Nape Nnauye: CCM tunapinga Uwepo wa Serikali Tatu.

kashatoka kwenye mizigo karudi kwenye katiba...alisema kweli Kikwete, mwanasiasa ni lazima uwe na agenda muda wote, huwezi kukaa kaa tuu!!!
 
Tutafika? Tufungue mlango wa kila kikundi kiwe huru kuwataka wanakikundi wake kutoa maoni ambayo yatawakilishwa mbele ya Tume sambamba na ya kikundi cha CCM. Makundi haya yanaweza kuwa ya kidini, kisiasa, n.k.
 
Nimeona CCM wametumia nguvu na pesa nyingi kulazimisha kuwa ktk bunge la katiba wabadilishe rasmu ya katiba mpya, kwenye issue ya aina muungano kutoka serikali tatu kana ilivyowekwa na tume na kuwa muungano wa serikali mbili. Wameitisha vikao, semina na washa nyingi kushawishi hili. Lakini kwa kuwa wengi wa wajumbe kwa sasa wamo ccm nusu nusu, na kwa kuwa serikali tatu ni wazo la cdm (wananchi) ambako hawa ndiko wanasubiria kutimukia kuachana na ccm (mafisadi), watapigia kura serikali tatu. Na huu utakuwa ushindi mara 1000 kuliko kushinda jimbo la Karenga kama mmoja anavyo shadadia eti cdm wakishindwa kulichukua wajizuru. CDM wapo zaidi bungeni kwa sasa kuliko kwingine kote. Tanganyika itazaliwa, ccm itakufa chama kama TANU yaani CDM kitatamalaki.
 
CCM haitokufa kwani bado kuna vitega uchumi ambavyo wakuu wanafaidika navyo ,isipokuwa itakuwa ipoipo tu ! Ila sikuelewa mara umelukia CDM ,umedai ikiwa serikali tatu viongozi wa CCM waondolewe ,sio wao ni uongozi mzima wa Serikali ya Muungano watakuwa wamepoteza ajira ndani ya Serikali mpya ya Muungano ,akina Mangula na akina Nape watabakia na Chama Chao ,kiherehere ni kwa hawa wanaoshikilia nafasi ndani ya serikali ya Muungano .hawa hivi sasa matumbo joto ,si ajabu ukasikia wengine presha juu na kupoteza maisha ,sio mchezo.Ndio ukaona wamebaki tunaingia bungeni na wito wa serikali mbili ,yaguju ,mwisho wa serikali mbili umefikia mwisho wake .
 
Kayamgo, Mwiba,Matola wote mabandiko yenu yanakidhalilisha kiswahili.
 

Siyo kubadilisha bali ni mjadala ndiyo maana inaitwa rasimu bado haijawa katiba kamili,hivyo kuitwa dodoma siyo kwenda kuwa rubber stamp ya tume ya warioba bali kujadili kili walichotunga kupitia watu 500,000 tu tena ni hoja kwa hoja na penye marekebisha wana haki ya kufanya hivyo,tuwe waelewa
 

Kwa nini ccm ilifanya kampeini? Katiba inatakiwa kuwa ya wananchi wanavyotaka. Ccm imewalisha watu maneno ya kuong'ea na ya mambo kupigia kura, ni kwa sababu gani. Wale wajumbe ni wawakilishi wa umma, inakuwaje mtu anatokea tu na kuwambia kuwa umma ni sisi, ccm! Hivyo ni sawa?
 
Binafsi nilijua mtoa maada utasema inatakiwa ccm wafukuzwe kwa mantiki ya kuwa watakuwa wamedhalilika kwa kupuuza maoni ya wananchi na hatimaye wameshindwa na walikuwa na nia ya kuwasaliti kwa kile wananchi wanachotaka(serikali 3)
 
CCM wanatfasiri sna vitu literally..HIli jambo la serikali 3 ktk vichwa vyao wanadhani litakuwa gumu zaidi kwa vile wanadhani serikali 2 zinatkuwa kazi kubwa sana,km ilivyo serikali 2 imewachukua mika 50, bila kitu hadi mabadiliko ya kiuchumi duniani na rasilimali na watu binafsi kuanza jenga nchi ndipo wanadandia sifa. Akili za Nape na wenzie ni kwamba serikali 3 watakufa kwa vile mbili tuu wameshatamani kubwaga anyanga.Kweli akili ndogo ni shida sana.Sijui wandhani serikali 3 inaongeza raia mara 3?
 
Tanganyika lazima ifufuliwe ili tuheshimiane, vinginevyo CCM ikitumia wingi wao kulazimisha serikali mbili, wakati sisi wananchi tunataka Tanganyika yetu. Hiyo ni dharau iliyovuka mpaka, maana katiba inayoandikwa sio ya chama wala kundi fulani bali yetu sisi. Watanganyika itabidi tujiandae kuitafuta Tanganyika kwa gharama yoyote ile, hata kama ikibidi kwenda msituni kuitafuta Tanganyika tutaenda.

Haiwezekani wengine wawe na serikali yao halafu sisi tuwalipie mishahara yao, tuwalipie bili za umeme, tuwasomeshee watoto wao, walale kwetu, wamiliki ardhi huku kwetu. Kisha watutukane, halafu sisi tuendelee kusema asante tu!!!
Tanganyika ni muhimu irudi katika enzi yake
 
CCM inatambua kwamba katiba ni ya wananchi ndiyo maana hujawahi kusikia CCM ikitishia kujitoa kwenye huu mchakato wa kuandaa katiba mpya.

Wewe inaelekea ni gamba tena la mamba, NAPE NNAUYE anataka kuwaburuza watu zaidi ya 6,000 kutoa maoni kwenye Tume ya kuratibu rasmu ya katiba mpya kwa manufaa ya nani? nani haelewi anachokifanya, acha kuwa limbukeni wewe
 
hakuna muungano wa kitu kimoja wala huitaji kwenda shule,Tanganyika + Zanzibar =Tanzania,wakitaka 2,hakuna muungano,huo ndio ukweli.
 
ccm ukitaka kujua ni vichaa au wachawi ni pale wanapopinga muungano wa serikali moja
 
Kingine kinachoipa CCM jeuri ni mali ilizonazo.

Ningependekeza kuwa mali zote zinazomilikiwa na CCM zilizochangiwa na wananchi wakati wa chama kimoja zichukuliwe na kugawanywa sawasawa kwa vyama vyote vya siasa ikiwemo CCM yenyewe.
 
mimi nimecheka hiyo picha jinsi udongo wa tg na zenj ulivyo mixiwa kisha kumwagwa baharini! Sio ushirikina huo? Isije ikawa kuna mwiko!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…