Mdanganywa
JF-Expert Member
- Jun 15, 2009
- 620
- 342
Uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi ulianza mwaka 1995. Hivyo hadi leo tuna miaka 25 ya uzoefu uchaguzi.
Mwaka 1995 tulisema Mrema kaibiwa kura. Mwaka 2005 Freeman Mbowe aliyegomea urais alikuwepo hata wakati Kikwete anatangazwa kuwa mshindi. Mwaka 2010 tukasema Dr. Slaa kaibiwa kura. Mwaka 2015 tumesema Lowassa kaibiwa kura.
Kule Zanzibar kila uchaguzi tunasema Maalim Seif kaibiwa kura. Hivyo upinzani Zanzibar umeibiwa kura mara tano na upinzani bara umeibiwa kura mara tatu.
Hivyo, kwa miaka 25 mtu unaibiwa kura na mwizi yuleyule kwa mbinu zilezile.
Hii habari ya kuibiwa kura inachosha. Ukiona hoja za wapinzani ni kama vile wamejiandaa siku moja CCM ilegeze kamba iache wizi huo ndipo wapinzani wapate ushindi.
CCM haijageuka kuwa mabingwa wa kuiba kura duniani. Kura zinaibwa kila kona duniani. Wakati nchi zingine hawakuishia kulalamika hadi vyama tawala wakang’oka, wapinzani wa Tanzania wanaishia kulalamika.
Serikali za kikoloni zilifanya hikihiki inachofanya CCM kwa wapinzani. CCm na serikali inachokifanya huko Zanzibar ni kilekile na ambacho ASP ilikuwa inafanyiwa na serikali ya wakoloni. Kinachofanyika Bara ni yaleyale ambayo TANU ilikuwa inafanyiwa kwenye uchaguzi wa mwaka 1958.
Uonevu ule haukudumu kwa miaka kumi TANU ikashinda na ASP ikatawala. Nyinyi hapa uonevu umedumu miaka 25, kwa sababu ya kudhani mkilalamika basi malalamiko yenu yatasumbus usingizi wa CCM.
Hivyo, kazi kwenu mwaka huu. CCM hawataacha kuiba kura na hata mwaka huu wataiba nyingi tu. Lakini pia hatutaki tena kusikia kilio kilekile cha kuibiwa kura.
Tunasikia mtaandamana nchi nzima, kitu ambacho hakijawahi kutokea hapa lakini hutokea kwingine. Kama ni kweli basi andamaneni hadi haki yenu inapatikane. Siyo mnaandamana kisha zikifyatuliwa risasi mbili tu mnatawanyika na unakuwa mwisho wa kelele zote.
Wengi husema CCM wana mbinu nyingi za kuiba kura. Nimesema hawana mbinu yoyote mpya wanatumia zilezile walizotumia wakoloni kwa TANU na ASP.
Mwisho wa uonevu huletwa na wewe unayeonewa na si anayekuonea. Hivyo, mwaka huu nitawaelewa kama mkiibiwa kura halafu mkachukua hatua zitakazokomosha uonevu na wizi wa kura.
Lakini mkirejea malalamiko yenu ya miaka 25 wala hatutawasikiliza.