OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 426
- 685
Nimemsikia Waziri Nape akisema serikali italinda uhuru wa kujieleza (Serikali italinda uhuru wa kujieleza). Maneno haya yametokana na serikali kuwasilisha Marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari tarehe 10 Februari 2023 bungeni
Je, ni kweli yanalenga kuimarisha uhuru wa kujieleza nchini?
Marekebisho yaliyowasilishwa bungeni ni yale yanayohusu makosa ya herufi au maneno na masuala ya adhabu ya vifungo na faini ambavyo vimepunguzwa.
Vifungu vingine ni kuhusu matangazo na vifungu vinavyoruhusu serikali kuvishishikilia vifaa vinavyodhaniwa kuwa vimeshiriki kufanya uchochezi.
MAMBO MUHIMU AMBAYO WANAHABARI WALIYATAKA
Ili kukuza uhuru wa habari nchini, wanahabari walihitaji vifuatavyo
1. Neno "Uchochezi" kupewa maana, suala ambalo mapendekezo ya tarehe 10 hayajaliweka na neno hilo linazidi kuwa tata.
2. Makosa ya kichochezi kutokuwa Jinai. Badala ya kuondoa jinai kwenye makosa haya, mapendekezo yamepunguza adhabu tu, hali ambayo inafanya makosa hayo yaendelee kuwaondoa wanahabari wengi masoko ya kimataifa ikiwa watakuwa wamekamatwa na jinai.
3. Ili kupeusha masuala ya kufungia fungia vyombo vya habari, wadau walishauri kupunguza mamlaka ya waziri aliyopewa na sheria. Kifungu 58 na 59 cha Media Services Act 2016 hakikuguswa.
Nape, mapendekezo yaliyoenda bungeni hayaongezi uhuru wa habari kwa namna yoyote. Yaani ni sawasawa na hakuna kilichofanyika.