Pre GE2025 Nape Nnauye: Kauli ya "Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza" ilikuwa ni ya utani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hii nchi yafaa sasa tuanze kuwa serious. Kila mtu ni utani utani tu. Ukiingia mitandaoni mtu akiguswa kidogo anajibu sio kila kitu ni cha kuchukulia serious, no one can judge me, kila mtu afuatilie maisha yake (sasa ukiweka kitu mtandaoni si umeturuhusu tukione?) nk.

Wanasiasa na viongozi nao hivyo hivyo (ingawa huu aliosema Nape ni ukweli). Angalia bunge lilivyo na upuuzi, utani wa Simba na Yanga wakati kuna mambo ya muhimu ya kujadili na kufanya.
 
Kauli hii ni kauli ya kweli, hiki ndicho kitu kinachotokea kwenye chaguzi zetu!. Nape ni mkweli daima.
P
 
Anafanya utani kwenye uongozi?

Kakubali kwamba anafanya utani kwenye suala linaloweza kuhatarisha usalama wa taifa?

Jambo hili linaweza kusababisha machafuko ya kisiasa na uvunjwaji wa amani, anafanya utani?
 
kule kanisani kwetu, kuna siku mchungaji alifundisha kuwa kuna njia nyingi za kupata taarifa. na kwamba hata iweje siku Mungu akiamua kukupa ufunuo wa yale tusiyoyajua; hata mawe yaweza kuongea ukweli.
 
Kauli hii ni kauli ya kweli, hiki ndicho kitu kinachotokea kwenye chaguzi zetu!. Nape ni mkweli daima.
P
Mbona unaposhina naye!
=> Yeye Nape amesema alikuwa Anatania (inamaana si ukweli)
=> Wewe unasema Nape ni msema ukweli daima.
Tumuamini nani ?


Nakumbuka kauli ya Benjamin Mkapa, kwamba "wanao amini Kiongozi anapatikana Kwa kupigiwa kura ni Malofa"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…