Nape: Wanaotaka serikali Mbili ndio wana akili Timamu

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,885
Source Uhuru 05/08/2013

Kauli tata za Nape Mnauye kama nilivyomnukuu katika gazeti la Uhuru kwa kauli za kejeli na matusi kwa kusema kuwa wanapenda serikali mbili ndio wenye akili timamu, kwa maana nyingine jaji Warioba na wananchi waliopendekeza ni mamburura.

Aliyasema hayo katika ukumbi wa BOT katika semina ya vijana wa CCM na akadai CCM inajiandaa kimkakati kuhakikisha serikali tatu inaondolewa katika katiba mpya. Na akahoji kama CHADEMA watasusia hawana faida kwani hata bajeti hawakuwepo na ikapita na hata kwenye katiba wasipo kuwepo wataipitisha
 
Ngoja aje akanushe hapa na kudai kwamba wamemnukuu vibaya.!
 
ni uhuru wa mawazo wa kila mtu kusema anachoweza kukisema pasipo kudhuru uhuru wa mwingine.Ila siafiki kauli kama hizi ambazo zinalenga kupotosha.ina maana anachowaza yeye ni sawa ila mwenzie akiwaza tofauti ni tatizo.
 
Aiseeee!! Niko kwenye serikali mbili lakini nape kwa kejeli zake? Wacha tu....
 
Na gazeti la uhuru nimekunukuu vibaya siyo? Ulevi wa madaraka ni mbaya kuliko ulevi wowote ule...pole
 
Mwaka huu hawana pa kujificha lazima tuwakurupushe tu.....!!
 
laana ya kuwaita wazee wenye busara kuwa wanakaribia kufa bado inamtafuna
soon tutakutana nae kariakoo au posta mpya akipiga siasa bila hadhira.
asipowaomba msamaha yatamkuta makubwa zaidi
 
Hamna Muungano wa serikali mbili. Hapa swala ni kama ni muungano IBAKI SERIKALI MOJA kama ni shirikisho serikali ni TATU.Watuonyeshe Tanganyika inafia wapi na watupe sababu za kuiua na kwanini ?mbona isiwe Tanganyika na Tanzania ?why Tanzania na Zanzibar ?Nchi kubwa inakufa inabaki kisiwa ambao wakazi wake wanakaribia kufikia wakazi wa mbagala ?

Labda kama wanatafuta vyeo kwenye urasimu wa serikali 2 maana kuna kubebana sawa kama ni kwa ustawi wa muungano ni serikali moja tu ama liwe shirikisho la serikali 3.
 
Lazima atakanusha
 

Hii ni vita ya fahari wawili.
 
Washauri wa Nape wanamdanganya ili aharibu wamtimue
 
Nape Mnauye hili suala la rasimu angeliacha na namshuri NAPE ACHA MASUALA YA RASIMU waamue Watanzania wenyewe.
  • Kuwalazimisha CCM wapendekeze Serikali 2 ni uasi kwani hata kura zikizidi na Wazanzibar wote wakikataa ni AIBU kwani ni sawa na kulazimisha ndoa ya watu wawili ambapo Mke keshamkataa mume.
  • Wazanzibar hawataki Serikali 1, wala Serikali 2, hata Serikali 3 wanachotaka ni Taifa lao Zanzibar Unguja na Pemba.
  • Kumbuka wakati wa Vyama vingi CCM walisema 90% wanataka Chama kimoja lakini J.K. Nyerere 1992 akawaambia lazima mkubali mabadiliko.
  • Watanzania walikataa EAC isiwe Jumuiya ya Nchi 5 kwa kuiongeza hasa Rwanda bado CCM mkafunika kombe, leo tunaona ya Rwanda 9tumemuingiza Ngamia hemani kumtoa ni aibu tunatoka wenyewe sasa tunamuacha Kenya, Uganda na Rwanda. Sisi na Burundi itasaidia nini.
Waachieni wananchi wapige Kura, waamue wenyewe, kwani huko mbele mpango wenu ukishindwa njue hata wa kushika Dola na utashindwa 2015 lazima.
Rasimu imezungumzia kila kitu Serikali 3. Bunge, Jeshi, Mahakama, Usalama wa Taifa. sasa mnapotaka Serikali mbili ni bora mkaanzisha Rasimu ingine mpya ambayo Wananchi wataitupilia mbali hata kabla
 
Kwa hiyo hata Jaji Bomani aliyekiri kupendelea serikali tatu hana akili timamu?
 
Nachokiona sasa hivi Nape ameamua kuharibu tu ni takalo na liwe maana yeye mwenyewe hana magnitude wala direction.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Mhariri Mtendaji anaitwa Josia Mufungo, ila NAPE kwa hulka yake ameyasema na ndio maana yakapewa uzito kwenye gazeti la chama.
Mkumbuke na Mwenyekiti wa Wazazi Taifa BULEMBO amewaambia wananchi huko Mbeya kuwa Rasimu hii ikipitishwa huduma za Shule, Zahanati, Hospitali na Halmashauri zitafutwa rasmi.
Changanya wote hao utapata kuona jinsi CCM walivyojipanga kupotosha umma.
kama Serikali tatu ni gharama kubwa basi tuwe na Serikali moja tu, lakini hatusemi kuundwa WILAYA NA MIKOA PIA KUONGEZA BARAZA LA MAWAZIRI kuwa ni gharama kubwa pia.
 
Kwanza huo ni unafiki. Nape una wasiwasi gani na sovereignity ya Zanzibar? CCM wasidhani wana vision kuliko watanzania wengine. Kuna mzigo kwa walipa kodi kushinda wabunge wa viti maalum? CCM anzeni na hilo kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…