, tutashinda vikubwa sana Tanzania
- Dkt. Bashiru: Aliye na dola ndiye ananufaika nayo kubaki madarakani, hata CHADEMA ikiingia madarakani ikaondolewa kwenye dola ni uzembe wao
- Kuelekea 2025 - Huyu ndiyo waziri anayetupa majibu kuwa hakuna uchaguzi wa haki hapa Tanzania