Nape: Watu wanastaafu wanakaa mpaka wanakuwa wanywa gongo kwasababu hamuwapi stahiki zao

Nape: Watu wanastaafu wanakaa mpaka wanakuwa wanywa gongo kwasababu hamuwapi stahiki zao

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, ameitaka Serikali, iunde tume ya kuchunguza madai ya walimu, waliopandishwa madaraja bila mishahara, waliofutiwa barua za kupandishwa madaraja.

"Serikali ya CCM, ni ya wakulima na wafanyakazi, twendeni tukatende haki, haki huinua taifa."

"Naiomba serikali, Chama cha wakulima na wafanyakazi twendeni tukatende haki kwenye suala la stahiki, leo kuna watu wanastaafu wanakaa kule mpaka wanakuwa wanyawa gongo kwasababu hamuwapi stahiki zao za kuondokea kwenye vituo vyao vya kazi"
 
Nape aache kubweka hovyo hovyo analaumu nini wakati yeye ni mmoja wa walioko kwenye mfumo kuanzia baba yake na yeye mwenyewe, mbona alipokuwa kilingeni hatukumsikia kubweka bweka au sababu kaona mwendazake hayupo ndio kapata nafasi ya kubweka bweka,ningemuona wa maana kama angeanza kubweka siku nyingi wakti mwendazake alipokuwa hai.
 
Cheo dhama bwana,kipindi kile hayo yote alikuwa ajui mzee kuzima bunge live.
 
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, ameitaka Serikali, iunde tume ya kuchunguza madai ya walimu, waliopandishwa madaraja bila mishahara, waliofutiwa barua za kupandishwa madaraja.

"Serikali ya CCM, ni ya wakulima na wafanyakazi, twendeni tukatende haki, haki huinua taifa."

"Naiomba serikali, Chama cha wakulima na wafanyakazi twendeni tukatende haki kwenye suala la stahiki, leo kuna watu wanastaafu wanakaa kule mpaka wanakuwa wanyawa gongo kwasababu hamuwapi stahiki zao za kuondokea kwenye vituo vyao vya kazi"
Du! Hilo suala lishakua sugu! Sidhani kama litatibika, sab tangu niwe na akili ya kujua hayo, nizaid ya miaka 10, hata hapa nlipo, jiran yangu amemaliza mwaka amestaafu, bt hajalipwa mpaka saiv navyo andika sms hii, saiv anauza mahindi.
 
Nape alikuwepo huko lakini hata siku moja hajawahi kuongelea mambo hayo zaidi ya kuhangaika sasa
 
Inafika hatua Kama ulimkopesha mstaafu, inakubidi usamehe TU ilo Deni

Mathalani,
Unamdai mstaafu laki 5, afu unamwona anakuja kukuazima elfu 2 ya unga watoto na wajukuu zake wakale.

Hiyo Nguvu ya kumdai laki 5 unaitoa wapi kwanza,

Zaid zaidi utamuongezea stress afe sikU SI zake, ujitaftie laana za bure.[emoji26]
 
Back
Top Bottom