SI KWELI Nape atahadharisha kufanywa kwa siasa za kijinga, asema zitagharimu roho na damu za watu

SI KWELI Nape atahadharisha kufanywa kwa siasa za kijinga, asema zitagharimu roho na damu za watu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Nimekutana nahii post kwenye mitandao ya kijamii kwenye akaunti yenye jina la mbunge wa Mtama ikitahadharisha watu kufanya siasa za kijinga akidai zitagharimu roho za watu na damu.

Je post hii ni hali halisi na imechapishwa na Nape mwenyewe?

1722596591686.png
 
Tunachokijua
Nape Nnauye (46) ni Mwanasiasa wa Tanzania na Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Amewahi kushika nafasi mbalimbali serikalini, ikiwemo kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo wakati wa Utawala wa Hayati Magufuli.

Nape Nnauye alichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Mtama tangu mwaka 2015 hadi sasa. Pia, aliteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari mwaka Januari 8, 2022 (Soma Hapa) na kutenguliwa nafasi hiyo Julai 21, 2024 (Soma hapa).

Mnamo Agosti 1, 2024 kupitia mtandao wa X limeonekana Chapisho la Akaunti inayoitwa Nape_Moses na na picha ya Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama likionya kuhusu siasa za kijinga nchini huku likitishia kuwa siasa hizo zinaweza kugharimu roho na damu za watu (Soma Hapa)

Upi ukweli kuhusu chapisho hilo?
JamiiCheck imefanya ufuatiliaji wa Akaunti na chapisho hilo katika mtandao wa X na kubaini kuwa andiko hilo si la Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama bali limechapishwa katika akaunti inayotumia jina lake inayojiita Nape_Moses. Aidha, ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa akaunti rasmi ya X ya Kiongozi huyo inatumia jina la Nnauye_Nape na imethibitishwa kwa tiki ya bluu na kwa sasa ameifunga.

Katika kufuatilia zaidi JamiiCheck imebaini kuwa mtu aliyechapisha andiko hilo ameweka taarifa kwenye bio yake kuwa amezaliwa 1998 wakati Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama amezaliwa Novemba 7, 1977

1722600962833-png.3059651

Akaunti inayotumia jina la Nape Nnauye

1722601824598-png.3059657

Akaunti rasmi ya Mbunge Nape Nnauye
Aidha, JamiiCheck imewasiliana na Nape Nnauye kupata uhalisia wa chapisho lililowekwa na Akaunti hiyo yenye jina lake ambaye amekanusha kuhusika na akaunti hiyo.
Hapo jamiiforums mmefanya vema,maana juna wananchi huamini chochote bila kujir8dhisha kama ni kweli au laa!
Ikiwezekana msiwe mnaweka taarifa bila ya kujiridhisha kama ni kweli mhusika kaitoa au laa!
 
Ngoja tusubiri kwanza, likitokea la kutokea ambalo litafanana na yaliyopo kwenye Acc fake, tutajiuliza sana je kweli ni Acc fake, time shall tells!
 
Hivi inakuaje haya mambo kuhusianishwa?

Kuna nini kati yake??
 
Back
Top Bottom