Pre GE2025 Nape Nnauye: Kauli ya "Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza" ilikuwa ni ya utani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ile kauli Kama mwanaccm imeniumiza Sana! Ina maana kazi zote wanazofanya CCM zinategeea wizi wa kura! Hivi nape Ana ubia na uwaziri?
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema video inayosambaa ikimuonyesha akisema kuna mbinu nyingi za CCM kushinda uchaguzi ikiwamo zisizo halali imepotoshwa na hakuwa na maana ili
Hii nchi hii tatizo ni hao wanaoaminiwa na Rais ndiyo hao wanamwangusha. Ndani ya CCM kuna watu wasafi kabisa mfano Bashungwa, Aweso, Mchengerwa na akina Biteko. Mbona hawatelezi katika maongezi yao?? Lakini hawa akina Nape, Mwigulu, Makamba mbona kuteleza kwingi sana?? Au tusema akiwazacho mtu ndiyo kimtokacho kinywani🤔🤔🤔🤔🤔🤔. Binafsi nasema hawa vijana bado sana kiuongozi ni mfumo na pesa ndiyo zinawabeba ila ni weupe kama karatasi vichwani mwao kiuongozi.
 
Harafu Bado et nape na Jery slaa wanabaki kuwa viongozi wakuu wa taifa letu
Sasa mkuu taifa lenyewe halijajengwa kwenye misingi ya kuwajibika unategemea nini? Yaani tutaendelea kupiga hatua mbili na kurudi nyuma hatua tano zaidi miaka kwa miaka kadri mabadiriko ya kiutawala yanavyochelewa. Angalia mpaka viongozi majirani wanatuonea huruma tunavyouza maliasili zetu kwa jina la uwekezaji.
 
Nimeenda kutizama Ile video na majibu yake haya nimekuta Nina jicheka mwenyewe
 
Nionavyo mm Kwa kweli nape amempotezea mama kura za mwaka 2025,ningeshauri mh Rais,achukue hatua mapema,sio jambo jema na halina afya Kwa mustakabali wa Taifa letu, Kwa nchi inayofuata misingi ya demokrasia
 
Ukiona viongozi wanaanza kuzitamka dhambi zao hadharani basi mwisho umekaribia yaani huu ni ulevi wa dharau ulopitiliza
 
Mwambie aache ujinga, lakini ajue Watanzania wakichinjana atakuwa amesababisha yeye.
 
Na kuita waangalizi wa kimataifa, wanafanya hivyo ili kupata uhalali kimataifa wala Siyo kwa ajili ya wananchi kupata viongozi bora
Na wala hajatania hata kidogo, cha ajabu wanatumia mabilioni kwenye kampeni na wanajua watajitangaza tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…