Uchaguzi 2020 Nape Nnauye ateuliwa kuwania Ubunge jimbo la Mtama peke yake baada ya wagombea wengine kukosa baadhi vya vigezo

Uchaguzi 2020 Nape Nnauye ateuliwa kuwania Ubunge jimbo la Mtama peke yake baada ya wagombea wengine kukosa baadhi vya vigezo

Nape alipeleka fomu jumapili ,Jana leo mkurugenzi kakimbia ofisi ilikuwa imefungwa kutwa wagombea wengine wakakosa pa kukabidhi fomu .
 
Nape umevuna uvumilivu ulioupanda. Pamoja na misukosuko uliyopitia ndani ya chama, lakini ulitulia na kuwa mwaminifu kwa chama chako. Hongera kwa ushindi pasipo kelele za vyura.
Kumbuka hajachaguliwa na wapiga kura!
 
Nape nilikuwa namuona kama mmoja wa wana CCM wenue uelewa kumbe ni muhuni fulani hivi, nashauri vyama vya ACT na CDM wamkatie rufaa mapema sana
 
CCM 9 Upinzani 0
1.Misungwi,
2.Ruangwa...

tukishindaa akatangazwa
najua tutakuwa na wa ubuge wachache kwa sababu ya figisu za NEC,

kitu Cha Kwanza Ni kufungua kesi za kupinga matokea ya wabunge waliopita kwa usanii nchi nzima,

na kurudia upya uchaguzi katika majimbo yaliyonajisiwa ili kufuta Upumbavu na uchafu wa NEC,

mtu Kama Majaliwa atakuwa na ubunge wa muda mfupi tu.
 
CCM=9 & UPINZANI=0.

kwa hali hii kuna kushinda uraisi kweli ? Naona ndoto za mchana hizi duuuuh
 
Sioni faida ya kuwa na wabunge wa CCM! Hata sijui huwa wanafanya nini pale bungeni....!.
Kazi kuu ya wabunge wa ccm bungeni ni kuitetea serikali na kutunga sheria za kuwakandamiza wanyonge a.k.a malofa na wapumbavu.
 
Ccm haipendwi wanafanya fitina za hovyo tu
Nec iko kimyaa
 
Yani haya mambo ya hovyo sana,mpinzani akirejesha fomu anakutana na vitimbwi ambavyo hata mbinguni havipo Mara Mkurugenzi ayupo mara fomu zimekosewa kujazwa,pamoja na kubambikiwa kesi na kutekwa!.

Yet bado tunataka maendeleo,it will take century! Haya mambo yanayofanywa na chama Tawala ni aibu,karne ya 21 mgombea anapita bila kupingwa.

Kweli biblia iliyosema amani pasipo upanga,hili neno lilikuwa na maana kubwa.
 
Back
Top Bottom