Warioba na tume yake kiukweli inabidi itege sikio lake kwa umakini.
Kuna maoni mengi hayakuingizwa kwenye rasimu hii iliyoandaliwa.
Mchakato bado sana
huu udaku upo kwenye tz daima sio mwananchi.
Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na Uenezi (Nec-CCM), Nape Nnauye, ametuhumu Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwa haitendi haki kwa kuwazuia wajumbe wa Baraza la Katiba kusoma waraka wa chama hicho unaopinga baadhi ya mambo yaliyopo kwenye rasimu.
Nape alitoa shutuma hizo jana alipozungumza kwa njia ya simu, alibainisha kuwa viongozi wa Jukwaa la Katiba akiwamo Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba, wanataka mapendekezo yaliyopo kwenye rasimu yapite yalivyo.
Kwani kufanya hivyo wanazuia maoni ya wananchi, ingawa hatujawatuma kuusoma kwenye mapendekezo, lakini wana haki ya kuutumia wanavyojisikia, alisema Nape.
Alisema wanajua wapo watu wachache wanaoupinga waraka huo wa CCM, lakini hawaelewi kwa sababu unahusu wanachama wao.
Tume itende haki isikilize mawazo ya kila mtu, inachofanya sasa ni ubaguzi, wao wanatakiwa kusikiliza maoni siyo kutetea rasimu, alisema.
Hivi karibuni vyombo vya habari viliripoti jinsi Jaji Warioba alivyokosoa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba wanaokwenda na matamko au nyaraka za vyama, badala ya maoni ya wananchi waliowachagua.
MWANANCHI GAZETI
Kwenye RED Tume itende haki isikilize mawazo ya kila mtu, lkn mh. Nape waraka wa CCM sio mawazo ya wanachama wa CCM, mmewapa waraka na kwa sababu ni vilaza wameingia nayo madesa(waraka) kwenye mabaraza. Na m/kiti wa tume alishasema mapema waacheni wananchi watoe maoni yao na si maoni ya vyama vya siasa.Mwanaccm huyu, sijui anaitwa Mateo Qaresi, "alieleza kuwa Serikali tatu haziwezi kuepukika na kuwataka wanasiasa wakiwamo wa CCM kuacha ushabiki".hii ni kutoka gazeti la mwananchi la leo. Watch out my friend, sio kila kitu ni siasa.Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na Uenezi (Nec-CCM), Nape Nnauye, ametuhumu Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwa haitendi haki kwa kuwazuia wajumbe wa Baraza la Katiba kusoma waraka wa chama hicho unaopinga baadhi ya mambo yaliyopo kwenye rasimu.