Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
![]()
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametaka kupewa maelezo maalum ya kimaandishi juu ya mwenendo wa mwimbaji wa nyimbo za Injili, Rose Muhando ili aweze kuchunguza madai ya utapeli yanayosemwa juu yake.
Nape alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa endapo atafanyia kazi tuhuma zilizotolewa na waandaaji wa Tamasha la Pasaka la kila mwaka, Msama Promotions, waliodai mwimbaji huyo hakutokea jukwaani, licha ya kupewa malipo yake na stahiki zingine zilizostahili.
![]()
“Kwanza ieleweke kuwa mimi sikuambiwa, ila nilisikia wakiwatangazia watu waliokuwepo uwanjani juu ya kutokuwepo kwa Rose kwenye tamasha hilo. Sasa mimi siwezi kufanya kazi kwa maneno ya mtaani, kama kuna wasanii wanatapeli, niletewe maelezo kimaandishi yakiwa na ushahidi wa tuhuma zao, hapo ndipo nitaweza kujua hatua za kuchukua,” alisema.
Awali, ofisa mmoja wa Msama Promotions aliyeomba hifadhi ya jina lake kwa kuwa siyo msemaji, alisema Rose alikuwa amepewa malipo yote, ikiwa ni pamoja na usafiri wa gari la kumtoa Dodoma hadi Mwanza, lakini hakuweza kutokea katika onesho hilo.
“Tulishamalizana na Rose na kila mmoja alijua atakuwepo, lakini tunashangaa mara ya mwisho hapatikani kwenye simu na hatujui kapatwa na masaibu gani,” alisema ofisa huyo.
Source: Naniliu
Hamna cha dhoruba Bali Ni kiburi chake tu usiweke maslahi mbele kwenye Kazi ya Mungu. Kiburi hiki shetani kawateka watumishi wengi Sana hasa waimbaji na baadhi ya wahubiri ukimsikia mwimbaji wa injili anadai milioni kadhaa ndio atokee kwenye kuinjilisha huyo ujue Ana pepoMaskini huyu mama sijui anayo yapitia, alikuwa anaeleweka ila sijui dhoruba gani imemkumba. Mungu amsaidie aione njia tena
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji39] [emoji15] [emoji15] [emoji15]Khaaaaaa !!!!!! Rose atapata dhambi hataki kumuimbia Mungu ???
Msama na Rozi wanajuana sana, baada ya Producer huyo kuingiza mambo ya kidunia zaidi kwenye habari za Mungu. Anavuna anachopanda.huyu rose mbona analalamikiwa kwa huu utapeli!na hao msama mbona walishamlalamikia sana inakuwaje wanaendelea kumpa hela ili hali wanajua ni tapeli!
Ongea polepole mi nitakuelewaHamna cha dhoruba Bali Ni kiburi chake tu usiweke maslahi mbele kwenye Kazi ya Mungu. Kiburi hiki shetani kawateka watumishi wengi Sana hasa waimbaji na baadhi ya wahubiri ukimsikia mwimbaji wa injili anadai milioni kadhaa ndio atokee kwenye kuinjilisha huyo ujue Ana pepo
That was my point brethrenTatizo ni kuifanya inayoitwa huduma ya Mungu biashara.
Ulikuwa unapendekeza ifanyikaje?Tatizo ni kuifanya inayoitwa huduma ya Mungu biashara.
Waziri nae anakubali vipi kushughulikia case ya mtu mmoja mmoja? Atashughulikia ngapi? Au ndo kutaka sifa tu?kwa hiyo waziri ndio polisi/mahakama?? Msama vipi tena?