Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata Cuf sera yao ni serikali 3.
Nimeona CCM wametumia nguvu na pesa nyingi kulazimisha kuwa ktk bunge la katiba wabadilishe rasmu ya katiba mpya, kwenye issue ya aina muungano kutoka serikali tatu kana ilivyowekwa na tume na kuwa muungano wa serikali mbili. Wameitisha vikao, semina na washa nyingi kushawishi hili. Lakini kwa kuwa wengi wa wajumbe kwa sasa wamo ccm nusu nusu, na kwa kuwa serikali tatu ni wazo la cdm (wananchi) ambako hawa ndiko wanasubiria kutimukia kuachana na ccm (mafisadi), watapigia kura serikali tatu. Na huu utakuwa ushindi mara 1000 kuliko kushinda jimbo la Karenga kama mmoja anavyo shadadia eti cdm wakishindwa kulichukua wajizuru. CDM wapo zaidi bungeni kwa sasa kuliko kwingine kote. Tanganyika itazaliwa, ccm itakufa chama kama TANU yaani CDM kitatamalaki.
Kayamgo, Mwiba,Matola wote mabandiko yenu yanakidhalilisha kiswahili.
Wewe kiswahili unakijulia wapi? by the way umepotea njia hili ni jukwaa la siasa na siyo jukwaa la lugha.Kayamgo, Mwiba,Matola wote mabandiko yenu yanakidhalilisha kiswahili.
Siyo kubadilisha bali ni mjadala ndiyo maana inaitwa rasimu bado haijawa katiba kamili,hivyo kuitwa dodoma siyo kwenda kuwa rubber stamp ya tume ya warioba bali kujadili kili walichotunga kupitia watu 500,000 tu tena ni hoja kwa hoja na penye marekebisha wana haki ya kufanya hivyo,tuwe waelewa
CCM inatambua kwamba katiba ni ya wananchi ndiyo maana hujawahi kusikia CCM ikitishia kujitoa kwenye huu mchakato wa kuandaa katiba mpya.
mimi nimecheka hiyo picha jinsi udongo wa tg na zenj ulivyo mixiwa kisha kumwagwa baharini! Sio ushirikina huo? Isije ikawa kuna mwiko!Kabla hata ya kuanza kwa zoezi la kukusanya mawazo ya wananchi kupitia tume ya Warioba, tayari wananchi tulikuwa tumeisha fungwa midomo kwa kuwekewa mipaka katika swala muhimu la muungano ambalo kimsingi ni tatizo SUGU tokea kuanziswa kwake April 1964 mpaka mwaka 2013 ambapo viraka zaidi ya 10 vimeishawekwa bila mafanikio huku mafarakano yakizidi kila kukicha katika hii ndoa tegemezi. Hiki kipengele katika Hadidu za Rejea hakikupaswa kuwepo pale kiliposema, Mwarobaini wa matatizo ya msingi siyo muungano wenye serikali moja, mbili au tatu bali ni sauti kwanza ya wananchi kupitia REFERENDUM kuamua wanataka kuendelea na hii ndoa TEGEMEZI au kuachana nayo. Kama ikitokea wananchi wengi wataamua kuendelea kuwepo na muungano basi wapewe tena nafasi ya kuamua ni muungano gani wanataka kuendelea nao. Kinachotakiwa kwa sasa TUPIGANIE REFERENDUM kujua mwerekeo wetu kwa kizazi chetu kijacho. One Look Is Worth A Thousand Words kama picha hapa chini zinavyoonyesha.