Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Kwa matamshi ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape aliyoyatoa majuzi huko Kagera, kuhusu mbinu anazozijua yeye ya namna ya kupata ushindi Kwenye chaguzi zetu na mbinu hizo hizo, akamfundisha Mbunge Byabato, kuwa kushinda uchaguzi hapa nchini, inategemea ni nani anahesabu kura na nani anatangaza matokeo hayo na hakutokani na matokeo ya box la kura!
Hiyo ni kashfa kubwa sana ambayo inaweza kusababisha machafuko makubwa nchini ya umwagikaji wa damu, ambapo alistahili Mheshimiwa Nape, ajiuzulu mara moja na kama hataki kujiuzulu, mamlaka iliyomteua, ambayo ni Rais atengue uteuzi wake mara moja.
Kinyume chake hatuoni dalili zozote za Nape kujiuzulu wala Rais aliyemteua kufanya maamuzi ya kumtimua kazi!
Tafsiri tunayopata sisi wananchi ni kuwa, hata Rais anaunga mkono kauli hiyo ya Nape, kuwa matokeo ya kura za nchi hii, hayategemei box la kura, bali inategemea Tume ya uchaguzi, inayotangaza matokeo!
Mimi naamini ingekuwa kwenye nchi nyingine inayotekeleza Demokrasia Kwa umakini, ni lazima mtu wa aina ya Nape angewajibika mara moja kabla hata ya kusubiri mamlaka iliyomteua, kumfukuza kazi.
Kitu kingine ambacho nimekibaini ni kuwa hata hizi 4R's anazojidai nazo Rais Samia, kumbe ni changa la macho!😎
Kitu kingine kinachonishangaza ni kuona kuwa Katibu wa Uenezi wa CCM, ameikana kauli hiyo ya Nape, lakini wakiendelea kumkumbatia!
Sasa kama Katibu Mwenezi wa CCM ameikana hiyo kauli ya Nape na kuiita ni yake binafsi, inayodai kuwa CCM hawategemei, kura zinazopigwa katika mabox ya kura, je ni kwanini nyiye CCM mnaendelea kumkumbatia Nape??😎
Pia soma: Kuelekea 2025 - Nape: Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza, ili mradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe!