Nape Nnauye: Nahisi Mashabiki wa Kiba ndio waliokuwa wakipinga Diamond kupewa Bendera ya Tanzania

Huyu jamaa atumbuliwe tu hakuna namna. Nchi ina shida kibao yeye yupo busy kujibu upuuzi. Atwambie ameweka mikakati gani kuhakikisha tunashiriki kwa wingi next time kwenye Olympics? Aaache uswahili sijui timu kiba
 
Huo ndio ukweli hata kama ni mchungu,sasa kama keshagudua kuwa wanaomshambulia yeye kwa kumpa bendera DIAMOND kina timu kiba kwanini asiseme ........ Kwani serikali inakatazwa kusema kwamba wanaoponda kitu fulani ni kikundi fulani ........ Mbona serikali ilisema kuwa waliovunja viti vya uwanja wa taifa ni simba,mbona hakuna aliyesema serikali kwa sasa na wenyewe ni Yanga ........Na hata humu wanaomshambulia waziri kwa kauli yake ni timu kiba tunawajua,kisha mnakataa sio ndio mnaopinga bendera kupewa DIAMOND.Mbona Serikali huwa inasema kuwa waliofanya tukio fulani ni WAISLAMU,mbona hakuna anayesemaga kama serikali imekuwa ya kikristo .........Ila kwenye hili serikali imewakabili moja kwa moja watu fulani ndio wahusika wa hili tukio,imekuwa kosa......??
 
'Hana tatizo na hao wasanii?'
hilo nalo ni tatizo wazir kuongozwa na mihemuko ya kishabiki
Kama ameshagundua kwanini asiseme,kwani ni kosa kusema kwamba kundi fulani ndio wahusika wa tatizo hili ...........??
 
Huyu namuona yuko nje ya baraza la mawaziri kabisaaa aanze kufanya clearance mapema.........Nimeota
Bora uendelee kuota tu,maana usingekuwa usingizini usingeongea kwa kufuata mkumbo,ila ungeleta kipengere cha sheria/katiba kinachomkataza waziri ASITAJE KIKUNDI CHA WATU KINACHOPINGA JAMBO FULANI.
 
'Hana tatizo na hao wasanii?'
hilo nalo ni tatizo wazir kuongozwa na mihemuko ya kishabiki
Mihemko gani hapo iliyomuongoza waziri,au hiyo kutaja kuwa timu kiba ndio wanaopinga yeye kumpa bendera DIAMOND ???
 
Punguza povu maana vitu vingine haviongezei taifa chochote zaidi ya kelele tu
 
yaani hii ni kauli ya waziri yaani kauli ya serikali
Yes,hiyo ni kauli ya waziri,maana yake ni kauli ya serikali,kuwa IMEGUNDUA TIMU KIBA NDIO WANAOPINGA KWA YEYE KUMKABIDHI BENDERA DIAMOND, NADHANI HAKUNA SWALI ???
 
Ni kauli ya Waziri hiyo na ukizidi kuhoji utajibiwa kwamba hapa "nimesema kama mwananchi tu na sio Waziri maana na mie nina haki binafsi ya kutoa maoni yangu"
Kwani kwa mfano hapo utahoji kipi kimfanye yeye kuukana uwaziri wake ......... Kwamba ni kosa KUSEMA KUWA TIMU KIBA NDIO WALIOPINGA DIAMOND KUKABIDHIWA BENDERA YA TAIFA ??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…