Pre GE2025 Nape Nnauye: Nawapa pole na naomba radhi kwa kauli yangu ya ushindi nje ya boksi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Na 2015 bao la mkono ilikuwa utani si eti! Hapana Mungu kafanya yake kutujulisha tabia zenu. Watakusamehe wengine. Ingekuwa umetamka mara moja labda ningefikiria msamaha. Halafu kamuombe Mwenyekiti wako unayemharibia safari yake.
 
MTu level ya WAZIRI anaetoa kauli za namna hiyo zaidi ya mara 1 maana yake anajua anachokiongea.

Kuomba msamaha ni order aliyopewa na wakubwa wake wa kazi.

Lakini haiondoi ukweli wa alichokitamka.

Ni vile tu hamna chama chenye wagombea wanaojitambua ndo mana watu wanaona acha hao CCM waendele tu kuwepo kwa namna wanavyojua.

Ila kungekua na mbadala wa CCM hii nchi, kingeshanuka ila ndio Hamna sasa.
 
Najaribu kuiweka kauli hiyo kiutani lakini inagoma kabisa
Kimtokacho mtu ndio kimeujaza moyo wake
 
Namwombea radhi alikuwa amelewa!🍻🍻🍽️🍽️🥂✔️✔️✔️
 
Hii serikali ya Samia inatudharau sana watanganyika, sishangai kitu hapo hata kama angeamua kukaa kimya pia najua bosi wake angempongeza tu.

Nape anajidai ana masikio ya kusikia wakati bosi wake kiziwi hana masikio.
 
Amekichafua chama aitwe kamati kuu ajieleze!
 
NN halisi ni yule aliyetamka yale maneno, huyu aliyeomba radhi sio yeye.

Bora angenyamaza tingebaki tunabashiri huenda Kuna namna imefanywa watu wamechezea mitambo. Hii anathibitisha kwamba ni kweli alitamka Yale maneno kuhusu wizi wa kura. Aibu sana

Tukikataa kupokea radhi yake atachukua hatua gani?
 
Hoves kabisa
 
Ni jambo jema
 
Anaingia kwenye rekodi ya People Who Mocked God ategemee wenzie walichokipata.Isingekuwa kufuru kama asingemhusisha Mungu!

Kwamba unatenda dhambi kwa makusudi halafu unaenda kuomba msamaha na unatoa hukumu kwamba "Mungu anasamehe!"

Ajifunze kwa aliyejenga meli ya Titanic.Huyu aliuzwa kuhusu usalama wa meli itakapoanza safari,jibu lake lilikuwa kwamba hata Mungu hawezi kuizamisha.Sote tunajua nini kilifuata!

Wako wengi,Bumunda ameongezeka!
 
Hii inasaidia nini? anawapa Pole Maiti za Tanzania
Siasa dunia nzima zishakuwa maigizo kama Trump alisema Grab them by the Pussy na kwamba anaweza akamshoot mtu hadharani na bado akapata Kura..., na alipata Kura na kuwa Rais; what does it tell you about the current politics ?

Politicians are out of touch and people just don't bother..., na wataendelea hivyo mpaka njaa zikiwazidi ndio hapo watu watapigana marungu
 
Uzuri ujumbe umefika! Iliyo tangulia imetangulia tu, sisi tunshukuru na tukaendelea kuusubiria wakati.
 
Alikusudia na alikuwa anajua kabisa anachoongea na kipo moyoni na alishafanya lile Goli la mkono

Ni mjinga tu atamuona ulimi umetereza
We umekusudia kusema kwa sababu unajua hakuna wa kukuburuza kutoka jukwani au kwenye gari
Nchi zingekuwa zinabadili mawaziri tungekupeleka Somalia kwa mda ukaongee hayo 😄
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…