Nape Nnauye kama January Makamba, maji ya shingo yamfika. Amuangukia Rais Magufuli baada ya kumnanga

Mwaka huu hautaisha ataulamba tena uwaziri, kuna mtu amechuja sana kwenye wizara moja hivi ,wale wapumbavu wa katibu wa CCM wote wanaenda kuomba msamaha,MAGUFULI KURA ZAKE 25% ZIPO MTWARA NA LINDI ,AMEONA WAOMBANE MSAMAHA YAISHE AENDELEE KUKUBARIKA ,NAPE NAE 2020 KAONA ASIISHIE TU UBUNGE WA MSIMU MMOJA ....
 

Kwa Africa mtawala ni mungu MTU nchi zilizoendelea kiongozi ni mtumishi wa watu
 
x,
Mwenye final say Kwenye Chama chetu ni chairperson .
 
Kwani si aombe kimya kimya kwani ni lazima ipewe coverage kuubwa.
 
Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amemuomba msamaha Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam kwa kile alichoeleza kuwa siku za hivi karibuni yametokea mambo mengi.

Waziri huyu wa zamani wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amefunga safari hadi Ikulu Dar es Salaam kuonana na Rais Magufuli ambapo leo ndipo wamekutana na kuzungumza.

"Nimekuja kumuona kwa sababu mnajua mambo yaliyopita, hapa katikati kumetokea mambo mengi. Mimi kama mtoto wa CCM nimeona ni vizuri nije niongee na Baba yangu na nina shukuru amenisamehe na amenipa ushauri," amesema.

Kwa upande wake Rais Magufuli amesema, "Na mimi nimeshamsamehe kwa dhati, Nape amekuwa akiandika hata meseji nyingi hata usiku wa manane akiomba msamaha, unamuona kabisa huyu mtu anaomba msamaha".

 
Wakudadavua huyu alisema mshamba kasamehewa, lakini yule aliyesema dictator uchwara, alininginizwa na kutupwa nje kabisa . Duniani kuna mambo
 
Mbona ameshukia mbali na makaz ya Rais akaanza kutembea kwa miguu? Uku tunaonaga wageni wengine wanashushwa mbaka karibia na ngazi za kuingia ndani ikulu.
Pengine ndio adhabu yenyewe hiyo
 
Kupambana na utawala si kitu mchezo.

Walikuwa wanafikiri sisi tunaonyanyaswa na chama tawala tunaraha!

Lazima ujitoe muanga kutetea wananchi hasa utawala huu.

Kwa hiyo korosho sasa zinakosa watetezi, bado Mwantumu.

Kutetea watu ambao hawajitambui siyo kitu mchezo.

POLENI SANA KWA KUJARIBU KAZI ZETU,
 
Juzi nilicomment kwenye Uzi flani nikawaambia Rais ana mamlaka makubwa na hilo liko wazi, wengi mliwananga akina ngeleja kuomba msamaha Leo nape kwenda wazi wazi, nawambia tena Rais ana mamlaka makubwa kumtukana na kumsengenya ni kosa kubwa sn
Sio mamlaka makubwa, bali anatumia vibaya mamlaka. Hamna asiye pingwa dunia hii, ila unapowakomoa kwa kuwaua kisiasa/ kimwili unayetofautiana naye kimtazamo ni kosa.
 
Zamani nilwahi kuskia ya kutoka kwa askari Polisi ya kuwa ukitaka kummaliza nguvu mtu tajiri ni kumpiga pingu mbele ya hadhara.Polisi huyu alinihakikishia ya kuwa mtu huyo hata awe tajiri vipi nguvu zinamuishia.
Nikaja kusikia kwamba njia mojawapo ya kuvunja mtu kisaikolojia ni kumvua nguo zote abaki uchi wa mnyama.
Miaka ya karibuni tukasikia tena ya kuwa ukirekodiwa ukifanya jambo baya unakuwa mateka wa aliyeku rekodi.
Juzi juzi nikasikia kuwa njia mojawapo ya kumfanya mtu akose amani ni kumuonyesha kuwa unamfuatilia kwa kila jambo.
Kwa udukuzi uliofanyika na kuvujisha sauti ni lazima wote waishiwe nguvu na hakuna atakayeweza kusimama tena,wamekuwa mateka wataimba na kucheza kama itakavyoamriwa.
Hii ndiyo na hizo ndio siasa.
 
Nimetazama sana kwa jicho la tatu nimegundua yafuatayo
1. Nape amesoma siasa na ameelewa nyakati hizi ni pambio gani linafaa kuimbwa . Nape halisi tutanwona 2025 panapo majaliwa

2.Nape ameelewa kitakachofuata kwake ikiwa hatajishusha ni kufutwa katika historia ya siasa kwasababu utawala wa sasa hautaki mchezo mchezo maana yake amesoma nyakati

3.tumtazamie Nape akiwa mpole sana Bungeni na yawezekana akarudi kwenye baraza la mawaziri maana ametambua alichokuwa anakitenda na anaye mtendea sio wa kawaida na hataki utani.

4. Ni vema Nape abadilike kabisa isiwe season break tu



Je wewe umeona nini
 
Maneno yako mazito japo umegusia aina moja ya "utekaji"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…