Napenda kufahamu historia ya kabila la Wasubwa lilipo Tabora,Shinyanga na Mwanza

Kifaru86

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2017
Posts
1,734
Reaction score
3,822
Jamani napenda kuuliza kuhusu historia ya kabila la wasumbwa hili kabila lilianza anza vipi,walitokea wapi chimbuko lao hadi kutawanyika

Maana hili kabila lipo sana Urambo,Kaliuwa,Kahama,Geita pamoja na Chato .

Lakini pia ningependa kufahamu hivi wasubwa wanapatikana jamii ipi maana kuna watu wanasema wasubwa ni wahaa.

Kuna wengine wanasema wasumbwa ni jamiii ya waangaza, wengine wasukuma,wengine Wasubi n.k.

Kutokana na hayo naombeni mnisaidie kunipa historia ya kabila hili la wasubwaa japo halifahamiki ile kivileee.
 
Jamani napenda kuuliza kuhusu historia ya kabila la wasumbwa hili kabila lilianza anza vipi,walitokea wapi chimbuko lao hadi kutawanyika

Maana hili kabila lipo sana urambo,kaliuwa,kahama,geita pamoja na chato .

Lakini pia ningependa kufahamu hivi wasubwa wanapatikana jamii ipi maana kuna watu wanasema wasubwa ni wahaa.

Kuna wengine wanasema wasumbwa ni jamiii ya waangaza, wengine wasukuma,wengine wasubi n.k.

Kiongozi umepata mchumba huko nini
 
Mkuu mama yangu msumbwa wa Urambo, kiukweli Kabila hili ni gumu sana kutambua asili yake wengine wanasema asili Yake Rwanda, wengine wanasema wasumbwa ni wanyamwezi ni moja ya subtribes ya wanyamwezi kama wakimbu, wagalaganza, wanyanyembe, wasenye, wayumbu, wayubi, wayombo, warambo, du !! Ifahamike tu wanyamwezi sio kabila .....na wanyamwezi wanapatikana DR Congo Kisangani, na Wengine Huko Fortpotal Uganda
 
Back to Nguni speakers, Wasumbwa ni moja ya makundi ya wangoni yaliyoingia Tanzania.
Kumbuka wangoni waliingia Tanzania kwa makundi na kwa nyakati tofauti, moja ya makundi ya Hata ni WASUMBWA walioweka masikani yao mkoani Shinyanga hususani wilayani Kahama (zamani) na kwa sasa BUKOMBE mkoani Geita katika maeneo ya Ushirombo, Masumbwe na maeneo jirani
 
Karne ya 21 tunazungumzia makabila? By J.Nyerere
 
Back to Nguni speakers, Wasumbwa ni moja ya makundi ya wangoni yaliyoingia Tanzania.
Kumbuka wangoni waliingia Tanzania kwa makundi na kwa nyakati tofauti, moja ya makundi ya Hata ni WASUMBWA walioweka masikani yao mkoani Shinyanga hususani wilayani Kahama (zamani) na kwa sasa BUKOMBE mkoani Geita katika maeneo ya Ushirombo, Masumbwe na maeneo jirani
Mkuu unataka kuniambia wasumbwa ni jamiii ya wangoni.
 
Mkuu mama yangu msumbwa wa Urambo, kiukweli Kabila hili ni gumu sana kutambua asili yake wengine wanasema asili Yake Rwanda, wengine wanasema wasumbwa ni wanyamwezi ni moja ya subtribes ya wanyamwezi kama wakimbu, wagalaganza, wanyanyembe, wasenye, wayumbu, wayubi, wayombo, warambo, du !! Ifahamike tu wanyamwezi sio kabila .....na wanyamwezi wanapatikana DR Congo Kisangani, na Wengine Huko Fortpotal Uganda
Mkuu hata mimi hiyo story nimewahi kuisikia kuwa wasumbwa ni wanyarwanda japo sijafahamu kama walitokea sehemu ipi ya rwanda
 
Jamani napenda kuuliza kuhusu historia ya kabila la wasumbwa hili kabila lilianza anza vipi,walitokea wapi chimbuko lao hadi kutawanyika

Maana hili kabila lipo sana urambo,kaliuwa,kahama,geita pamoja na chato .

Lakini pia ningependa kufahamu hivi wasubwa wanapatikana jamii ipi maana kuna watu wanasema wasubwa ni wahaa.

Kuna wengine wanasema wasumbwa ni jamiii ya waangaza, wengine wasukuma,wengine wasubi n.k.

Kutokana na hayo naombeni mnisaidie kunipa historia ya kabila hili la wasubwaa japo halifahamiki ile kivileee.
Wasumbwa ni waha / wanyamwezi, waha walikuwa na kawaida ya kusafiri kutoka kwao kwa ajili ya kutafuta maslahi maeneo ya urambo na uyovu (runzewe) ikaja kutokea vita kati ya wayovu na milambo ya kugombea mipaka hiyo vita ikaamuliwa na ruhinda mtawala wa wasubi (biharamulo na chato) akawapatanisha hadi kuanza kuoleana MTOTO aliyepatikana kati ya muha na mnyamwezi naye akaanzisha lafudhi yake akikopa kwa waha wanyamwezi na wasubi kwa mfano salami anasalimu "katule" ambayo ni kama kinyamwezi au mwalala yewa ambacho ni kama kisubi na matambiko yao ni ya waha.wao hawapendi kuwalinganisha na waha ila ndo hali halisi.
 
Nimeipenda hii historia uliyoweza kunipatia sasa nimeanza kupata picha kamili maana hata wakati nipo urambo picha ya wasumbwa

Niliweza kuiona jinsi ilivyokuwa
 
Exactly, wangoni walitapakaa toka Songea hadi Kenya ila kundi dogo likajikata na kuweka masikani Kahama (Masumbwe, Runzewe-Geita kwa sasa) na Hawa ndo wasumbwa leo hii
Nimelewa sana kaka lakini mbona wanazungumza kisukumaa
Na kinyanwezi tuu.

Tofauti na kingoni
 
Hao wote ni walowezi kutoka kusini. Walipokuja Tanganyika waligawanyika sehemu mbali mbali

1. Wasukuma (maana yake kasikazini) hao inazungumzia wasukuma waliolekea pande za kaskazini (shinyanga na mwanza kidogo)
2. Wadakama (Wanyamwezi) Dakama means kusini (hawa waliweka maskani yao magharibi ya tz
3 Banakiya (wa masharikii) hii inajumlisha wanantuzu wote (bariadi na meatu)
4 Banamweri (hii inamaanisha magharibi) hapa utawapata wasumbwa, wasubi, Wazinza
Ukifuatilia hao wote kuna mwingiliano mkubwa sana katika lugha yao na kwa kiasi kikubwa wanaelewana (wasukuma, wanyantuzu,wanyamwezi, wasumbwa etc)
 
Wasumbwa ni Kabila la Watu kutoka eneo la wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita , Kaskazini mwa nchi ya
Tanzania .
Mwaka 1987 Idadi ya Wasumbwa ilikadiriwa kuwa 191,000 [1] .
Lugha yao ni Kisumbwa , jamii ya Kisukuma na
Kinyamwezi .
 
Back
Top Bottom