Nape: CCM bado ina imani na tume ya katiba nchini

Nape: CCM bado ina imani na tume ya katiba nchini

W.J.Malecela should take a chill pill and relax,This Constitutional Proposal is for the National interest and not for the Chama cha Mapinduzi's interest.Malecela Junior should take that into his big head.

Tatizo lao wanajisahau na kuzani Serekali tatu ni Mapendekezo ya warioba au ya tume, Kumbe ni mapendekezo ya Watanzania walio wengi, na wanaotaka serekali mbili ni MACCM amabao hata 5Mil hawafiki.
 
Nape Nnauye,
Hiyo mijadala unaifanyia wapi ili nasi watanganyika tujumuike nawe kujadiliana kwa hoja? Hatukuoni kwenye mijadala yoyote; Vinginevyo, kwa manufaa ya CCM, ni muhimu kamati kuu ya CCM (wewe ukiwa ni mmoja wa wajumbe wake) muelewe kwamba imefikia mahali ambapo wananchi wengi wataweza kustahimili kwa urahisi sana kifo cha ccm kuliko watakavyoweza kustahimili kifo cha Tanganyika;
Nape Nnauye , inasikitisha sana kijana wa umri huo una upeo huo.
Kwanza ulianza kuwalaani wazee wafe kwasababu hawana lolote, hujawaomba radhi.

Nape Nnauye huwezi kueleza faida za serikali 2 au kwanini hataki 3 anachofanya ni kutumia nafasi yako kuuvuruga umma. Nape nchi aliyoiongoza baba yako si nchi unayoidhani wewe ni kiongozi.

Unakuja na propaganda eti wananchi wengi katika mabaraza ya kata wametaka serikali mbili.
Tulijua kwanini kulikuwa na ugomvi kati ya wapinzani na CCM katika kuunda mabaraza ya kata na hata bunge la katiba.

Tunajua mnachotaka ni kufanya 'uhalifu' wa kuteka hoja na matakwa ya wananchi kwasababu tu nawe unataka kumrithisha mwanao kiti cha uenezi kama ulivyorithishwa kutoka kwa baba yako.

Tunakuhakikishia kuwa siyo CCM tu itakayokabiliana na umma, serikali itakabiliana na umma na wewe ulieyjipambanua kuwa mmoja wa wanaotaka dhuluma ifanyike utakutana na nguvu ya umma.

Wewe ni mjumbe wa kamati kuu na NEC, kawaambie kuwa jaribio lolote la kufanya kinyume na matakwa ya umma litakutana na nguvu ya umma tu.

Nape ni bora ukae kimya kama msaliti mkubwa sana wa Tanganyika.
Ipo siku isiyo na tarehe utajutia usaliti huo. Hutaweza kuizuia tarehe hiyo iliyonjiani.

Tunafahamu kwa Tanganyika wewe ndiye kiongozi wa kikundi kidogo sana cha wasaliti.
Hata pale maojrity ya viongozi/wasomi na wazee wakiwemo walioishi zama za Tanganyika wakiitaka Tanganyika wewe umekuwa ni msaliti. Unatumiwa na kundi fulani kilisaliti taifa la Tanganyika kwa pesa mbili.

Hakikisha azma yako ovu dhidi ya Tanganyika inafanikiwa, vinginevyo gharama zake kisisa na kijamii zutakuelemea, ipo siku umma utakutomasa madole ya machoni wakikutemea mate msaliti mkubwa wewe.

John Tendwa keshafutika katika magazeti na tunamuomba mungu atusadie afutike katika kumbu kumbu za fikra zetu na nchi hii haraka iwezekanavyo.
Makamba yuko wapi?
 
Mkuu @W.J.Malecela nilidhani muda uliokaa nje ya nchi umekusaidia lakini sioni hilo katika mawazo yako upo kama wazee wa kijijini aliyenyimwa elimu ili aweze kutawaliwa,aliyenyimwa fursa ya kupata habari ili mawazo na fikra zake zake zidumae na hatimaye akubali umasikini alionao ni mpango wa Mungu wakati rasilimali zilizomzunguka ardhi,madini and other resources ni kwaajili ya warasimu waliojazana katika mawizara yetu.

- Binafsi sina imani kabisa na hii tume kwa sababu hawana busara wala ustaarabu, CCM ni chama cha Siasa sio cha mpira wa miguu ni lazima isimamie interest yake kwa kuwaelimisha wanachama wake what is good and what is not good in the long run kwa CCM as chama cha siasa chenye lengo la kushika dola. Hawa kamati ya tume ya Katiba kwa nini wasianzishe chama cha siasa cha kutaka Serikali Tatu?

- Hawawezi kupitisha agenda zao under the expense of Kamati ya Katiba, mimi siwapendi hasa pale wanapojaribu kutumia nguvu kubwa sana na vitisho kulazimisha wanachama wa CCM kukubali mawazo yao mgando sana, waondolewe haraka sana!!

Le Mutuz
 
Nape Nnauye,
Hiyo mijadala unaifanyia wapi ili nasi watanganyika tujumuike nawe kujadiliana kwa hoja? Hatukuoni kwenye mijadala yoyote; Vinginevyo, kwa manufaa ya CCM, ni muhimu kamati kuu ya CCM (wewe ukiwa ni mmoja wa wajumbe wake) muelewe kwamba imefikia mahali ambapo wananchi wengi wataweza kustahimili kwa urahisi sana kifo cha ccm kuliko watakavyoweza kustahimili kifo cha Tanganyika;
Hapo ni kweli kabisa heri kifo cha CCM kuliko Kifo cha Tanganyika yangu.
Kitu wanachokosea ni kusema hii Rasimu ichambuliwe kichama zaidi, wakati havihusiani ni
RASIMU YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Ikiwa imebeba kila Sura na kila kurasa habari za Serikali 3, sasa ukiondoa kipengele chochote na kusema ni Serikali 2 ina maana umetoka nje ya Reli na huko mbele huwezi kurudi.
Kuna vigingi vingi tu ambavyo Treni ya Serikali mbili haiwezi kuvuka asilani na hata tukija kwenye Bunge la Muungano lenye Wabunge wasiozidi 40 haliruhusiwi kujadili au kutunga Sheria inayohusu Mambo ya Tanzania Bara au Baraza la Wawakilishi la Zaznibar ni BATILI (SURA YA TISA Kif 109 aya (2), (3), (4) kwa hiyo inaonyesha wazi kuwa wao Zanzibar tayari wana katiba yao sisi Watanganyika bado na CCM wanataka tutumie tu hiyo ya Muungano.
Ndio maana nasema hapa Vyama vya SIASA havitakiwi ni Raia wote watoe maoni. Mchambuzi naona Nape Nnauye angesoma ile post yako ya
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-lao-na-hatima-ya-muungano-6.html#post6985858
angejua Watanzania wote sasa wamebadilika hawapo tena Kisiasa zaidi ila kimaslahi na hawatishani tena ukweli ubaki ukweli tu
 
Tatizo la ccm kupishana kimtazamo na kamati ya katiba,ni ccm kulazimishwa kucheza ngoma wasiyoijua,na tatizo la kudandia hoja kwani ukiangalia kwenye ilani yao ya uchaguzi hawakuwa wameipa kipaumbele kubadilisha katiba lakini mara waliposikia upinzani wameansika kwenye ilani yao kwamba wataandika katiba mpya nao wakaidaka,sasa inafikia Nape anawatukana wazee kwamba wanaotaka Muungano wa Swrikali tatu ni wazee wanaosubiri kufa,Hebu akumbuke baada ya kutoa kauli hiyo Mengi alimjibu nini? Leo anajidai kasahau na wengi waliochaguliwa kuandika hiyo Katiba mpya ni wazee kwa hiyo wanasubiri kufa hao watu

Tatizo la Nape ni utoto na ujinga anasema neno halafu anasema alilishwa hakusema ni akili ndogo,kumbuka watu wanakumbuka na siku zote mla ndizi husahau ila mtupa maganda hasahau

Nape wapo watu ambao hawana shule kama wewe i mean hawakusoma kama wewe lakini wanakuzidi kwa kila kitu hekima,busara kwa hiyo kudhani kwamba unaweza kuwadanganya watu
 
Mkuu @W.J.Malecela nilidhani muda uliokaa nje ya nchi umekusaidia lakini sioni hilo katika mawazo yako upo kama wazee wa kijijini aliyenyimwa elimu ili aweze kutawaliwa,aliyenyimwa fursa ya kupata habari ili mawazo na fikra zake zake zidumae na hatimaye akubali umasikini alionao ni mpango wa Mungu wakati rasilimali zilizomzunguka ardhi,madini and other resources ni kwaajili ya warasimu waliojazana katika mawizara yetu.

- Ni maneno ya Upinzani ila hayana anything to do na the ishu hapa, eti msimamo wako ni upi maana wangu umeuona?

Le Mutuz
 
Mkuu W. J. Malecela hoja ya katiba mpya si suala la chama kama CCM inavyolichukulia sasa,hili ni suala la kitaifa ukianza kuichambua katiba kwa kufuata itikadi ya chama hakika utajikuta unapigania mfumo utakao linda maslahi ya chama badala ya maslahi ya taifa.

Sera ya serekali mbili imezalisha kero nyingi hasa kutoka upande wa Zanzibar,ni ajabu kero hizo tumeanza kuzisikia hata upande wa Tanganyika.Sasa anapotokea mtu mzima kama wewe unayeelewa matatizo ya muungano bado unashikilia msimamo wa serekali mbili lakini hapo hapo unashindwa kutoa maelezo jinsi utakavyo ondoa kero zinazosababishwa na mfumo wa sasa !.Bwana Malecela lazima uzingatie tume ya Mzee Warioba imetumia fedha nyingi za walipa kodi,bahati mbaya hilo CCM hawalioni wapo tayari kuvuruga kazi nzuri ya Mzee Warioba kwa mtazamo wa kulinda maslahi ya kisiasa badala ya kulinda maslahi ya nchi.

Napenda kukuhakikishia mnaweza kulazimisha serekali mbili lakini hiyo itakuwa ni solution ya muda mfupi sana tena pengine kuliko mlivyotarajia.



- Ni maneno ya Upinzani ila hayana anything to do na the ishu hapa, eti msimamo wako ni upi maana wangu umeuona?

Le Mutuz
 
Last edited by a moderator:
- Ni maneno ya Upinzani ila hayana anything to do na the ishu hapa, eti msimamo wako ni upi maana wangu umeuona?

Le Mutuz

Nafikiri umefika wakati sasa..tukaacha kila kitu kusingizia UPINZANI.....ndugu kinachotakiwa ni mfumo wa kuifanya hili taifa lisonge mbele......naamini kama hili swala lingeshughulikiwa tangu kile kipindi Baba yako na wenzake wadai serekali ya Tanganyika...leo hii tusingetumia mamilioni ya wapiga kura kuunda tume

haiingii akilini tume muunde nyie sasa mnaanza kukana matokeo ya kazi ya mliyoipa.....kwani hiyo RASIMU kaandika WARIOBA NA FAMILIA YAKE????kwani hiyo RASIMU ndo mawazo yake au ya TUME?

Ni vema MKAACHA UNAFIKI....tatizo lenu mnajidanganya mtatawala milele,,,,,,na mtarisishana madaraka tu kama mnavyopenda....hilo sahauni.....kumbuka kinachotakiwa ni mfumo ambao waote kama taifa tutaufuata....watawale CCM...CUF waufuate.....sasa nyie mnangangania mawazo yenu (namaanisha chama chanu) ndo yaungwe mkono na wote????

Hata mkifanikiwa...hamjawahi jiuliza....CUF wao msimamo wao ni nini? na Je wakichukua nchi watasimamia msimamo wa chama chenu????

Nilichokigundua WANA CCM wengi ni wanafiki, na siasa ndio zainawapa mikate yenu ya kila siku ndio manaa mnashindwa kusimama na hoja zinazokingizana

Umeishi nje...tulitegemea..ungekuja na mtizamo chanya kumbe hakuna lolote.....
 
Wanaibisha chama cha mapinduzi
"Natamani kufanya mapinduzi"
"Vox popoli vox dei"
 
lkn tume haijachambua ni kivipi hii serikali 3 itaendeshwa......na pia wapi makao makuu ya serikali
 
Back
Top Bottom