Nape na Chalamila mna la kujifunza katika kipindi hiki kifupi

MIGNON

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2009
Posts
4,108
Reaction score
5,110
Nape alijitokeza na kutishia wote waliouliza kuhusu alipo Makamu wa Rais. Kwa kipindi kifupi alipigwa spana Tweeter za kutosha.

Hazikuwa spana kavu bali na vifungu vya sheria na katiba na kidogo wakampekua hata mambo yake mengine. Ametulia!

Chalamila alijivika Uamiri Jeshi (kwa cheo cha Mwenyekiti wa kamati ya usalama ya mkoa (neno ulinzi limeondolewa).

Alichokutana nacho leo kafanya usafi na wajumbe.

Hii nchi ni yetu sote tusimamie zaidi katika sheria na katiba kuliko Uchama.
 
Walimpigia mbuzi uzi wa gitaa
 
Samahani nipo nje ya mada wakuu kwani Leo usafi ulifanyika?
Ufanyike wapi, huyo Chalamila alikuwa anataka kuendekeza siasa chafu, lakini nadhani wanajeshi waligomea huo upuuzi.
 
Aliyemteua Chalamila, anaemsikiliza na kumtilia maanani Chalamila wote wana hitilafu katika uelewa na akili zao.

Chalamila ni debe tupu kuliko madebe matupu yote ya CCM. Jamaa ni pumbavu la mwisho kabisa.

Kuhusu swali lako, nina akiba ya Mil kama 100 kwenye mikeka ya kubeti, ukitiki huo basi mambo yatakuwa muswano
 
Rais Samia tayari ameingia katika Kitabu Cha KUMBUKUMBU, Marais wa kiume wote waliogopa maandamano, mama amedhihirisha ni mlezi. Aliyepita alisema uchaguzi ukiisha basi hakuna mikutano mpaka miaka 5 ipite, mama mlezi ameruhusu. Aliyepita alisema mwanafunzi anayezaa akiwa shule asirudi shuleni, Mama mlezi ameruhusu. Aliyepita alisema mkurugenzi ambaye eneo lake atachaguliwa mpinzani Hana kazi, hili Sasa mama mlezi aruhusu sanduku la kura lichague aliyechaguliwa na Wananchi, siyo achague yeye kama aliyepita. HONGERA sana mama mlezi, waliyoshindwa wanaume,wewe umeweza.
 
umenena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…