Nape ndiye Rais ajaye 2025, akikatwa CCM ataenda upinzani watampitisha

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Kwa kuwa siasa ni mchezo usiotabirika, kadhalika anaeweza kuimudu ni yule mwenye uwezo mkubwa wa kusoma alama za nyakati. Alifanya kosa kidogo kwa kuchelewa kumsoma bosi wake wa awali ila amecheza karata vizuri ambapo kwa sasa ameanza kuteka mioyo ya makundi mbalimbali ndani na nje ya chama.

Ukimlinganisha na wanasiasa wengine tangu CCM mpaka upinzani sioni wa kumshinda.

Tumuombee uzima na afya tele.
 
Nyie mnampa air time sana.
Kama mlivyompa yule wa kulia jicho 1 dc flan hv
 
Nape huyuhuyu mwenye bichwa kubwa kama la harmonize lakini akili kisoda
 
Sawasawa, kila mtu ana Uhuru wa kutoa maoni yake. Umetumia vizuri Uhuru wako.
 
CHADEMA hawawezi kurudia kosa kama lile la 2015. Chama kina hazina kubwa ya viongozi ambao wana sifa za kukiwakilisha chama katika chaguzi nyingi tunazozitarajia siku za usoni.
 
A
Atakua raisi wa ufipa
Kuna mwingine mlimdanganya eti kachero mbobezi mpaka sasa hajulikani alipo.
 
Hahaha.. mzee wa goli la mkono
 
Ahahahahahahahahahaha! Nimemkumbuka Mwanadiplomasia nguli na Kachero mbobezi Bernard Camillius Membe! Hivi, si wanatoka Jimbo moja hawa? Ahahahahahahahahahah!
 
Nimejikuta nacheka kwa sauti dah!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…