econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Rais yupi? Huyu anayedai kilimo apewe msomali?. Huyo Hana jipya.Mpaka asubuhi bado atakuwa waziri basi nitaamini hakuna Rais
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Rais yupi? Huyu anayedai kilimo apewe msomali?. Huyo Hana jipya.Mpaka asubuhi bado atakuwa waziri basi nitaamini hakuna Rais
PoleAcha mtu aongee kama Jambo halikuhusu kaa kimya.
nijaposema kwa lugha za malaika.....Tuna kazi kubwa Kama taifa, aliyoyasema ndiyo yanayofanyika anaongea kupitia uzoefu!!
Hii nchi hii tatizo ni hao wanaoaminiwa na Rais ndiyo hao wanamwangusha. Ndani ya CCM kuna watu wasafi kabisa mfano Bashungwa, Aweso, Mchengerwa na akina Biteko. Mbona hawatelezi katika maongezi yao?? Lakini hawa akina Nape, Mwigulu, Makamba mbona kuteleza kwingi sana?? Au tusema akiwazacho mtu ndiyo kimtokacho kinywani🤔🤔🤔🤔🤔🤔. Binafsi nasema hawa vijana bado sana kiuongozi ni mfumo na pesa ndiyo zinawabeba ila ni weupe kama karatasi vichwani mwao kiuongozi.Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema video inayosambaa ikimuonyesha akisema kuna mbinu nyingi za CCM kushinda uchaguzi ikiwamo zisizo halali imepotoshwa na hakuwa na maana ili
Sasa mkuu taifa lenyewe halijajengwa kwenye misingi ya kuwajibika unategemea nini? Yaani tutaendelea kupiga hatua mbili na kurudi nyuma hatua tano zaidi miaka kwa miaka kadri mabadiriko ya kiutawala yanavyochelewa. Angalia mpaka viongozi majirani wanatuonea huruma tunavyouza maliasili zetu kwa jina la uwekezaji.Harafu Bado et nape na Jery slaa wanabaki kuwa viongozi wakuu wa taifa letu
Mpaka Sasa hivi angekuwa amejiuzulu mwenyewe.Eti nyie mliotembea naomba mtuambie , hivi kauli kama hii kwenye nchi za wenye akili timamu sio kosa la jinai?
Umeona eh! Eti msomali apewe kilimo wakati nchi yao ina njaa kila mwaka.Rais yupi? Huyu anayedai kilimo apewe msomali?. Huyo Hana jipya.
Rais gani amfukuze Nape?Huyu Jamaa amekosea sana ila maneno ya hivi yanaweza sababisha kufukuzwa hata Uwaziri.
Yanaondoa uaminifu wa Umma kwenye mchakato wa Uchaguzi,ikifaa Rais amfukuze kazi.
Mwambie aache ujinga, lakini ajue Watanzania wakichinjana atakuwa amesababisha yeye.Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema video inayosambaa ikimuonyesha akisema kuna mbinu nyingi za CCM kushinda uchaguzi ikiwamo zisizo halali imepotoshwa na hakuwa na maana iliyotafsiriwa na watu wengi.
“Nimeona mjadala wa video hii. inapotoshwa kwa kukata vipande watakavyo wapotoshaji. Msingi wa mjadala huu ulikuwa utani wa hoja ya zamani ya “goli la mkono”.. uliorushwa wakati naongea ndio maana kuna kicheko kabla. Haikuwa serious version. Mimi muumini wa uchaguzi huru na haki. Vizuri tuendelee kushindana kwa hoja,”ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa X leo Jumanne Julai 16, 2024.
View attachment 3044076
Pia soma: Kuelekea 2025 - Nape: Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza, ili mradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe!
Nape ameibuka kuelezea hoja hiyo ikiwa ni saa chache tangu Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla leo, aseme kauli hiyo haitokani na msimamo wa chama hicho.
“Kuna kiongozi nimemsikia huko mitandaoni anasema eti ushindi wa uchaguzi hautokani na kura za kwenye boksi, mimi nataka nimwambia hiyo kauli isitazamwe kuwa inatokana na CCM,” amesema.
Pia soma: CCM wapinga kauli ya Nape Nnauye kuhusu imani yake kwenye ushindi wa chaguzi nchini, wasema CCM haihitaji mbeleko
Nape alitoa kauli hiyo jana Julai 15, 2024 usiku alipotembelea soko la Kashai mkoani Kagera na kuzungumza na wananchi na kauli hiyo ililenga kumhakikishia ushindi wa Mbunge wa Bukoba Mjini, Stephen Byabato katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Na wala hajatania hata kidogo, cha ajabu wanatumia mabilioni kwenye kampeni na wanajua watajitangaza tu.