DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema kuwa katika vikao vyake CCM haikukurupuka kumpitisha Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bali walijiridhisha kuwa mgombea huyo anatosha, ni mzalendo na muumini wa utu wa binadamu hivyo anaweza kuongoza na kuleta maendeleo nchini.
Akimnadi mgombea Urais Kupitia CCM, Dkt.Samia Suluhu Hassan leo Septemba 29,2025 Pangani mkoani Tanga, Nape ametoa ushahidi wa kuthibitisha kauli yake akisema kuwa Dkt. Samia amefanya mambo makubwa ikiwemo kuendeleza miradi aliyoikuta, kuongeza fursa za ajira pamoja na kuongeza mapato ya Serikali.