Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Waziri wa Nape Nnauye amesema kwamba hakuna Mtanzania yeyote aliyekamatwa ama anyeshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa sababu tu ya kukosoa mkataba wa uwekezaji wa bandari kati ya serikali ya Tanzania na Dubai kama ambavyo imekuwa ikitajwa na mashirika ya Kitaifa na Kimataifa.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti 16, 2023, kufuatia kukamatwa kwa Balozi Dkt Willbrod Slaa, Mdude Nyagali pamoja na Wakili Boniface Mwabukusi, ambapo Waziri Nape amesema watu hao wamekamatwa kutokana na kauli zao zinazoashiria vitendo vya uvunjifu wa amani pamoja na kupanga maandamano ya kuiondoa serikali madarakani.