Nape na Makamba mjue kujaribu kumshusha thamani Hayati Magufuli, ni sawa na kumfuata mamba kwenye kina kirefu cha maji

Nape na Makamba mjue kujaribu kumshusha thamani Hayati Magufuli, ni sawa na kumfuata mamba kwenye kina kirefu cha maji

Etwege

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2018
Posts
7,207
Reaction score
17,674
Nape Nnauye aliposimama mbele ya bunge na kuhoji matumizi ya mkopo wa Dola bilioni 9 uliokopwa na serikali ya awamu ya tano, Wabunge baadhi waliduwaa na wengine wakagonga meza, walikubali? Hatujui, walikataa? Hatujui?

Aliyekuwa Rais wa Awamu ya nne, Jakaya Kikwete aliwahi kusema kwamba, "Mwenezi wangu akisimama kwenye jukwaa huwa sijui anaenda kusema nini! Na hatabiriki katika anachoenda kukisema. Hapa Kikwete alikiri kwamba Katibu Mwenezi wake wa chama (Nape) huwa hatabiriki katika maongezi yake.

Ni kweli, Nape aliwahi kusema mengi yenye kutia mashaka na hata yenye ukakasi ila akayafanya yaonekane ya kawaida mbele yake. Mmesahau goli la Mkono?

Leo Nape anahoji matumizi ya mkopo wa Dola bilioni 9. Na kutaka uchunguzi ufanyike wa matumizi ya hizo Dola bilioni 9. Inachekesha lakini pengine hajui anachokisema. Uchunguzi hauishii kwenye makaratasi ya kandarasi na matumizi pekee.

Aliyekuwa Waziri wa fedha katika awamu ya tano ni Dr Philip Mpango ambaye ni makamu wa Rais wa sasa, anataka huyu akatoe ushahidi wa matumizi yake mbele ya jopo la wachunguzi? Kwa kifupi Waziri wa fedha ndiye anaeandaa proposal zote za mikopo kulingana na uhitaji na hata msaada wowote ule lazima upitie kwake.

Aliyekuwa Waziri mkuu wa Awamu ya tano ni Kasim Majaliwa, ndo huyuhuyu wa sasa, huyu ndo msimamizi wa shughuli zote za serikali, anajua nje ndani kuhusu hii mikopo, je Nape anataka Majaliwa nae akakae kwenye hiki kikaango Cha mahojiano ya mikopo ya Dola bilioni 9?

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Awamu ya tano ndo huyu Rais wa sasa, huyu alishiriki kwenye vikao na mijadala inayohusu mikopo hii, je anataka na Rais akahojiwe juu ya mikopo hii?

Kuna muda chuki zinaathiri uwezo wa kufikiria! Wataalamu wa afya ya akili wanasema hivi "ukiihifadhi chuki moyoni, sio tu itakunyima Uhuru wa mawazo bali itakudumaza akili, lakini pia inaweza kukusababishia afya ya kimwili"

Nape akubali kwamba awamu ya tano imepita, imemaliza kazi yake, WATANZANIA wanajua na dunia inajua kuwa awamu ile haikuwa awamu ya majaribio. Ilikuwa awamu ya "Hapa kazi tu" na kazi ilionekana na kufanyika. Nimkumbushe Nape kwamba tukianza kuchunguzana chunguzana hatutaishia katika awamu ile pekee, tutafikia makaburi katika awamu pendwa kwake pia. Na pengine tunaweza kuanza kuihoji hata awamu hii kabla ya kumaliza hata mwaka mmoja madarakani.

Lakini tunaweza kubariki uchunguzi hata katika namna ya goli lile la Mkono ikiwa lilitumika ama halikutumika na waliohakikisha ushindi huo unapatikana. Ukianza kila nyama ya mtu kamwe huwezi kuacha.

Kama ilivyo kwa Nape, January nae akajikwaa pale pale alipoteleza Nape, yeye akasema mradi wa ujenzi wa Bwawa la Mwalimu NYERERE lilicheleweshwa kwa zaidi ya siku 400 [emoji23][emoji23] siku 400 ni mwaka na mwezi mmoja, sijajua anazungumzia mradi upi huo.

Akaja na ngonjera kwamba hakuna cranes za kunyanyua uzito wa TANI 26 nchini hadi nje ya nchi, akasahau kwamba hizohizo material zilishushwa bandarini, lakini pia akasahau kuwa kwenye mradi wenyewe hizo cranes zipo. Niseme tu kwamba kwenye mradi wapo ndugu zetu huko wanafanya kazi, alipojichanganya akasema hazipo, ma_opareta wa hizo cranes wameduwaa.

Lakini pia hata zisingekuwepo, hizo cranes zinakodishwa na makampuni kadhaa hapa nchini. January ameendeleza alipoishia Nape. January ameshindwa kutuambia ni KWANINI Kuna mgao wa umeme hivi Sasa, ameshindwa kutuambia WATANZANIA ni kwa sababu gani nchi imeweza kulala kwenye Giza kwa masaa 24 bila umeme katika baadhi ya mikoa na tatizo hilo limesababishwa na nini.

Nape aelewe kwamba wanaoipinga awaku ya tano ni mabwanyenye na sio WATANZANIA masikini. Watanzania wa kipato Cha kati na Cha chini hawako tayari kusikia awamu ya tano ikisemwa vibaya.

Lakini pia serikali ya awamu ya tano ielewe kwamba wananchi wanaoisemea mazuri awamu ya tano ni kwa sababu ya hawahawa VIONGOZI kuisema vibaya awamu ya tano. Kwa hiyo wamejikuta wanavutana na wananchi bila kujua kuwa sababu ya mvutano ni wao wenyewe. Awamu hii ikiacha kuinanga awamu iliyopita, hutosikia mtu akiisema vibaya awamu ya sasa, vinginevyo kitaumana kila siku.
 
Kimsing, kujadili watu kama Nape na Makamba ni kutumia muda wako vibaya; angalau Makamba ni waziri ambaye maamuzi yake yanatuhusu sote, huyu tunaweza kumjadili lakini siyo Nape. Tutaanza kumjadili Nape akipata uteuzi ambao anautafuta sana.
 
Jini jiwe alikuwa mwongo, mzandiki na mfitini.

Alitudanganya kuhusu SGR kipande Cha Dar -Moro kuwa kingeanza mwezi August mwaka 2020 mpk leo zii

Alitudanganya kuwa tunajenga miradi mikubwa kwa fedha zetu za ndani lkn kumbe anakopa kama hana akili nzuri.

Alitudanganya kuhusu reli ya Dar -Moshi/Arusha mpk leo kimya.

Nina hakika hata hiyo kauli ya Kalemani ilikuwa fix tu
 
Moja ya sifa za utawala Bora duniani Ni uwazi kwenye matumizi ya raslimali za Nchi.
Tatizo la watu kuomba taarifa ya matumizi wa fedha zao Ni lipi?
Au unadhani Kama Magufuli alikopa, Ni familia yake watalipa?

Kama alikopa na kutumia kwa mujibu wa taratibu na sheria, hofu ya kuomba ukaguzi inatoka wapi?

Tena nadhani ndio ingekuwa vizuri mikopo hiyo ikakaguliwa ili marehem awe cleared.
Tusianzishe upashkuna usiokuwa na sababu
 
Kwahiyo kinga ya hizo pesa kuchunguzwa ni kwa kuwa kuna viongozi wa juu walishiriki ama nini? Kwani hawa viongozi wa juu hivi sasa wana utakatifu gani mpaka kusifanyike ukaguzi?

Viongozi ambao wako madarakani kwa wizi wa kura wana sifa gani ya kukepwa fedha zilizokopwa kuchunguzwa?

Kama unaowaona wana hadhi hiyo ni ww, maana ulifaidika na matumizi mabovu ya mikopo ile, hivyo unajua ukaguzi ukifanyika ukweli utafahamika na sifa zote za kijinga zitakoma.
 
Back
Top Bottom