Lyambalyetu
JF-Expert Member
- Apr 6, 2021
- 278
- 255
Dkt. Mwigulu wewe unatakiwa kucheza vizuri tu na watu wako ambao wanasemwa semwa kuwania ubunge jimboni Iramba, usijaribu kumpuuza Prof. Kitila Mkumbo na Gwajima pia. Wapo kadhaa na wengine wameshajitambulisha mpaka level ya kitaifa chamani. Sitawataja hapa lakini jua wapo na ni watu smart kweli kweli - wengine ni vijana wadogo tu below 40yrs.
Unajaribu kuwa makini na kuepuka mitandao inayoanza kwa sasa ikiwepo mtandao wa Januari na Nape. Kuna mtandao pia wa Bashe na Musukuma lakini ninaona unajitahidi sana kujiondoa kwao. Pamoja na kuwa tabia zako ni taofauti sana na Juma Aweso pamoja na Doto Biteko lakini hao ndiyo unapaswa uwafuate kwa matendo na tabia zao. Ni wastaarabu wa hali ya juu, wanyenyekevu na wanajua uongozi kuwa sio ubabe au ubosi bali ni kuongoza kwa vitendo. Tabia zako zile za kutokeza kifua na kichwa chako kwenye gari na kuhutubia kama Mkuu wa nchi uziache. Tabia zako za kuongea KiNyiramba chetu ukiwa jimboni uziache kwani unafuatiliwa kwa karibu sana. Usijaribu tena kale katabia ka kujitangaza kwenye mawe nchi nzima. Zaidi ya yote yule mke wa mtu uliyempa uongozi chamani pamoja na elimu yake ya kuunga unga mwishowe atakudondosha, bahati mabaya hata ukuu wa wialaya hana sifa ya kupewa. Timu yako uliyoweka Iramba kukushindisha uchaguzi Iramba haipo kitaifa so ni rahisi sana sana kuparaganyishwa. Jiimarishe Kitaifa lakini kwa ajili ya kupata ubunge isiwe Urais. Kura za maoni ndani ya chama mwaka 2025 kwa jimboni kwako hazitatosha, utapaswa kupata huruma kutoka Taifani, onesha unyenyekevu kwake mama YETU.
Ninajua kweli kabisa kuwa wewe unaliwa timing yaani ukiteleza kidogo tu mwakani kabla ya Agosti, baada tu ya kupita Bajeti utaliwa kichwa mazima mazima na ubunge utapoteza. Kuwa makini POTI Mwigulu!