johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Kama hajamkosea ni nini kilichompeleka Ikulu wakati wenzie wako bungeni!alimkosea nini Magu?
Siyo siri,upinzani inabidi kujipanga sana kuiondoa Ccm madarakani. Hawa jamaa wako very well organized. Wanajua kumaliza tofauti zao wenyewe kwa wenyewe. Ingekuwa ni upinzani hapa watu wameshafukuzana siku nyingi kwenye Chama. Kitu kingine nilichojifunza kwenye hili sakata,wazee ni watu muhimu sana ndani ya chama. Busara zote hizi nina uhakika ni za wazee ndani ya Ccm.Mbunge wa Mtama Nape Nnauye amefika Ikulu jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kuomba msamaha. Ameomba msamaha na kusamehewa kosa aliliofanya miezi michache iliyopita.
Akizungumza akiwa nje ya Ikulu baada ya kuzungumza na Rais Magufuli, Nape Nnauye amesema "Kwanza nimekuja kumuona baba yangu lakini Mwenyekiti wa Chama changu, Rais wangu kwasababu wote mnajua mambo yaliyopita au kutokea hapo katikati na mimi kama mtoto wa CCM, kama mwanae, nimeona ni vizuri nije niongee na Baba yangu.
Nashukuru kwamba amenipa fursa ya kuja kumuona na ameniambia amenisamehe na amenipa ushauri na kwakweli kwa dhati ya moyo wangu nishukuru sana amenipa fursa kubwa sana."
Mbunge Nape anaendelea kusema "Kwa kweli Muheshimiwa Rais kama Baba yangu, kama mzazi wangu nashukuru sana kwa fursa uliyonipa kwa kunisikiliza, kwa kunisamehe, kunishauri, kunielekeza nifanye nini huko mbele ninapokenda."
Rais Magufuli amesma "Mimi nimeshamsamehe kwa dhati Nape, amekuwa akiandika 'message' nyingi sana za kuomba msamaha hata saa nane za usiku nimemuona huyu mtu akiomba msamaha'"
"Leo ameniomba hapa aje anione na kabla, amejaribu sana, ameenda kwa Mzee Mangula amefika hadi kwa Mzee Opson na Mama Nyerere, amehangaika kweli. Na kwamba sisi tumeumbwa kusamehe, na wewe umemuona asubuhi amekuja hapa nikasema siwezi kumzuia kumuona ngoja nimuone kwanza japo nilikuwa na kikao kingine na kikubwa" ameongeza Rais Magufuli
"Anachozungumza ni kwamba naomba Baba unisamehe, najua kusamehe kunaumiza lakini nasema kwa dhati kabisa nimemsamehe kabisa na anaeleza yaliyokuwa yanamsibu na baadhi ya watu waliokuwa wanamrubuni. Wengine wapo kwenye chama lakini nasema yote tumesamehe kwa sababu bado ni kijana mdogo na ana 'future' nzuri kwenye maisha yake."
"Nikiendelea kumshikilia kwenye moyo wangu, kwanza ni dhambi kubwa kwa mwenyezi Mungu na imeandikwa tusamehe saba mara sabini na Mungu amtangulie katika shughuli zake, akalee mke wake na familia yake, akakitumikie chama na akawatumikie wananchi wa jimbo lake." Amemalizia Rais Magufuli
Wakimalizia katika maongezi yao nje ya Ikulu, Rais Magufuli alimuuliza Nape "Kwa hiyo ulikuwa huna amani?"
Nape: Sana
Rais Magufuli: Uwe na amani na Mungu akusaidie
Pia soma;
Imevuja sauti inayodaiwa ni Maongezi ya Simu ya Nape Nnauye na Abdulrahman Kinana kuhusu njama za kuichafua CCM
Ni kuhusu barua iliyotolewa na Makamba na Kinana kuhusu kuchafuliwa na Musiba. Ni Maelekezo ya Kinana Kumtaka Nape aisambaza barua kwenye vyombo vya habari. Kinana: Mwambie bwana hawa jamaa wanatoa statement leo, Unafikiri tumpe nakala? [Nape: Hapana] Mwambie wanaiandaa Mzee wataitoa leo...www.jamiiforums.com
Karibuni sana nyumbani kumenoga!Wapinzani mjiandae kisaikorojia na kule kusini korosho lishapatiwa uvumbuzi mh alikubari kukurupuka sasa katuachia vijana tupige pesa na wakulima wetu oya fursa hiyo ya korosho kusini sasa ndio habari ya mujini mh. Raisi hongera kwa ili la korosho nakupa tano safi sana Acha bro Nape arudi na tutarudi wengi
Njaa ya umalaya wa kisiasaKama hajamkosea ni nini kilichompeleka Ikulu wakati wenzie wako bungeni!
Mbona makamanda mmekasirishwa sana na kitendo cha Nape kuomba msamaha?!!Njaa ya umalaya wa kisiasa
Magufuli kujiongezea muda baada ya 2025 ni stori za vijiweni kaka. Hazina ukweli wowote,watu tulio wengi hatuifahamu Ccm vizuri. Mfano mzuri ni hili sakata la akina Nape,Kinana na wenzake,wengi wetu hatukujua lingefikia kuombana misamaha.Kashashinda mbona na kuna mkakati wa kumuongeza miaka mingine 10 baada ya 2025[emoji23][emoji23]
Nime angalia picha nimeona bado huyo mwisho anaye angalia
Mkuu utachoma mafuta kwenda kuomba msamaha kwa mtu bila kumtendea kosa?makosa gani alimfanyia Magu?
Nimeona Nape anatembea umbali mrefu sana ndani ya maeneo ya Ikulu.
Alishushiwa nje ya geti kuu la kuingia ikulu ?
Niliona mpaka anajifuta jasho kwa kutembea umbali mrefu.
Nimeona kama ametembea umbali mrefu sana.
Haaminiki ?View attachment 1203928
Kwenye siasa hakuna adui wala rafiki wa kudumuHii inaonesha Tanzania tuna watu wa wanamna gani! Jinsi gani watu walivyo vigeugeu wasiyo jua wanacho simamamia na hao ndiyo viongozi wetu, dah! Nawaonea huruma sana mnao panga foleni kwenda kuwachagua hao wanao itwa viongozi.
Lisu hatamsahau maishani ujue!Ndugai naye ni mtu wa kumuweka kwenye watu mentally capable of integrating things?
Kitendo cha mbunge wa jimbo la Mtama mh Nape Nnauye leo kwenda kuungama dhambi zake zote kwa Rais Magufuli kumeacha dilema na maswali yasiyojibika vichwani mwa wafuatiliaji wa siasa za chama tawala na za upinzani nchini.
Je, maungamo na kukiri toka moyoni alikokufanya leo Nape ni majuto kweli ya makosa na fedheha alizomfanyia Rais Magufuli au ni kujikosha tu baada ya kubaini wenzake kina Makamba na Ngeleja walienda kuomba msamaha na wakasamehewa?
Je, kambi ya upinzani iliyokuwa ikiwatetea Nape na wenzake, hivi sasa inasemaje baada ya kuona baba na mwana wamepatana?
Tujadili kwa pamoja.
View attachment 1203829