Napenda kuandika

Napenda kuandika

Swahilian

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2009
Posts
591
Reaction score
69

NAPENDA KUANDIKA

Kalamu ya risasi tosha, naandika na kufuta.
Matendo yalonikosha,pia yalonikokota.
Yote nayaoanisha, wazo kamili napata.
Kwa njia ya ushairi, mie hupenda andika.

Lugha yangu ni rahisi, yeyote ataisoma.
Natoa yalo halisi, uwongo waja nichoma.
Hamasa ni ufanisi, najifunza toka zama.
Ushairi ulo wazi, hujikita kwa jamii.

Nawe naomba usome, kesho ushike kalamu.
Zili mbivu uzichume,walishe wapate hamu.
Nikosowe nijitume. Niithamini kalamu.
Ushairi kwazo beti, nafundisha maadili.

Nyimbo za chekecheani, na hadithi za nyakati.
Pia zao tafrani, za masai na mang’ati.
Sekeseke za mitaani,na mbu funua neti.
Shairi lajazwa ladha, kwa lugha ilo mkato.

Naandika lugha ya watu, Kiswahili ndo yetu.
Nawazima roho kwatu,wanoabudu ya watu.
Haishiki kutu katu, haipambi ukurutu.
Shairi lilo hisia, hakika talirudia.

Wanoumwa subiria, zipo dawa nawagea.
Tamathali ndo tumia, siku zote kwa kwongea.
Hisia sije achia, mafumbo sije tegea.
Shairi liwe makini, lipambwe vina mizani.

Iwe dhiki au nema, sintopotosha asili.
Lilo baya liwe jema, mi si pungufu akili.
Sintochelea kusema, japo meshika makali.
Shairi ni kama tumbo, njaa yake iwe wimbo.

Tamati nina kiburi, lughaye ni Kiswahili.
Yatamba zote bandari,yauza bila dalali.
Wateja haisubiri, wafata wale asali.
Napenda tena andika, shairi la kusomeka.



 
asante mshairi ,mie hapa hata sijui pa kuanza kukandamiza
 
NAPENDA KUANDIKA
Kalamu ya risasi tosha, naandika na kufuta.
Matendo yalonikosha,pia yalonikokota.
Yote nayaoanisha, wazo kamili napata.
Kwa njia ya ushairi, mie hupenda andika.
.......................................................
Naandika lugha ya watu, Kiswahili ndo yetu.
Nawazima roho kwatu,wanoabudu ya watu.
Haishiki kutu katu, haipambi ukurutu.
Shairi lilo hisia, hakika talirudia.
............................
Tamati nina kiburi, lughaye ni Kiswahili.
Yatamba zote bandari,yauza bila dalali.
Wateja haisubiri, wafata wale asali.
Napenda tena andika, shairi la kusomeka.

POKEA TANO;

Pokea tano wakwetu, ni wengi umetukuna!
Ukisemapo kikwetu, kwa lafudhi yenye mana
Unatukuza cha kwetu, kwa ladha sikunung'una
Ni wengi umetukuna, wakwetu pokea tano!


Upokee hizo tano, mikono ije kutana
Tuletee nono nono, tungo zilizo mwanana
Tucheke tutoe meno, wakati twachekeana
Ni wengi umetukuna, nasema pokea tano!


Hizo tano upokee, mikono ikigongana
Na sote tuchekelee, uhondo wako kijana
kwa hamu tukodolee, beti zako kiaina
Ni wengi umetukuna, nacheka natoa tano!


Natoa tano nacheka, nasema umetukuna
Kwa ladha umeandika, shairi lenye maana
Kutujuza waandika, vyenye neema na mana
Ni wengi umetukuna, nagonga natoa tano!


Tano ni yangu tamati, nasema tutagongana
Namalizia ubeti, kwaheri ya kuonana
Siongezi hata futi, nawaagia vijana
Ni wengi umetukuna, wakwetu pokea tano!
 
r33ot.jpg
 
1.hizo tano zanikosha,mie mfungaji tosha.

tujilieni vya kwosha,vichafuchafu vyavisha.

zipandazo na kushusha, zifiazo twachajisha.

majigambo yote kwisha, walo kinyaa tapisha.

2.kiswahili ji latisha, ji kubwa kama maisha.

chakatika kijikasha, paparika vijitasha.

taabika chawawasha,kademika tetemesha.

waliweza wao jana, sie mpaka kiama.

3.wapi yu aja kuzima, mdundo huu wa ngoma.

hata umeme kizima, hapo ndo bado mapema.

hiki ndio chanda chema, siku zote mwakihema.

wangapi tu bado wima,tuombeane uzima.

4. tamati ya nne beti, sijatulia kwa kiti.

nawasha kwa kiberiti, nivute kisigareti.

takwenda na marikiti,pale nilapo chapati.

yaniuma njaa sasa, yafaa mie kwondoka.
 
Back
Top Bottom