Pre GE2025 Nape kuendelea kung'ang'ania madarakani na Rais Samia kuzidi kukaa kimya kunazidi kuiangamiza CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hii kauli ya NAPE ameitoa kipindi kibaya kuelekea uchaguzi mkuu ni kauli yenye ukweli lakini Rais asipoizungumzia na kuwapa confidence wananchi kwenye uchaguzi huu inatengeneza majeraha siyo kwa upinzani tu hata kwa CCM yenyewe na wananchi kwa ujumla.
 
Kwa matamshi ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape aliyoyatoa majuzi huko Kagera, kuhusu mbinu anazozijua yeye ya namna ya kupata ushindi Kwenye chaguzi zetu na mbinu hizo hizo, akamfundisha Mbunge Byabato, kuwa kushinda uchaguzi hapa nchini, inategemea ni nani anahesabu kura na nani anatangaza matokeo hayo na hakutokani na matokeo ya box la kura!

Hiyo ni kashfa kubwa sana ambayo inaweza kusababisha machafuko makubwa nchini ya umwagikaji wa damu, ambapo alistahili Mheshimiwa Nape, ajiuzulu mara moja na kama hataki kujiuzulu, mamlaka iliyomteua, ambayo ni Rais atengue uteuzi wake mara moja.

Kinyume chake hatuoni dalili zozote za Nape kujiuzulu wala Rais aliyemteua kufanya maamuzi ya kumtimua kazi!

Tafsiri tunayopata sisi wananchi ni kuwa, hata Rais anaunga mkono kauli hiyo ya Nape, kuwa matokeo ya kura za nchi hii, hayategemei box la kura, bali inategemea Tume ya uchaguzi, inayotangaza matokeo!

Mimi naamini ingekuwa kwenye nchi nyingine inayotekeleza Demokrasia Kwa umakini, ni lazima mtu wa aina ya Nape angewajibika mara moja kabla hata ya kusubiri mamlaka iliyomteua, kumfukuza kazi.

Kitu kingine ambacho nimekibaini ni kuwa hata hizi 4R's anazojidai nazo Rais Samia, kumbe ni changa la macho!😎

Pia soma: Kuelekea 2025 - Nape: Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza, ili mradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe!
Bado hamjasema 😆😆👇👇

View: https://twitter.com/Aduiwayanga/status/1814243185809318150?t=WSohD3LVscW6u_l-70CoxA&s=19
 
Hii kauli ya NAPE ameitoa kipindi kibaya kuelekea uchaguzi mkuu ni kauli yenye ukweli lakini Rais asipoizungumzia na kuwapa confidence wananchi kwenye uchaguzi huu inatengeneza majeraha siyo kwa upinzani tu hata kwa CCM yenyewe na wananchi kwa ujumla.

Kwani hiyo kauli ina Jambo gani la uongo?
 
Huo ndio ukweli, kila mtu anaenda na Jambo lake, mwingine kumuona Tu Rais, au kuona msafara, au kusikiliza hotuba na wengine ni kushangaa wasanii
Mlisema mnamchukia sana na hana watu,vipi tena mkamuone? 😂😂
 
Hiyo nyomi inayotokana na msafara wa magari yasiyopungua 150, ambayo yanalipiwa mafuta Kwa Kodi zetu, Wala Sina wasiwasi nao hiyo nyomi
Ndio nasema hivi Bado hamjasema.

Vipi Ile nyomi ya msafara wa chopa? 😆😆😆😆😆
 
1721396608213.jpeg
 
Kwa matamshi ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape aliyoyatoa majuzi huko Kagera, kuhusu mbinu anazozijua yeye ya namna ya kupata ushindi Kwenye chaguzi zetu na mbinu hizo hizo, akamfundisha Mbunge Byabato, kuwa kushinda uchaguzi hapa nchini, inategemea ni nani anahesabu kura na nani anatangaza matokeo hayo na hakutokani na matokeo ya box la kura!

Hiyo ni kashfa kubwa sana ambayo inaweza kusababisha machafuko makubwa nchini ya umwagikaji wa damu, ambapo alistahili Mheshimiwa Nape, ajiuzulu mara moja na kama hataki kujiuzulu, mamlaka iliyomteua, ambayo ni Rais atengue uteuzi wake mara moja.

Kinyume chake hatuoni dalili zozote za Nape kujiuzulu wala Rais aliyemteua kufanya maamuzi ya kumtimua kazi!

Tafsiri tunayopata sisi wananchi ni kuwa, hata Rais anaunga mkono kauli hiyo ya Nape, kuwa matokeo ya kura za nchi hii, hayategemei box la kura, bali inategemea Tume ya uchaguzi, inayotangaza matokeo!

Mimi naamini ingekuwa kwenye nchi nyingine inayotekeleza Demokrasia Kwa umakini, ni lazima mtu wa aina ya Nape angewajibika mara moja kabla hata ya kusubiri mamlaka iliyomteua, kumfukuza kazi.

Kitu kingine ambacho nimekibaini ni kuwa hata hizi 4R's anazojidai nazo Rais Samia, kumbe ni changa la macho!😎

Kitu kingine kinachonishangaza ni kuona kuwa Katibu wa Uenezi wa CCM, ameikana kauli hiyo ya Nape, lakini wakiendelea kumkumbatia!

Sasa kama Katibu Mwenezi wa CCM ameikana hiyo kauli ya Nape na kuiita ni yake binafsi, inayodai kuwa CCM hawategemei, kura zinazopigwa katika mabox ya kura, je ni kwanini nyiye CCM mnaendelea kumkumbatia Nape??😎

Pia soma: Kuelekea 2025 - Nape: Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza, ili mradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe!
Tatizo la CCM siyo Nape. Wakosoaji wengi wa serikali ya CCM huwa wanajisahau na kuanza kutoa ushauri wa nani aondolewe na nani abaki utadhani CCM ni chama chenye viongozi wazuri sana ila tu wana kasoro ndogo ndogo.
 
siyo jambo la uongo Alilosema Nape,ila tuzingatie usemi wa USILE NA KIPOFU UKAMSHIKA MKONO.
Alilosema Nape, ndiyo ukweli halisi Kwa asilimia 100.

Lakini kinachowashangaza maccm, ni kwanini amemwaga mchele mbele ya kuku wengi?
 
Inashangaza kuona Rais Samia yuko kimya, anajifanya eti haoni huu uvunjifu wa hali ya juu wa utawala wa sheria

Ataonaje, ikiwa yeye mwenyewe huko gizani anafurahia na kutegemea wizi wa kura? Matendo husema kwa nguvu zaidi kuliko maneno.
 
Back
Top Bottom