Nape, Tido Mhando wawatembelea wafanyakazi wa Azam TV waliopata ajali

Nape, Tido Mhando wawatembelea wafanyakazi wa Azam TV waliopata ajali

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Waziri wa Habari, Nape Nnauye akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tindo Mhando, jana usiku walifika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam kuwajulia hali waandishi wa habari wanne wa Azam waliopata ajali ya gari Mlima wa Kitonga, Iringa wakiwa safarini kwenda Mbeya.

Awali, majeruhi hao walipokelewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuendelea na matibabu na wote hali zao zinaendelea vizuri.

Uwanjani hapo majeruhi hao walipokewa na viongozi waandamizi wa Azam Media Limited, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye na Mbunge wa Buchosa, Erick Shigongo.



FLifCp5WUAYhd-H.jpg


FLifCp7WQAMEVFT.jpg


FLifCp9WQAAJjsr.jpg
 
Mungu awasaidie warejee mapema katika hali zao.
 
Back
Top Bottom